Hi video clip imenihuzinisha, tunakoendea ni hatari!

Shida ya serikali ni tozo tu, hakuna kingine.

Kama vipi waweke tu tozo ya stand ya Magufuli, kila basi linalovuka kuingia na kutoka Dar lilipie hiyo Tozo, ila kushusha na kupandisha itakuwa juu yao.
 
Ni system inayokulazimisha kwa hiari kufanya wanayotaka. utachelewa sana kuielewa Tanzania.
 
Kwamba,

Abiria anaenda Mbagala.

Bus linaenda Mbagala huko huko.

Lakini abiria anatakiwa kushushwa Mbezi apande daladala kwenda Mbagala wakati Bus na lenyewe linaenda Mbagala likiwa TUPU.

Aliyefanya haya maamuzi Ni CHOKO, ANAPULIZWA NYUMA
😂😂😂
 
Watu wakubwa wafungue Lodge za buku Kumi waache dili za matilioni hacha utani wewe

Kinachofanyika sio sahii unamlazimishaje mwenye bus Aishie mbezi wakati anaweza kufika Mpaka mbagala kushusha abiria

kosa la kiongozi mmoja husisingizie wote
Kuna mmiliki wa mabasi katika hiyo clip ndio amezungumza hayo mkuu
 
Kazi ipo
 
Mambo mengine kuyatetea ni upuuzi mtupu.

Inchi zote zinazojitambuwa huwezi kukuta abiria wanapanda mabasi uchochoroni.

Ni Kwa vile serikali yetu inaendeshwa Kwa mihemko ya mitandaoni.

Ni wakati sasa wa mabasi yote yawe sehemu moja.
Hii itapelekea watu wote hata wageni kutambuwa sehemu maalum ya kupata usafiri.
Muhimu ni kuwa na connection za usafiri kutoka pembezoni mwa mji kufika Magufuli terminal.

Wabongo tupunguze uswahili na ujuaji usio na msingi.

Mbona JNIA airport watu wanafika na kuondoka kwenda makwao bila kulalamika?
Mbona hawasemi airport isogezwe karibu na kwao.

Vitu vingine ni upuuzi mtupu kulalamika.
 
Nilihuzunika Kweli yule mama anasema anaishi mbagala na wenye basi wamesema wanawafikisha mpaka huko,,serikali inatakiwa ijue sio kila msafiri akifika mbezi anakuja kupokelewa na ndugu wengine hawana ndugu,,,na hawana nauli za zile taxi zao walizoeka pale,,,,we utoke na mizigo mpaka kwenye daladala umechoka hapo nauli ushatoa elfu 36 huko hatar sana wangeacha tu mtu wa hali ya chini ndie anayeenda kuumia hapa!!!
 
Jana Bashungwa ( Waziri wa TAMISEMI), alisema moja ya sababu ya mabasi kushushia abiria pale stand ya Magufuli ni pamoja na kukagua wageni kutoka nje ya nchi.

Wataalamu naomba mnisaidie, hivi foreigner anatakiwa akaguliwe mkoa alioanzia safari au anapoishia? Je, humo njiani hakuna checkpoint?

Tuchukulie mfano basi kutoka Kigoma, halikaguliwi lilipoanzia safari kubaini wageni na magendo zaidi ya kilomita 1200 mpaka lifike Dar stendi ya magufuli ndio likaguliwe?
 
Huu ni upumbavu wa kiwango cha PHD
 
Yaani tuko kwenye taifa la hivyo sana. Na watawala wameamua kufanya ujinga kuliko wanyama
 
Watu wamewekeza biashara zao hapo, maduka na magesti.., kwahiyo mnateswa kwa sababu hiyo.
 
Ma BUS yote yashushe hapohapo Stend.


Raia achague mwenyewe, Kulala hapohapo Stend mpaka pakuche au ajiongeze !!.


Raia hapaswi kubembelelezwa kwenye jambo kama Hili.
Mambo ya kukaa kwa shemeji raha sana. Toka ukatafute cha kwako uone kama utaropoka eti abiria waachwe stendi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…