Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hodiii
Karibu xana.....
Hii nayo kazi. Labda itafika mahali ikubalike kama ilivyo kwa upande wa saa. Saa 5:00, utaambiwa ni saa kumi na moja.!!! Na 12 ni 6!.
Kaka vipi salama, naona lugha imebadilika (xana)!!
Hicho ni kizungu cha kifipa.
hahahaaaah!!! Kaka umewahi kumsikia Mzindakaya akiongea ung'eng'e...??
Mimi sijawahi. Ila tungejivunia kiswahili chetu na kukifanyia kazi, mbona tungekuwa mbali sana. Wachina wenyewe wengi hawana mpango na ung'eng'e lakini wapo mbali vibaya mno
kweli kabisa mkubwa inabidi tukinadi kiswahili chetu, huu ulimbukeni wa kuiona lugha ya malkia ni bora kuliko kiswahili inatakiwa ipigwe vita kwa nguvu zote...
Kiongozi umesema sawa kabisa. Taifa hili limejaa maajabu. Unafaulu hujui kusoma wala kuandika, ukiongea kingereza unaonekana wa maana na umesoma.
Jamaa fulan alienda uingereza, kurudi akasema "wenzetu wameendelea sana. Yaani watoto wadogo kabisa wanaongea kingereza fasaha". Asijue kule ndio kwao na ndio lugha yao.