SoC02 Hichi Ndicho Kipele Cha UKIMWI ambacho Huonekana Mapema Mtu anapopata Maambukizi

Stories of Change - 2022 Competition

lonepair

Member
Joined
Nov 6, 2017
Posts
20
Reaction score
22
Kipele kinaweza kuwa dalili ya awali ya VVU, Lakini kirusi cha UKIMWI kinaweza kikasababisha aina mbalimbali ya vipele hivyo ni lazima ufahamu haya ambayo leo tunaenda kukufahamisha. Watu watakaotwa na kipele na akakumbuka kuwa alipitia kwenye vihatarishi vya kupata virusi hivi basi ni lazima atafute ufumbuzi kwa kuwahi kwenda kupima mapema.

Kirusi cha ukimwi kinaweza kikasambaa kutoka mtu A kwenda Mtu B kama maji maji ya watu hawa yatagusana. Maji maji haya ni pamoja na Damu, Shahawa, Maji ya ukeni na kwenye haja kubwa na maziwa.

Maji maji haya yanaweza kugusana pale mtu A anapojamiana na mtu B bila kinga au mtu A anapojikata na kitu chenye ncha kali kilichotumiwa na muathirika.

Kipele kipi kinahusishwa na ukimwi?
Kulingana na one source wamechapisha kuwa kipele kinachohusishwa na maambukizi ya awali ya ukimwi huwa hakina rangi au wakati mwingine huwa na rangi nyekundu yaani redish ambacho hakina maumivu yoyote wala hakiwashi.

Lakini tafiti nyingi zinaonesha kuwa kipele kinachoonekana kwa watu wenye maambukizi ya ukimwi kipindi cha awali hutokea kwa sababu inayoitwa seroconversion.bHii ni ile hali ya mwili kujaribu kupambana na kirusi na kuweza kusababisha hata mafua.

Hivi vipele pia huweza kutokea kama kirusi kingine tofauti na cha ukimwi kitaingia mwilini hivyo hakuna kipele kimoja ambacho kinaweza kuthibitisha kuwa mtu ana ukimwi kwa asilimia mia moja.

Dalili za kipele cha UKIMWI
Kipele kinaweza kuwa dalili ya awali kwa mtu alieambukizwa kirusi cha ukimwi. Hii ni dalili ya awali kabisa ambayo hutokea kati ya wiki ya kwanza na ya pili baada ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi. Kipindi cha awali au wiki moja hadi wiki mbili hujulikana kama hatua ya seroconversion.

Katika hatua hii ya seroconversion mwili hutengeneza antibody kwa ajili ya kirusi.Kati ya asilimia 80 hadi 90 ya watu walioambukizwa kirusi hiki katika kipindi hichi huwa na dalili ya mafua na baadhi yao huwa na kipele kwenye ngozi ambacho hakiwashi wala hakiumi.Mara nyingi kipele ni dalili pekee ya awali ya maambukizi ya ukimwi lakini kutokana na ukweli kwamba kirusi hushambulia kinga ya mwili basi dalili zingine huzalishwa ambazo ni pamoja na hizi hapa chini.

Dalili za awali za UKIMWI ambazo zinaweza kuambatana na kipele ni pamoja na: Maumivu ya misuli, kutetemeka inayoambatana na homa kali, Koo kuwasha, Kuvuja jasho usiku, Kujihisi vibaya mwilini, Tezi kuvimba, Vidonda mdomoni na kuchoka kupita kiasi.

Kulingana na jarida la center of diease prevention and control (CDC) dalili hizi hujitokeza kati ya wiki ya kwanza hadi ya nne baada ya kupata maambukizi na hudumu kwa siku kadhaa au wiki kadhaa.Mtu yeyote ambaye amekutana na hatari ya kupata VVU hapo nyuma akiona dalili hizi anashauriwa kutafuta ushauri wa kupima na ushauri mwingine unaomfaa.

Aina ya vipele vya VVU
Kama kipele kimetokea kama dalili ya awali ya kuambukizwa virusi vya ukimwi mara nyingi kitatoweka chenyewe kadri mwili utakavyokuwa unatengeneza antibody zinazopambana na virusi hivi.Lakini kama mtu hataanza matibabu ya kufubaza virusi vya ukimwi vinaweza vikatapakaa zaidi na kusababisha matatizo makubwa ya ngozi.

Kama kinga ya mwili itaendelea kudhoofika inakuwa rahisi sana kwa bakteria,fangasi,virusi na visababishwi vingine kushambulia kipele hicho.Aina ya vipele ambavyo vinaweza vikadhuru ngozi ni pamoja na:

Molluscum Erythema, furuncles and carbuncles, Warts,impetigo, mkanda wa jeshi cellulitis,scabies na maradhi mengine ya ngozi. Hivyo ni muhimu kupima kwani kipele peke yake hakitoshi kujithibitishia kuwa una kirusi cha ukimwi.

Hivyo basi ukiona kipele kimeota kwenye ngozi yako unapaswa ujitafakari kwanza kama je, katika kipindi cha nyuma umekutana na mtu ambaye humuamini ukafanya nae faragha au umejikata au kujichoma na kitu chenye ncha kali ambacho mtumiaji hajulikani.Baada ya hapo tafuta huduma ya vipimo kutoka kwa wataalamu wa afya walio karibu nawe.

#Credit:Medical news today&CDC
Mwandishi Loning'o Alais
Mawasiliano:0752937278 loningoalaisi@gmail.com
 
Upvote 2

Aisee!
 
Kuna mtu alikuja kuniomba ushauri akasema nimusaidie kujua afanye Nini inaama alilala namtu ambaye hazui status yake akasema alitumia condom Ila badae akaja kugusa majimaji yako kwenye condom na ilikuwa na damudamu Ila kwawakati huo hajashituka alikuja kushituka baada ya siku sita akahisi kuwa alielala naye siyo salama.
Akataka kwenda hospital apewe pep Ila masaa 72 alikuwa ashapita. Ko Mimi nilichomushauri nikwamba aende hospital aombe pep akaanze kumeza kwasiku28 baada kwamba japo masaa 72 amepita Kama alielala naye ni muasirika itaweze kumusaidia hata kidogo kuziwia maambukizi.

Nisaidieni nilimushauri sahihi?
 
Asihangaike na Pep wala Prep, asubiri wiki 2 akapime na kama ni positive mwàmbie aanze ARV fasta.
 
Back
Top Bottom