Ipo tofauti kubwa kabisa.Advance diploma ni course ambayo ilikuwa inatolewa kwenye bathi ya college na institutions mbalimbali ikiwa ni equivalent ya degree kabisa ambayo ukifaulu vizuri unaweza kwenda masters bila matatizo,SEMISTER ZIPO 6 likewise kwenye degree.na hata ukiangalia wahasibu wengi wa hazina na baathi kwenye wizara nyingine wengi wamesoma ADA na hata kazi zinazotangazwa utaona wanaandika adv dipl/degree.
Turudi kwenye Higher Diploma,kwa uelewa wanngu na nikilinganisha na baadhi ya mifumo ya elimu za kimataifa,ni elimu inayotolewa baada ya diploma pale mtu akishamaliza ordinary diploma yako unaweza soma higher diploma ambayo ni mwaka mmoja then degree mwaka mmoja kama kumalizia,ila ni mfumo tofauti na tuliozoea.ambayo mimi nahisi ni mfumo mzuri,kuliko mtu kusoma certificate labda ya accounts masomo yaleyale ya first year atayarudia diploma,akifika degree for almost two years atasoma yaleyale,mwaka wa mwisho ndo atasoma vitu vya undani kidogo,labda ubadilishe fani kwa kila stage!