Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Kwanza niwape pole wahanga wote wa ajali ya jana moshi mjini. Pili niseme kuwa jukumu kubwa usalama wa eneo lile lilikuwa la Mwamposa na waandaaji wa ile shughuli. Lakini najiuliza iwapo vyombo vya usalama (hasa polisi) hawakuwa na jukumu lolote kuhakikisha lile eneo ni salama?
Mtu anapoenda kuomba kibali cha kukusanyika, kabla ya kumpa hawataki kuhakikishiwa kuwa kutakuwa na wanaosimamia usalama?.
Naomba wale waliofanya uzembe jana na kuleta maafa wawajibishwe na pia tujifunze na kuweka utaratibu ili jambo kama hili lisitokee tena.