Hii back to school kwa Wanawafunzi Wajawazito imekaaje?

Tengeneza Njia

Senior Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
121
Reaction score
205
Nimeona kuna shule huko Mtwara mwanafunzi ameripoti na mtoto wake mchanga shuleni baada ya kujifungua, nawaza:

1. Muda wa masomo mambo yanakuwaje? Kuna mtu anakaa na mtoto nje na binti anaendelea kusoma?

2. Binti anapata nafasi ya kutoka toka nje/ au humo humo darasani kumnyonyesha kichanga?

3. Kuna msaada wa kisaikolojia, kimwili, akili etc. unatolewa kwa huyu mama mwenye mtoto maana process ya kupona tu kwa mzazi katika nyanja hizi, na bado aweke akili yake darasani, kumtunza mtoto mpya ukizingatia na yeye ni mtoto ni balaa!

3. Au kuna vyumba maalumu vya mama na mtoto kujisitili hapo shuleni?

4. Mwisho, au anafundishwa kwa wakati wake mwenyewe na sio kujichanganya na wengine?
 
Mkuu kunakuwa tu na baby sitters hapo shuleni ambao wanaajiriwa na serikali kwa ajili ya kuwaangalizia watoto watoto wao.Ikifika saa ya breki anaenda kunyonyesha.
 
Nimeona kuna shule huko Mtwara mwanafunzi ameripoti na mtoto wake mchanga shuleni baada ya kujifungua, nawaza...
Zianzishwe shule maalum kwa mabinti hawa na sio kuwafukuza au kuwanyima kuendelea na masomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…