Hii barabara ya Mpunguzi iliyopo Dodoma ina viraka vingi, iwekwe sawa kupunguza athari za majanga

Hii barabara ya Mpunguzi iliyopo Dodoma ina viraka vingi, iwekwe sawa kupunguza athari za majanga

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257

Dodoma: Hii ni barabara ya Mpunguzi iliyopo jijini Dodoma ni barabara ambayo yanapita magari kuelekea mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na mikoa mingine.

Ukipita kwenye barabara hii utakutana na vishimo vingi ambayo vinaweza kusababisha madhara ikiwemo kuharibu magari na kusababisha ajali.

Vishimo hivyo vina muda mrefu, hivyo madereva wengi wanaendesha kwa tahadhari kwa kuvikwepa vishimo hivyo.

Mamlaka zinazo husika, zinapaswa kuchukua hatua kuziba mashimo haya yalipo barabarani ili kulinda usalama wa watu wanaotumia barabara hii, hususan wanaotumia vyombo vya moto.
 
Back
Top Bottom