Hii biashara inanipa stress wallah!

kovidii

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
277
Reaction score
266
Nimekuwa mkulima wa miwa ya kuzalisha sukari katika Bonde la Kilombero kwa miaka kadhaa sasa ila kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita soko limeyumba kupita kiasi. Tatizo kubwa ni mwekezaji(kiwanda Cha sukari) kushindwa kuhimili wingi wa miwa ya wakulima wa nje (autogrowers).

Kwakuwa ni uwekezaji mkubwa na nguvu nyingi nilielekezea huko ilibidi nitafakari njia mbadala ya kuiuza miwa ile (ukizingatia mimi ni ni mkazi wa Dar, so hata usimamizi wa mauzo kule shamba unakuwa mdogo). Mwanzoni mwa mwezi March nikapata wazo la kuileta Dar kuiuza kwa wanaouza juice ya miwa. Nikaanza kufanya upembuzi wa kutafuta soko kwakuwa miwa ile iko tofauti kidogo kulinganisha na miwa iliyozoeleka kukamua juice hapa mjini.

Ilibidi nilete sample ya bidhaa yangu kwa wateja niliowakusudia, walionyesha kuikubali sababu miwa ile ina sukari zaidi ya hii waliyoizoea. Nikatafuta pia mahali pa kuweka mzigo wangu pindi nitakapoianza hiyo biashara. Baada ya kuona kila kitu kimeenda sawa wakati najiandaa kufuata mzigo ndo balaa la Corona likawa limepamba moto then kukawa na mfungo wa Ramadhan so ikabidi nitulie kidogo.

Baada ya hali kutulia na mfungo kuisha nikafanya safari. Kwa kuanzia nilipanga kuanza na angalau tani10, ili kama biashara itaenda vizuri niongeze ukubwa wa mzigo. Nilifanikiwa kukata na kupakia fuso, Jumapili tarehe 21/6 nikaingiza mzigo Dar.

Balaa lilianza kesho yake Jumatatu nilivyoanza ku-suplly mzigo kwa wateja wangu. Biashara haikuwa kama matarajio niliyokuwa nayo. Hadi leo ninandika thread hii mzigo uko zaid ya tani 7. Mbaya zaidi bidhaa hii baada ya siku 10 haifai tena kwa matumizi kwahiyo nikiangalia uchache wa mzigo ninaoupush per day naona kabisa mzigo hautakwisha na nitapata hasara.

Kinachoniumiza kichwa, matumaini yangu kama biashara ingekuwa vizuri hiyo hela ndo ingenisaidia kumsafirisha first born wangu shule this weekend. Kilichonisukuma kuandika uzi huu wakuu, ni imani yangu kwamba jukwaa hili lina aina zote za watu so kwa yeyote anayefahamu maybe mtu mwenye uzalishaji mkubwa wa Cane juice au popote kwenye kiwanda cha kutengeneza ethanol/spirit ili niiuze hii tani 7 kwa pamoja angalau niokoe gharama za msingi nilizoingia especially usafiri, labour charges etc.

Kwa yeyote mwenye kujua ufumbuzi wa hili jambo nahitaj msaada wake
Mwasiliano: 0624406434
Natanguliza shukrani!
 
Kwa kweli sina nijuacho kuhusu miwa lkn pole sana mkuu ila next time ukitaka kufanya kilimo bongo hii kumbuka kitu hiki:

Kilimo=Umaskini.

Mi huwa nikimuona mtu anahangaika kuwekeza kwenye kilimo huwa namuonea huruma sana..
Nchi hii kama kuna watu kilimo kinawatoa basi ni wachache sana!
 
Pole but first relax.....halafu mwambie Mungu akusaidie ,nimemuona Mungu akifanya mambo ambayo kwangu ilikuwa ni ngumu,lakini hata kwa yale niliyodhani ningeweza kufanya mwenyewe nilishindwa mpaka nilipomuomba Mungu msaada.
Mfano niliwahi kukosa wapangaji miezi3 mfululizo na nyumba ni classic ila nilipoomba wateja walimiminika from no where.


So muamini na mtegemee Mungu hakuna Neno gumu kwake,Siku moja kwa Mungu ni kama miaka 1000,so anaweza kufanya jambo within a second.....hii dunia tu unayoiona aliiumba kwa siku 5 tu siku ya sita ndo akamuumba mwanadamu,kifupi hashindwi na anatuwazia yaliyo mema.
 
Mkuu pole sana aisee,ila nikiri kwamba ulikosea mwanzo kukata tani 10 zote kwa ajiri ya wakamua juice.

Ilifaa uchakate hasara kati ya miwa kuendelea kukaa shambani au kukatwa na kukaa ndani.biashara zina zigzaga sana.

Wapumbavu badala ya kupigia kelele mambo yenye tija kama haya kwa maslahi mapana zaidi ya taifa,wanambwambwaja na democrasia.
 
Mi huwa nikimuona mtu anahangaika kuwekeza kwenye kilimo huwa namuonea huruma sana..
Nchi hii kama kuna kilimo kinawatoa basi ni wachache sana!
Sasa wote wakikimbia hali itakuwaje!!!

Hawa hawa wachache ndio wanalisha taifa hili,mpaka linajidai kwa kushiba,tuwatie moyo,hasa ukizingatia si kila wakati hali huwa mbaya hivi.
 
Mi huwa nikimuona mtu anahangaika kuwekeza kwenye kilimo huwa namuonea huruma sana..
Nchi hii kama kuna kilimo kinawatoa basi ni wachache sana!
Huo ni ukweli mchungu mkuu,kuna mtu anakwambia mpk rais mstaafu JK analima mananasi,mimi ni nani nisilime?hahah nawaambiaga wenzako wanafanya kilimo kama leisure tu/pa kwenda kupotezea muda weekend.,sasa wewe iga tu utalielewa somo kwa uzuri.
 
Na usiwasahau wale wapuuzi wanaosema nchi hii inategemea wakulima kwa 80% wkt huo huo wakiipa bajeti kiduchu kuliko maelezo huku wakisubiri Miujiza itokee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…