Hii Chuki inatokana na nini? Hili jambo limeusononesha moyo wangu

Hii Chuki inatokana na nini? Hili jambo limeusononesha moyo wangu

Mmoja ya madereva wetu amepatwa na shida kidogo ya kifamilia. Nikaona ni vyema kumtembelea jamaa huyu sababu namfahamu kitambo kabla hajawa dereva wa ofisini.yeye ndo alishiriki vizuri sana kunifundisha kiswahili miaka hiyo nafahamu kiingereza, kichina, kijerumani na kihispania.

Nimeenda mitaa anayoishi Masaki. nimeshtuka leo naendesha gari nawaona ducks. niliambiwa wanaitwa bata.kiuhalisia hawa nimekuwa nikiwaona tu kwenye movies na picha.

Basi kumbe wakati naondoka baada ya kuwaangalia na kupiga picha waliingia chini ya gari...sina hili wala lile nikakanyaga wawili.

Raia walipiga kelele mpaka mmoja kunikimbiza na pikipiki.mimi nilikuwa kwenye Merc Benz kama kawaida nimefunga vioo vumbi lisiingie.ndio anakuja kupark mbele yangu.nikamwuliza shida nini.akajibu nimeua bata.

Kiukweli hili liliniumiza moyo sana.nilimwomba turudi mpaka sehemu husika.haikuwa mbali kwenda nikakuta jamaa wamewawahi kuwachinja kabisa.

Basi nikauliza utaratibu unakuaje.ndio kunambia kuwa kwa wale bata wadogo kila mmoja natakiwa nilipe tsh 70,000. Nikatoa 300,000 nikawapa.na yule dereva wa boda boda aliyenifuata nikampa 50,000 ya usumbufu na mafuta.ingawa umbali toka sehemu ya tukio na aliponikuta ni kama hatua 30 tu.

Shida ilikuwa maneno magumu jamaa waliyoyatamka wakishutumu kuwa wenye magari wanadharau sana hawajali watu wengine tena mmoja akasema nilipopita hata sikuwasalimia.

Nilishangaa kusema nyie wenye vijihela mna jiona bora leo sasa ndo utatuelewa sisi nasi maeneo yetu.wengi walionekana kuwa na hasira ambazo sielewi zilitokana na nini.kijana mmoja tu ndio alionesha uungwana na kuwaambia mbona sikuwa nimeongea neno lolote baya.

Huyu alionekana kuwa na uwezo mzuri wa kureason.nilimwachia 50,000 aweke voucher anitafute siku moja tuongee.

Sifahamu kwa nini watanzania wengi wanapomwona mtu mwenye kauwezo kidogo wanamwona ni adui.hili nimeliona sehemu nyingi sana.wakisikia kuna mtu kafilisika wanafurahi.

Hawaangalii kwa kufilisika huyu wangapi watakosa ajira.kama nikiuza magari yangu au yakifa hawaoni kuwa mafundi wa dt dobie na cfao watakosa kazi? Je vituo vya mafuta vya total sisi wenye magari wote tukawa hatuna magari nani atanunua mafuta lita 60 na zaidi kwa week?hivyo kuna watu watakosa kazi.

Wanapokuwepo wenye pesa mzunguko unakuwa mkubwa.unadhani ukiniombea mabaya nikiacha kwenda supermarkets kubwa kubwa wale waajiriwa nani atawalipa?

Haya mambo yanategemeana sana kama hujaajiriwa direct na mwenye pesa unaajiriwa indirect.lakini ni wangapi tunasaidiana mfano gari zangu zote sita sasa ( nimeingiza Jeep last week) unadhani nani anaosha?

Anyway tusiombeane mabaya ndugu zanguni. Mimi nauza FORD RANGER unadhani kama wote ni makapuku nani atanunua? Si gari itaozea tu parking kwangu?

Kuna siku nilijisikia vibaya nipo sehemu nina FORD RANGER pale posta nimepark zile parking za Golden Tulip naenda nakuta kuna mtu mwingine pia anayo gari hiyo hiyo na Rangi zimefanana. Ndio siku niliyoamua kuiuza.

Nashukuru kuna Jamaa ofisini kanambia anaihitaji maana anadai ni kama imetoka Japan leo hii hii. Imetembea kms chache kwa maneno yake 38,000. Tyres mpya n.k

Tuishi kwa upendo nikipata mimi shukuru.na ukipata wewe nitashukuru.unadhani ningefanya nini hii gari kama ndio mimi peke yangu nina pesa wengine ndio hivyo tena?

Sisi wenye vijicent tunapenda tuwe wengi ili biashara zetu ziende vizuri maana nikiwa peke yangu kuna mambo nitakwama.tuache kuchukiana isipokuwa tuombeane mema.

Maneno ambayo walisema jamaa yalikuwa ya kusononesha sana walionesha chuki kwangu wakati sijafanya kosa lolote.
chuki imeanza kwa mwenye mkoa. Imeshuka kwa Raia
 
Hiyo ni kweli,kuna siku nilikanyaga deli LA mama mmoja LA kuwekea maandazi sikuliona bahat mbaya,wewewee wale kina mama walitaka kunigawana aisee!!
Ikabidi ninunue maandazi yote pamoja na hela ya kununulia deli jingine jipya!
 
Hakiamungu leo nimeamini huyu bwana kiduku anayoyahadithia hapa ni ya kweli kabisa sikuwahi kuwazaga. Mi ni shuhuda wa tukio zima jinsi alivyowagonga bata mpaka amefukuzwa na kulipa fidia yote. Nilkua nimevalia pensi nyeusi na flana ya kahawia sikua nafoka kama wengine nilkuwa kimya tu.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukio la kukanyaga bata lilirushwa Live kwenye TV,watu wengi walikuwa wanakulaumu kwa kuendesha ukiwa umelewa,ulikuwa unanuka pombe ya komoni,dereva ulikuwa ni ka mtu fulani kafupi sana kenye meno yaliyochomoza nje ya mdomo,na macho mekundu sana,alafu ile uliyokuwa anaendesha si ni Corolla humu nimeshangaa sana unasema ulikuwa anaendesha benz,
 
Back
Top Bottom