Hii game ya Usma na Berkane itakuwa kipimo tosha Cha uhuru wa CAF ya Motsepe

Hivi kosa la USMA ni nini mpaka waadhibiwe?
 
Daaah!! Wenzetu weupe hakika WANA MISIMAMO THABITI HASA.

INgekuwa hapa kwetu tungeacha tu kwa kigezo cha UTULIVU NA AMANI
 
Nami nakubali Caf ndio wenye shida jersey zinaweza kuwa na bendera ila sio ramani
Endapo Caf walijua kuwa hii jersey italeta shida walipaswa kuzuia isitumike kwa Algeria mi naona wako sawa
 
Mbona tayari USM Algers alishapokonywa point 3 na magoli matatu na hao hao caf baada ya mechi ya kwanza kule Algeria?
Sheria za mpila zipo wazi sana kiasi ambacho nyeupe huwezi kuiita nyeusi
Hata mtoano unapora mtu points? Hawa caf hawana akili toka lini mtoano ukawa na points?
 
USM hana sababu, ameshapigwa tayari
 
Maelezo yamenyooka sana, sasa hao USM nao wametoa sababu gani ya kutoingiza timu uwanjani! Hawajaenda kabisa Morocco au vipi!?
 
Maelezo yamenyooka sana, sasa hao USM nao wametoa sababu gani ya kutoingiza timu uwanjani! Hawajaenda kabisa Morocco au vipi!?
Mkuu wao hawaafiki kitendo Cha berkane kupewa ushindi wa 3-0 mezani, hata we ungeingiza timu kutafuta goli nne za jasho? Wakati mwenzako kapewa ya bure

Msimamo wa usm Alger ni kua mambo ya serikali hayamuhusu
 
Kweli ni ngumu kwenda kutafuta magoli manne. Kwa hiyo hawajaenda kabisa Morocco au sio
 
Wazee mmeandika uongo..ishu ipo hivi Algeria anaishutumu Morocco kusupport maseparist kwenye eneo la kybilia ambalo lipo ndani ya mipaka ya Algeria kwa kulipiza Algeria nae anaunga mkono uhuru kamili wa Jimbo la western Sahara ambalo Morocco anadai ni lake..
 
Hawajapeleka team uwanjani pale Morroco
Namaanisha ile mechi ya kwanza kule Algeria CAF waliwalima magoli matatu na kuwapa Berkane, swali langu kosa la USMA lilikuwa nini?
 
Namaanisha ile mechi ya kwanza kule Algeria CAF waliwalima magoli matatu na kuwapa Berkane, swali langu kosa la USMA lilikuwa nini?
Mi nadhani hapa ndio siasa za Caf ziliingia
Kosa la USMA ni kwamba jersey za Berkane zilizuiwa maana zilikuwa na bendera ambayo ni ishara mbaya kwa upande wa Algeria kutokana na migogoro Yao
Mamlaka za Algeria zikawaambia Berkane watafute jersey zingine wakagoma na hivyo hawakuweza kuingia uwanjani Caf wakawapa ushindi Berkane ambao hawakuingia uwanjani maana jersey zao zilitaifishwa kwa kuwa na ujumbe ambao sio mzuri kwa Algeria
Kuja huku Morroco USM wakagoma kuja nadhani Berkane atapewa ushindi acheze na Zamaleki
Ni upuuzi wa Afrikan football
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…