Hii gari itanigharimu shilingi ngapi mpaka kuitoa bandarini?

lukatony

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2011
Posts
667
Reaction score
523
Jamani naomba msaada kwa anayefahamu,kwa gari hii aina ya Toyota Harrier,itanigharimu shilingi mpaka kuitoa bandarini na kuwa nayo mkononi?na kwa wataalamu wa magari je gari hii ni si mtumiaji mkubwa wa mafuta?Msaada tafadhari!!!!!


[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100"]
[TR]
[TD] Model: [/TD]
[TD] TA-ACU15W [/TD]
[TD] CC: [/TD]
[TD] 2400 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Transmission (Gear): [/TD]
[TD] AT [/TD]
[TD] Color: [/TD]
[TD] Black/Silver [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Drive: [/TD]
[TD] 4WD [/TD]
[TD] Door: [/TD]
[TD] 5 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Steering Wheel: [/TD]
[TD] RHD [/TD]
[TD] Body Style: [/TD]
[TD] SUV [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Fuel: [/TD]
[TD] Petrol [/TD]
[TD] Mileage: [/TD]
[TD] 109000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Engine Type: [/TD]
[TD] 2AZ [/TD]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100, align: left"]
[TR]
[TD]
FOB Price:
[/TD]
[TD]
US$ 4,200
[/TD]
[TD]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Points Benefit:
[/TD]
[TD]
US$ 0.00
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Freight:
[/TD]
[TD]
US$ 1,050
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Vanning:
[/TD]
[TD]
US$ 0
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Inspection:
[/TD]
[TD]
US$ 300
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

Ya mwaka gani?
 
Low milleage: 50,000km
2001 model, VVTi engine,
2360cc, 4cylinders

Bei: 22m.

Call me at 0767-515333

 
Kwa uzoefu wangu gari ya 2001 m 22 sio kweli dubei awiri gari kama hiyo ni us3000 hasa ukizingatia, mwaka ni ya zamani sana

Duh mkuu unaongelea Harrier au Rav4.. hio dollar elfu3 hata Rav4 ya 1995 hupati. Siamini kama kweli una uzoefu na magari. Kumbuka Dubai gari zinatokea japan kwahio bei huwa ni kubwa zaidi na ukikuta bei ndogo jua gari mbovu hio..

Mie mwaka huu alone nishaagiza gari 9, wewe mkuu ushaagiza ngapi?
 

Kwa uzoefu wangu gari ya 2001 m 22 sio kweli dubei awiri gari kama hiyo ni us3000 hasa ukizingatia, mwaka ni ya zamani sana

Naapa kwa jina la Marehemu babu yangu hakuna Harrier ya 3,000USD.. Pengine binaadamu wenye uzoefu na pikipiki hudhani kuwa hata magari is the same price.


Samahanini kwa kuapa. Be serious jamani.
 
Kwa uzoefu wangu gari ya 2001 m 22 sio kweli dubei awiri gari kama hiyo ni us3000 hasa ukizingatia, mwaka ni ya zamani sana

Dubai Al Aweer gari kama hilo si bei hiyo,ila likiwa na 6 cylinder pamoja na 3000cc wawezapata kwa bei hiyo uliyosema mpaka $4500 maana Harrier ya sifa hizo sokoni zipo chini kutokana na demand ndogo ya wateja.Hiyo ya jamaa hapo juu sijui ni ya mwaka gani lakini kama ina uchakavu awe na 7.2ml kama kodi pekee bado gharama nyingine
 
kwa magari ya bei rahisi angalia hapa Japanese Used Cars | BE FORWARD. Hapa unaweza kuonesha kwamba gari linakuja Tanzania ktk bandari ya Dar es Salaam na utapewa CIF (gharama ya kulifikisha gari lako bandarini Dar es Salaam. NB: sina uhusiano na beforward na wala sifaidiki kipesa kwa kuwataja hapa.

Ukiingia katika website ya TRA unaweza download excel files zenye bei na jinsi ya kukadiria kiasi cha kodi utakacholipa. Hata hivyo kuna njia rahisi ya kukadiria kiasi cha kodi hapa Welcome to GariShwari (nao wanatumia viwango vya TRA)

Kwa specifics za gari uliyoweka hapa, inaonekana ni Harrier hybrid, hivyo jiandae na pesa isiyopungua milioni 25. Unaweza chagua haya hapa

All the best katika ununuzi (ukifanikiwa toa mrejesho hapa.....ahahaahah)
 
Naapa kwa jina la Marehemu babu yangu hakuna Harrier ya 3,000USD.. Pengine binaadamu wenye uzoefu na pikipiki hudhani kuwa hata magari is the same price.


Samahanini kwa kuapa. Be serious jamani.
http://www.beforward.jp./stocklist/make=1/veh_type=/fuel=/drive_type=/model=181/veh_type_sub=/steering=/mission=/fob_price_from=/fob_price_to=3500/mileage_from=/mileage_to=/cc_from=/cc_to=/color=/seats_from=/seats_to=/mfg_year_from=/mfg_year_to=/area=/dcper_min=/dcper_max=/keyword=/more_acce=2/view_cnt=25/page=1/sortkey=e/
Wewe acha kutudanganya fungua hapa kama hazipo,
 
Asante kwa kutoa ufafanuzi... ni sawasawa na tofauti ya bei kati ya same cars zenye engine ya D4 na VVTi.. huwa hawaelewi haya mambo kwahio ukiwatajia bei za magari hudhani wanaibiwa bila kufanya research
 
Naapa kwa jina la Marehemu babu yangu hakuna Harrier ya 3,000USD.. Pengine binaadamu wenye uzoefu na pikipiki hudhani kuwa hata magari is the same price.


Samahanini kwa kuapa. Be serious jamani.

Hahahaha, nimecheka sana! Harrier mbona 3000USD CIF ni bei ya kawaida sana kwa gari ya mwaka 2003 kushuka chini!!! Bei ya harrier inakuja kupanda ikitandikwa kodi za ajabu hapa bongo. Harrier ya miaka hiyo mpaka barabarani usilipe zaidi ya 17M.

Used HARRIER TOYOTA for Sale | BF232345 | Japanese Used Cars Exporter BE FORWARD
Used HARRIER TOYOTA for Sale | BF234133 | Japanese Used Cars Exporter BE FORWARD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…