Hii hali ilishakukuta na wewe?....

Nishawahi tafuta kalamu kumbe njmeichomeka kichwani. Nilipoenda washroom wakati nanawa ndiio naiona kupitia kwenye kioo cha washing basin.
 
Hahahahaha kuna mwamba usiku alikua anatafuta simu yake huku anatumia tochi ya simu hiyohiyo anaoyoitafuta.
Nadhani hua kunakua na fuse zimelegea kwenye ubongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka nimewahi kuagizwa nyama nikapewa elfu 10 nikiwa secondary basi kufika buchani sioni hela asee nilirudi natafuta njia nzima sijaiona kama nusu saa nikasema leo kipigo.
Ikabidi nirudi home kusema nikagombezwa vibaya sana nikapewa nyingine kufika buchani naiona ile 10 ipo kwenye mfuko wa shati na nilitafuta mwanzo sikuiona [emoji1][emoji1][emoji1].
Ikawa pocket money ya shule maana nishasemwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ile unachukua simu unataka kumpigia mtu (fulani ) ghafla unasahau ulitaka kumpigia nani...unabaki unatoa mboni tu...inakuwa baada ya dakika tatu au zaidi ndo unakumbuka...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…