TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
Katika maisha yangu yote sijawahi kuwa na marafiki,na sipendi kabisa masuala ya marafiki,hata nikipata tatizo sina rafiki wa kumwambia mtu pekee ninayeweza kumwambia ni mama tu.
Lakini pia si mtu mwepesi wakueleza hisia ama changamoto zangu kirahisi hata kwa mama,huwa namueleza nikiona kabisa hii inaniendea kombo.
Nikikaa na kundi la vijana wenzangu huwa nakuwa msikilizaji tu tena kwa muda flani tu kisha naondoka zangu.
Napenda kujitenga sana na ninaweza kukaa Siku nzima peke yangu bila taabu yoyote ile,nikitumia muda huo kufanya kazi zangu Za kiofisi au nikifanya coding ama kufanya simulation za sakiti mbalimbali kama nipo nje ya majukumu ya kitabibu.
Nikiona mtu anaanza kunizoea huwa namkwepa haraka sana maana sipendi mazoea na watu.
Sehemu ninayoishi wapangaji wenzangu inaweza pita miezi 2 hatuja onana.
Sipendi kabisa kwenda katika matukio ya sherehe na hata ikiwa ni lazima huwa nakuwa mtu wakujitenga sana maana Mara nyingi huwa siambatani na mtu kabisa.
Sipendi kupiga piga picha hovyo kabisa. Napenda sana familia hapo ndio nadhani ni marafiki pekee naweza kudumu não japo sina família.
Japo kuna wakati huwa nakuwa mpweke mno hasa nisipokuwa na na kazi ya kufanya ,hivyo huwa najitahidi kuhakikisha nakuwa na kazi Ya kufanya kila Siku.
Mimi napambana kivyangu na mambo yangu sipendi kumshirikisha mtu kabisa ,ila huwa nakuwa na hisia yakumshirikisha mke tu lakini sina.
Ninaamini kwamba kuwa na marafiki na kujichanganya sana na watu ni njia rahisi ya mimi kujiletee matatizo.
Nafikiria kuoa ili kuepukana na hali hii nadhani itanisaidia.