Hii hali inanisumbua sana. Nakosa amani moyoni

😵 😵 unahisi tatizo huwa ni nini?
Tupe experience yako yote ya utotoni
Kuna mtu ulikuwa unapenda umfurahishe/umridhishe kila wakati(mzazi/mlezi) mkali?? Uliteseka utotoni??

Mara nyingi watu waliokuwa na bad childhood experiences huwa wanaathirika ktk kujiamini na kujikubali mara nyingi hujihisi hawajapatia jambo au wakosefu
 
Kiufupi you are soft hearted and selfless, unajali kuhusu hisia za wengine na mara nyingi unatamani kuonekana upo right mbele za watu.
Mbaya zaidi hauna maamuzi ya faster na una tabia ya kupuuza vitu vidogovidogo till vionekane kuathiri mahusiano yako na hao watu. Ukifanya hivyo huwa unahisi kama watu wanakufikiria tofauti na ulivyo sio !!!!..

Hata mimi huwa inanitokea na amini tu mtu ambaye anakujua vizuri hawezi kukuchukulia tofauti kwa vitu vidogo kama hivyo na kama atafanya hivyo bhasi hastahili maelezo yako. Tena usijaribu kufix vitu, chukulia kama kusahau au kukosea kama binadamu, Don't be too hard on yourself mkuu
 
jacana said:
Kwa father ni sawa ila kwa mother ulikosea sana angalau ungelishuka kwa Toyo mkatembea wote
Hata kwa father niliona si sawa coz najihisi kama sijamheshimu.
 
Bora tu shule zifunguliwe mwende shule mkasome

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha msingi fanya mambo yako tu, mapema ukilijua hili itakusaidia Sana kaka, we Ni Kati ya Binadamu wachache Sana wenye moyo uliopondeka.. na usipo angalia utabeba Mizigo mpaka.. speaking out of experience
 
Client9 said:
Tupe experience yako ya utotoni
Kuna mtu ulipenda umridhishe kila wakati(mzazi/mlezi) mkali?
Uliteseka utotoni?
Haswaa mkuu.

Huwa sitaki kuona mtu anaumia kisa mimi ndo niliyesababisha. Kiufupi najali sana... hasa mama yangu sitaki kabisa kuona/kuhisi anaumia kwa sababu yangu.

Kuhusu utotoni nimetokea kwenye familia duni. Historia ni ndefu kidogo ipo siku nitaileta hapa.
 
Kijana hebu jaribu kuwa unafanya mazoezi Mara kwa Mara hii itakusaidia ubongo wako kuwa active vinginevyo uwe na notebook itakusaidia kurejea makosa yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…