Hii hali inanisumbua sana. Nakosa amani moyoni

Hii hali inanisumbua sana. Nakosa amani moyoni

😵 😵 unahisi tatizo huwa ni nini?
Tupe experience yako yote ya utotoni
Kuna mtu ulikuwa unapenda umfurahishe/umridhishe kila wakati(mzazi/mlezi) mkali?? Uliteseka utotoni??

Mara nyingi watu waliokuwa na bad childhood experiences huwa wanaathirika ktk kujiamini na kujikubali mara nyingi hujihisi hawajapatia jambo au wakosefu
 
Kiufupi you are soft hearted and selfless, unajali kuhusu hisia za wengine na mara nyingi unatamani kuonekana upo right mbele za watu.
Mbaya zaidi hauna maamuzi ya faster na una tabia ya kupuuza vitu vidogovidogo till vionekane kuathiri mahusiano yako na hao watu. Ukifanya hivyo huwa unahisi kama watu wanakufikiria tofauti na ulivyo sio !!!!..

Hata mimi huwa inanitokea na amini tu mtu ambaye anakujua vizuri hawezi kukuchukulia tofauti kwa vitu vidogo kama hivyo na kama atafanya hivyo bhasi hastahili maelezo yako. Tena usijaribu kufix vitu, chukulia kama kusahau au kukosea kama binadamu, Don't be too hard on yourself mkuu
 
jacana said:
Kwa father ni sawa ila kwa mother ulikosea sana angalau ungelishuka kwa Toyo mkatembea wote
Hata kwa father niliona si sawa coz najihisi kama sijamheshimu.
 
Heri ya Eid Mubarak wanaJF!

Nipo hapa sina amani. Jioni hii nilitoka home nikaenda kitaa kuzunguka kidogo, wakati wa kurudi njiani nikakutana na baba yangu mdogo tukaja hadi home.

Kinachonikosesha amani ni kwamba huyo baba yangu mdogo alibeba mfuko wa mahitaji madogo madogo kutoka dukani ambapo tuliongozana wote akiwa anaubeba yeye.

Baada ya kufika nyumbani nikakumbuka kwamba kwanini sikumpokea ule mfuko?

Kisa cha pili kinachoniumiza kwa muda kila nikikikumbuka ni kwamba kuna siku (mwaka 2018) dereva alitupakiza kwenye piki piki (tupo wawili na dereva wa tatu) tukaja tukamkuta mother njiani tukampita; nyumbani kuna umbali wa kama dakika 10 kwa mguu.

Baada ya kufika home nikakumbuka kwanini sikushuka ili mama apande?

Kiukweli hii hali imekuwa ikinitokea kila mara ambapo inanikosesha amani. Hata nikisahau kidogo ila nikimwona huyo mtu najikuta nakosa amani na kujiona kwamba nimemkosea sana.
Bora tu shule zifunguliwe mwende shule mkasome

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha msingi fanya mambo yako tu, mapema ukilijua hili itakusaidia Sana kaka, we Ni Kati ya Binadamu wachache Sana wenye moyo uliopondeka.. na usipo angalia utabeba Mizigo mpaka.. speaking out of experience
 
Client9 said:
Tupe experience yako ya utotoni
Kuna mtu ulipenda umridhishe kila wakati(mzazi/mlezi) mkali?
Uliteseka utotoni?
Haswaa mkuu.

Huwa sitaki kuona mtu anaumia kisa mimi ndo niliyesababisha. Kiufupi najali sana... hasa mama yangu sitaki kabisa kuona/kuhisi anaumia kwa sababu yangu.

Kuhusu utotoni nimetokea kwenye familia duni. Historia ni ndefu kidogo ipo siku nitaileta hapa.
 
Mkuu tatizo ni kwamba, huwa sikumbuki ila baadae mwishoni baada ya tukio ndio akili inafunguka na kukumbuka kuwa hivi kumbe sikumfanyia kitu fulani muhusika?

Yaani mkuu mwanzo huwa sikumbuki kabisa ila mwishoni ndo nakumbuka na hapo ndo penye tatizo.
Kijana hebu jaribu kuwa unafanya mazoezi Mara kwa Mara hii itakusaidia ubongo wako kuwa active vinginevyo uwe na notebook itakusaidia kurejea makosa yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom