Hii hali ya corona Tanzania tumejifunza

Hii hali ya corona Tanzania tumejifunza

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Hatuko huru kuchagua viongozi tunaowapenda. Mfano tu uchaguzi wa marudio wa Mbunge wa Kinondoni. Uchakachuaji ulikuwa dhahiri. Ilipelekea maandamano yaliyofanywa na raia kuonyesha jinsi ambavyo hawakubaliani na matokeo. Polisi walivamia maandamano yale na kifo cha Akwilina kilitokea. Uongozi wa Chadema uliishia kwenda gerezani.

Afande Muroto alisema atakae andamana atapata kipigo cha mbwa koko. Maandamano katika nchi zenye demokrasia ndiyo njia ya kufikisha ujumbe. Sisi tunatishwa na tunabaki kuwa waoga.

Hivi vifo vinavyotokea vitufunze kuwa tukiacha kuandamana maamuzi mabaya ya viongozi wetu yataletea vifo pia. Hiki tunachopata sasa hivi ni zaidi ya kipigo cha mbwa koko.

RIPuzi wangu ninajia huna maisha marefu.
 
Chadema mtaongea kila lugha ila Ndio kwisha Habari yenu
tapatalk_1588071371291.jpeg


Wanaojielewa wanaenda Nccr mageuzi

Sacos anabaki nayo dj
 
Umenena dada. Huwa nawaambia watu huandamani kwa faida ya Mbowe. unaweza kuona haikuhusu ila ipo siku yako tu. Leo hii madaktari wanatamani tuseme zaidi ya hapa kwa ajili yao
Nafikiri shida wewe huwa unawaambia watu hivyo, lakini na wewe unabaki kuwa Kama wao.
Hakuna hatua zozote unazochukua za kuishi Maneno yako.

Maandamano yanaweza kuanza na mmoja. Wewe andama alafu utaungwa mkono mbele ya Safari. Lakini ukiwaambia watu namna hiyo wakt kichwa umeinamisha kwenye keyboard, somo lako litaendelea kuwa gumu kueleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom