Hii hali ya kujisikia homa nyakati za usiku hasababishwa na nini?

Naxria abdalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2025
Posts
204
Reaction score
379
Kila usiku ninapokaribia kulala, napata hali kama ya homa na nahisi baridi. Kichwa kinakuwa kizito kana kwamba nataka kutapika, lakini siwezi kutapika. Wakati mwingine ninajisikia kama kizunguzungu na hali hii huambatana na hofu kali isiyoelezeka.

Hali hii imenitesa sana na imenifanya nisiwe na amani. Naomba kujua nini hasa husababisha hali kama hii, kwa sababu inanisumbua sana
 
Kapime
 
Anza kukagua mazingira unayolala je ni salama kuna hewa ya kutosha ndani kama umejirishisha na mazingira then nenda hospital.
 
Nenda hospitali kapime damu yako itakuwa na infection then utapewa dawa...
 
Mkuu tangu umeanza kuulizia kuhusu hali yako kiafya hukufuatilia zaidi kwa vipimo?
 
Mwili wako unaǰuaje kama muda huo ni usiku ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…