mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 8,860
- 11,554
Hili ni bonge la idea ila bila mtaji ni ngumu kulitekeleza.Habari JF
Mimi kama mwanafunzi wa chuo kikuu, leo hii nimeamua kuwasaidia wanafunzi wenzangu kwa kuwapa mpango mzuri wa biashara.
Usishangae sana, uzuri? Wa mpango huu wa biashara unaweza kuanza bila mtaji kabisa. Yaani ukaanza kwa uwezo wako mzuri wa kufanya mawasiliano kupitia smartphone yako.
Kupitia uwezo wako wa kuongea na kuhamasisha.
Kwanza naanza kwa kukupa tatizo na jinsi ya kusolve.
Twende champion!
Hivi umeshawai kwenda mahali hapa Dar es Salaam, ukakuta hakuna huduma muhimu kama maduka mpaka ukajiuliza hivi hawa watu huwa wananunua wapi nyanya?? Karoti?? Bamia nk??
Nina imani umeshawai kuona jamii ya namna hivyo, mara nyingi maeneo ya hivyo yametawaliwa na high na middle class..yani watu wa hali ya juu na kati wengi ni matajiri..na kuna wale wa tabaka la kati .
Sasa unachotakiwa kufanya wewe ni kusambaza huduma.hakuma kitu anapenda binadamu kama kuonekana wa thamani hata kama hana kitu.
Sasa unaweza kufanya biashara nyingi, ila leo naanza na hizi fast moving product yaani bidhaa zinazotembea na kutumika kila siku.
Usishangae sana.
Hapa unaenda kuanzisha kitu kinaitwa Mobile Genge, au genge la mtandao.
Unachokifanya wewe, ni kwenda nyumba hadi nyumba kuomba order juu ya maemezi ya kesho..
Dili na vitu common kama nyanya, viazi, ndizi, pilipili nk.
Baada ya mtu kukupa order wewe unaenda ilala kuchukua mzigo limited kutokana na watu wali request aisee utapiga pesa balaa. Na hutokuja kupata hasara
Ukimaliza kuwa karibu na wateja wako utaunda kikundi cha whatsap kila mteja atatoa oda yake humu..
Mambo ya kuzingatia
Kila nyumba utakayo toa huduma hakikisha ni nyumba ya kishua kuna fense kali yani kwa madoni, wao wanapenda kuletewa.
Hakikisha unamuelezea mteja wako vizuri akuelewe na ahitaji bidhaa yako usiforce...
Komqa baadae tafuta usafiri wako, ukiwa vizuri nunua toyo unanunua vitu then unatembeza kwa wateja wako wanachagua
.
Naendelea vizuri kwa sasa.
Maoni yote yanaruhusiwa wazeee wa kutukana uwanja ni wenu.
Linahitaji mtaji mkubwa kwenye mambo yafuatayo
1.Stock yako inahitajika iwe kubwa yaani minimum uwe na mazaga ya milioni 5 kila siku.
Fikiria kwa mfano mshua mmoja tu anachukua mazaga ya kutumia wiki 2 sasa kama mtaji wako wa kuungaunga utaweza kuhudumia mtaa mzima?
2.Unahitaji gari yenye closed body la cold room kwa ajili ya kuhifadhia stock yako ili hata isiponunuliwa kwa wiki nzima itakuwa bado iko fresh tu.
Sasa umebeba nyanya na bamia kwenye ndoo ukakosa wateja kwa siku 2 hizo zitaharibika ni hasara kwako,lakini mbali na hivyo washua wanajali sana hygiene yaani mazingira ya usafi ni lazima uzingatie hayo ili wakuelewe huwa hawapendi kufanya mchezo wa afya zao.
Ukiweza kufanya hayo ubilionea unakuita japo unahitaji ubunifu wa mara kwa mara maana ukishaanza kutoboa kuna wabongo watacopy na kupaste wazo lako halafu wauzaji mtakuwa wengi mtaani kama yeboyebo.