Hii hapa biashara bila mtaji

Hili ni bonge la idea ila bila mtaji ni ngumu kulitekeleza.
Linahitaji mtaji mkubwa kwenye mambo yafuatayo
1.Stock yako inahitajika iwe kubwa yaani minimum uwe na mazaga ya milioni 5 kila siku.
Fikiria kwa mfano mshua mmoja tu anachukua mazaga ya kutumia wiki 2 sasa kama mtaji wako wa kuungaunga utaweza kuhudumia mtaa mzima?
2.Unahitaji gari yenye closed body la cold room kwa ajili ya kuhifadhia stock yako ili hata isiponunuliwa kwa wiki nzima itakuwa bado iko fresh tu.
Sasa umebeba nyanya na bamia kwenye ndoo ukakosa wateja kwa siku 2 hizo zitaharibika ni hasara kwako,lakini mbali na hivyo washua wanajali sana hygiene yaani mazingira ya usafi ni lazima uzingatie hayo ili wakuelewe huwa hawapendi kufanya mchezo wa afya zao.
Ukiweza kufanya hayo ubilionea unakuita japo unahitaji ubunifu wa mara kwa mara maana ukishaanza kutoboa kuna wabongo watacopy na kupaste wazo lako halafu wauzaji mtakuwa wengi mtaani kama yeboyebo.
 
Nashukuru sana kamandq
 
kwa namna yoyote wazo lako linahitaji utafiti wa hali ya juu....watu wa eneo hilo wanajishughulisha na nini na wanafanya akzi maeneo gani wanapendelea nini..ni wazo kali sana ila pia mtaji unahitajika....
 
Biashara bila mtaji then nunua Toyo , toa ushauri wa kupata Toyota bila mtaji!! Biashara bila mtaji ni biashara ya ukahaba tu mkuu ,tena sio kivile lazima pia awe na pamba za kiaina.
Angeandika tu
Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwennyewe
 
heading na ulichokizungumza ni vitu viwili tofauti uko chuo ndio mnafundishwa hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…