Hii hapa hukumu ya Kiswahili iliyotolewa na aliyekuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Mh. Galeba

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Nimeisoma hukumu hii na kwa maoni yangu JPM ametenda haki kumpandisha cheo.

Aidha nitoe rai kwa vyuo vyetu vikuu vione namna ya kutambua mchango wa Jaji Galeba wafikirie kumpa Udaktari wa heshima.
 

Attachments

Ningeshauri wapewe udaktari wa heshima raia wote wanaohangaika kutengeneza dawa za Corona asilia, wao ndio wanamchango mkubwa zaidi kwa jamii kuliko huyo alieandika hukumu kiswahili.

Sasa hivi tanzania kuna ufumbuzi wa zaidi ya dawa asilia 1,000 za Covid 19 zinazopigiwa Promo. So unaweza kushangaa zikatakiwa kutolewa "DOCTORATE ZA HESHIMA" kwa raia 3,500 nchi nzima. Mpaka Corona iishe raia wanaweza kufika 5,000 wenye Doctorate Za Heshima. Alievumbuwa "NYUNGU" apewe u "PROFESSOR" kabisa.

Ila chonde chonde kuna siku tutakuja kunyweshana sumu.
 
Hahaha!

Huyu mdingi atakuwa kasoma Kantalamba....

Itakuwa alikuwa anawaza kwa Kiswahili halafu anaweka maandishi kwa Umombo...
Unaweza hisi ni nakala fake. Utafikiri yuko kwenye debate za education is better than money. Japo kiingereza siyo usomi lakini hii kwa jaji haikubaliki.
 
Mkuu nimeipitia niyakawaida tofauti ni Lugha tu ila kumpa Ujaji niswala la utashi wa ksiasa.
 
mimi pia napongezs watooe hukum kwa kiswahil.kwa yale maneno ambayo yahitaji ufafanuz unayatafsir tu.kuna ishu ilitokea kwamba kesi isiklizwe upya.ila ilo neno sasa la kilatin balaaa.
 
Jaji alikua na bahati tu maana hiyo siyo hukumu ya kwanza ya mahakama ya juu kwa kiswahili .

Ipo hukumu ya mahakama ya rufani iliyoandikwa kwa Kiswahili ilikua inahusiana na ule mvutano wa kama YESU ni Mungu ama la?

Nadhani mnakumbuka ishu ya DIBAGULA.

Kwahiyo bahati ilimuangukia kama dodo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…