Hii hapa mikoa inayotegemewa na TRA kwa mapato ya Kodi

hii ni ishara kwamba, ukiacha dar kodi nyingi za tra zinapatikana mipakani...

kilimanjaro, arusha, songwe, tanga zote ziko na boda...
 
arusha, kilimanjaro, tanga, songwe, kagera, mara wana boda...

mwanza, mbeya, morogoro, mtwara?.....

dar na pwani wana viwanda vya kutosha...

dodoma, maduka ya vifaa vya ujenzi...
 
hii ni ishara kwamba, ukiacha dar kodi nyingi za tra zinapatikana mipakani...

kilimanjaro, arusha, songwe, tanga zote ziko na boda...
Utaratibu wa ukusanyaji hauko fair.

Ni ajabu kwamba kiwanda Cha bia Kiko Mbeya ila Kodi inatozewa na kuhesabiwa Dar.

Benks Zina matawi Nchi nzima ila malipo ya Kodi yanahesabiwa HQ ambazo ziko Dar.

GGM Kodi yake inalipiwa Dar wakati mgodi uko Geita.

So mpaka hapo inaonekana Dar inaongoza lakini sio Kwa uhalisia .
 
Ndio maana nikasema ni vyema TRA ikaanzisha madawati ya qalipakodi wakubwa huko huko mikoani.

Takwimu za Kodi hazitoi picha halisi ya mchango wa Kila Mkoa sana sana inaendelea Dar.

Picha halisi ya mchango wa Mkoa kwenye Uchumi ni Kupitia GDP.
Si tulishakubaliana Tanzania ni nchi moja hakuna kutoa takwimu za kudhalilishana?

Na tukaanza na NECTA? Keki ya taifa inagawanywa centrally; Tanzania ni moja tuache ubaguzi wa kipato!
 
Sisi mara hatuna ligi na mtu ila kila mwaka hatukosekani top 10 na haturingi wala.
 
Mwisho orodha hii sio rasmi Bali ni Kwa Ajili ya discussion tuu ya hapa JF Kwa sababu haitoi picha halisi maana Walipaji Wakubwa wa Kodi hulipia Dar licha ya kwamba miamala imefanyika Nchi nzima mfano Banks,Migodi kama GGM ,Viwanda vya Bia ,Soda nk.
Si ndiyo nikawa nashangaa yaani Shinyanga hatumo pamoja na kuwa na migodi ya madini ya Bulyang'hulu, Buzwagi na Mwadui? Halafu Kagera ambayo inasemekana watu wake ni maskini mbona inategemewa na tra?
 
Si ndiyo nikawa nashangaa yaani Shinyanga hatumo pamoja na kuwa na migodi ya madini ya Bulyang'hulu, Buzwagi na Mwadui? Halafu Kagera ambayo inasemekana watu wake ni maskini mbona inategemewa na tra?
Buzwagi ni mashimo tuu hakuna mgodi tena walisomba Madini mkaachiwa mashimo Hadi yameisha.

Pesa zimepelekwa Dar,Dom & Arusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…