Hii hapa true stori ya lile sanduku la agano la bwana; the misery unsolved

Raphael Mtui

Member
Joined
Nov 26, 2024
Posts
78
Reaction score
204
Ilikuwa jioni ya tarehe 9 mwezi Av (tano) mwaka 3175 kwa kalenda ya Kiebrania (Hebrew Calendar) sawa na mwezi July au August mwaka 587 kabla ya Kristo kwa kalenda yetu.

Mkuu wa majeshi ya jeshi kubwa kuliko yote duniani kwa wakati huo aitwaye Nebuzaradani kutoka Babeli, alikuwa ameingia ndani ya Hekalu la Sulemani pale jijini Yerusalemu.

Alipoingia tu, akakutana na tukio ambalo hata wewe ungeona ungestaajabu mno! Alishangaa kuona damu ikitokota kutoka sakafuni kule hekaluni.

Yaani, damu ya binadamu ilikuwa inapanda kutoka ardhini bila kukatika! Iliogopesha, pia ilifadhaisha sana!

Na usifikiri kwamba damu hiyo ilikuwa imeanza asubuhi ya siku ile.

Turudi nyuma mpaka miaka 250 iliyokuwa imepita.

Sehemu hii ambayo damu ilikuwa inapanda kama maji ya chemchem, palikuwa pamefanyika tukio la mauaji.

Narudia, miaka 250 iliyokuwa imepita!

Kuhani mmoja kwa jina Zakaria Yehoyada, ambaye baadaye Mungu alimbadilisha na kumfanya kuwa nabii, alikuwa akiwakemea Waisraeli kwa dhambi walizokuwa wanafanya juu ya Bwana.

Unabii wake haukupokelewa vizuri, hata mfalme mwenyewe Yoashi na makuhani hawakuufurahia.

Likapangwa tukio, nabii huyu akauawa kwa kupigwa mawe hadi akafa.

Mauaji haya hayakufanyika mitaani, yalifanyika ndani kabisa ya hekalu la Yerusalemu, au tuseme, mbele za Bwana!

Hebu tuone tukio hili:

2 Mambo ya Nyakati 24:20-22 (KJV)
20 Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi.

21 Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya Bwana.

22 Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA NA AYAANGALIE HAYA, AKAYATAKIE KISASI.

Ingawa hutokea mara chache mno nabii wa kwenye Biblia kuacha neno baya ikitokea ameuawa, lakini Zakaria aliacha 'laana' fulani ya kwamba kuuawa kwake kulipwe kisasi na Mungu.

Balaa likaanza pale pale, siku hiyo hiyo walipomwua.

Hata baada ya kutoa maiti yake pale, lakini damu ikaendelea kutoka ardhini kama chemchem ya maji isiyokauka.

Usafi na mbinu zote 'hazikufua dafu.'

Hekalu liliendelea kunajisika!

Hali ile ikadumu miaka ya kobe, mpaka miaka mia mbili na hamsini iliyofuata, hadi kwenye hii tarehe ya leo!

Nebuzaradani anauliza, "Ni nini maana ya damu hii ya kutisha tena hekaluni!"

Makuhani wakajaribu kumdanganya ili kuficha hiyo kashfa!

Nebuzaradani akawapiga mkwara mzito, akawaambia wasiposema ukweli, atawatoboa-toboa nyama za miili yao kwa kutumia chanio kubwa la chuma!

Makuhani wakamwambia: "Kulikuwa kuna nabii mmoja hapa alikuwa akigombeza watu mara nyingi sana, viongozi wetu enzi hizo wakaamua kumwua, na tangu wamwulie hapa, damu yake imekuwa haiachi kupanda kutoka ardhini!"

Wakamweleza kuwa nabii yule alitangulia kutabiri kwamba Hekalu la Sulemani (Hekalu la Yerusalemu) litabomolewa kabisa.

Nebuzaradani kusikia hivyo, akaapa kusema 'Leo nitamtuliza Zakaria, na damu hii itakauka leo'.

Akiwa na makamanda wake, akakamata wanafunzi wa chuo cha Torati akawaulia pale, lakini damu ya Zakaria haikukoma.

Akaenda kukusanya watoto wa shule, akawaua hapo hekaluni, lakini damu ya Zakaria ikaendelea kuchemka kama kawaida.

Akaenda kuleta makuhani vijana, akawaua, lakini damu ya Zakaria haikukoma.

Nebuzaradani kuona vile akaanza kuua kila mtu, kuanzia kuhani mkuu wakati huo, viongozi wote, na wananchi, akaua mpaka wakafika watu elfu tisini na nne, lakini damu ya Zakaria haikukoma!

Nebuzaradani kuona hivyo, akaenda pale damu inapochemkia, akapiga kelele kwa sauti akisema: "Zakaria! Zakaria! Nimeshaua wakuu wote, bado unataka niue nimalize watu wote kabisa??"

Hapo hapo damu ya Zakaria ikakoma!

Baada ya Nebuzaradani kumaliza pale, akaanza rasmi kuharibu nyumba ya Mungu, yaani Hekalu la Yerusalemu, au kama tuliitavyo, Hekalu la Sulemani.

Dunia nzima wakati huo, hakukuwa na jengo kubwa na la kifahari la mambo ya ibada linalozidi ukubwa na ufahari wa Hekalu hili.

Hili ndilo lile Hekalu lililojengwa na Mfalme Sulemani, na ndio tunaliita Hekalu la Kwanza.

(Habari yote ya Ujenzi wa Hekalu hili na Ikulu soma 1Falme sura ya tano na ya sita).

Hekalu hili lilikuwa ndio fahari kuu ya Israeli, na lilijizolea umaarufu duniani kote. Hakukuwa na hekalu duniani kote lililokuwa kubwa kuzidi jengo hili.

Habari za hekalu hili kila mtu hapa anazijua.

Kwa miaka mingi, manabii wengi kwenye Bibkia tunaona walivyokuwa wametabiri kwamba kuna siku taifa la Yuda watavamiwa na taifa kubwa duniani, na watafanya maangamizi makubwa sana, na kubwa zaidi WATAHARIBU HEKALU!

Ujumbe ama unabii huo ulipuuzwa kabisa na Wayahudi kwani HAWAKUWEZA KUAMINI KAMA MUNGU ANAWEZA KURUHUSU TUKIO BAYA NAMNA ILE LITOKEE, TENA MAHALI PAKE ANAPOKAA NA KUSEMA MOYO NA MACHO YAKE YAMO HUMO.

Kwanza, ilionekana kama ni kufuru kutabiri jambo kama hilo. Lakini tunajua Mungu alishasema mapema hatajali, kama Waisraeli hawajali kutii amri zake.

Unabii huu ndio ulikuwa unatimia leo.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu, majeshi ya Mfalme Nebukadreza yakiongozwa na Nebuzaradani, yalikuwa yametawala nchi nyingi na kufanya uharibifu mkubwa wa kivita.

Nchi za jirani na Israeli walikuwa 'wameshaona cha mtema kuni.'

Sasa, majeshi yalikuwa yamefika Yerusalemu, na wakaamua kuwatesa watu kwa namna ya kikatili sana.

Kwanza, walizunguka tu mji wa Yerusalemu, ikawa hakuna mtu anayethubutu kutoka au kuingia. Walikaa muda mrefu nje ya ukuta wa Yerusalemu, wakazingira mji KWA MUDA WA MWAKA MMOJA NA NUSU!

Huduma za maji na chakula zikawa balaa! Hakuna chakula kinaingia mjini wala huduma zozote.

Majeshi yalijikalia pembeni kuuzunguka ukuta wa Yerusalemu bila kufanya chochote, ila watu wanajifia humo ndani kiulaini kwa njaa!

Sasa, baada ya mwaka mmoja na nusu, majeshi ya Nebukadreza yakavunja ukuta na kuingia mjini, kazi ikawa ni kuua wananchi na kuchoma moto majumba yote huko mjini.

Mpaka wanafika tarehe hii niliyoitaja, ndio Nebuzaradani anaingia Hekaluni akiwa na majeshi yake, ili waone kama kuna kitu cha maana cha kuiba kwanza kabla hawajachoma moto Hekalu la Mungu Aliye Hai.

Tukumbuke, katika Hekalu kulikuwa na vyombo vingi sana vya thamani, vya dhahabu tele, na kupitia kitabu cha Danieli tunajua majeshi haya yalichukua vyombo hivi vya Bwana na kuvipeleka Babeli kwa mfalme Nebukadreza.

Nebuzaradani alipoingia, ndipo alikutana na habari ambayo nimeieleza hapo juu ya damu ya Zakaria na alipomaliza operation ile, ndipo kazi ya kuchoma na kuharibu Hekalu ikaanza!

Moto ukashika kasi ya ajabu! Hekalu likawa limeanza kuteketea rasmi majira ya jioni. Kutokana na Hekalu kuwa kubwa mno, liliungua kwa siku nzima hadi kesho yake jioni.

Huzuni kubwa mno kwa taifa la Yuda na Israeli kwa ujumla!

Mungu wao yuko wapi!

Kikundi cha makuhani vijana ambao walikuwa wakishika funguo za kile chumba cha Patakatifu pa Patakatifu, ambapo ni Kuhani Mkuu pekee ndiye alikuwa akiingia humo tena mara moja tu kwa mwaka, siku ya kitaifa ya Upatanisho (Yome Kippur) kila tarehe 10 mwezi wa saba kwa kalenda ya Kiyahudi, walisogea eneo la tukio.

'Waseminaristi' hawa walipanda juu ya paa la Hekalu lililokuwa likiteketea, wakapiga kelele wakisema: "Bwana wa Ulimwengu wote! Kwa kuwa sisi hatuna tena haki ya kumiliki Patakatifu pa patakatifu, chukua funguo zako".

Wakatupa funguo zile kuelekea Mbinguni.

Habari za kuaminika zinasema kulitokea mkono uliodaka funguo hizo na kutokomea nazo huko angani!

Kisha, kikundi hicho cha makuhani vijana wakajitupa kwenye moto, wakateketea!

Nebuzaradani aliua watu wengi mno jijini Yerusalemu, jumlisha waliokufa kwa njaa, kwa upanga wake, walifikia milioni kadhaa!

Dunia nzima ilinuka damu siku ile!

Ule unabii wa Isaya kwamba siku hii ya leo wanaume watauawa kiasi ambacho wanawake watakosa wa kuwaoa, ulitimia.

Tukio hili liliua wanaume karibu wote kabisa na wengine kupelekwa uhamishoni Babeli.

Hiki ndio kipindi ambacho wanawake walikuwa wakimng'ang'ania mwanaume mmoja wakiomba wazae naye tu, suala la matunzo kwa mama na mtoto mwanaume hatodaiwa chochote kabisa. Gharama yake ni alale nao tu wapate 'mbegu', basi.

Isaya 4:1
Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.

Hekalu lilianza kuungua na kuteketea rasmi tarehe 9 Av (mwezi wa tano) mpaka kesho yake.

Mpaka sasa hivi bado hatujagusia kabisa kiini cha stori yetu, SANDUKU LA AGANO LA BWANA.

Pamoja na kwamba habari zili-break dunia nzima kuhusu kubomolewa kwa hekalu maarufu zaidi duniani, lakini habari mbaya sana kwa WAYAHUDI ilikuwa NI KUPOTEA KWA SANDUKU LA AGANO LA BWANA.

HIYO NDIYO HABARI MBAYA MNO MNO! HEKALU LINGEWEZA KUJENGWA TENA MBELENI, LAKINI ILIKUWA HAIWEZEKANI TENA KUPATA LILE SANDUKU LA AGANO, HASA VILE VITU VILIVYOKUWEMO MLE NDANI.

Habari hii yote ya uvamizi wa majeshi ya Nebukadreza na uharibifu wote wa jiji la Yerusalemu na kuchomwa kwa Hekalu, zimeandikwa katika vitabu vifuatavyo: 2Falme sura yote ya 25, ikarudiwa kwenye 2Nyakati 36:13-21, na kurudiwa tena na nabii Yeremia sura yote ya 39.

TUSISITIZE KABISA, SANDUKU LA AGANO LA BWANA LILIKUWA NDIO UWAKILISHO WA UWEPO WA MUNGU KATIKATI YA WAISRAELI.

Ngoja kwanza nikueleze kile ambacho pengine hujui kuhusiana na taifa la Israeli.

Ukienda pale Israeli siku ya tarehe 9 mwezi Av (Abu) yaani mwezi wa tano, ambapo kwa kalenda yetu huwa mojawapo ya siku za mwezi July au August, utakuta nchi nzima imenyamaza kimya. Hutasikia mziki ovyo ovyo mtaani.

Ni marufuku mtu kula au kunywa chochote siku hiyo.

Ni marufuku kufanya tendo la ndoa au vitendo vya kimapenzi.

Ni marufuku kusalimiana.

Ni marufuku kufanya starehe yoyote.

Ni marufuku kuvaa nguo nzuri.

Ni marufuku kukaa kwenye viti vya juu, ni kukaa chini kabisa au kwenye vigoda.

Kulikoni?

Kila siku ya tarehe hii ni maarufu kwa jina la TISHA B'AV.

Tisha B'Av ni siku kubwa sana katika Historia ya Israeli.

Wayahudi husafiri kutoka maeneo yote duniani kuja Israeli kukutana Wayahudi wenzao na hukutanika mbele ya ule ukuta maarufu uitwao Western Wall au kwa jina lingine Ukuta wa maombolezo (Wailing Wall). Wanapofika hapa hufanya ibada za maombolezo makali sana.

Kwa nini wanafanya hivi?

Kwa ufupi sana, HII TAREHE NI TAREHE AMBAYO HUWA INAKUJA NA MABALAA MAKUBWA SANA KWA TAIFA LA ISRAELI.

Mabalaa yote makubwa ambayo yamewahi kuwakumba Waisraeli, iwe ndani au nje ya Israeli kwa Wayahudi waishio nje, YAMETOKEA TAREHE YA TISHA B'AV!

Sasa, tukio tunaloeleza leo la uharibifu wa lile Hekalu la Yerusalemu lilitokea tarehe hii.

Hata lilipojengwa tena, lile la pili ambalo Yesu alipozaliwa duniani alilikuta, lilikuja kubomolewa tarehe hii hii ya Tisha B'Av mwaka 70AD, (miaka mia sita baada ya hili tukio la leo) kama Yesu alivyolitabiria kuwa halitasalia jiwe juu ya jiwe!

Sasa tuache yote hayo.

Kama tulivyosema, moja ya vitu ambavyo WAISRAELI WALIJUTIA MNO MNO, NI KUPOTEA KWA LILE SANDUKU LA AGANO LA BWANA.

KWA HUZUNI KUBWA, TISHA B'AV YA LEO NDIO ILIKUWA IMEKUJA KUCHUKUA SANDUKU LA AGANO LA BWANA, NA MILELE HALITAONEKANA TENA!

Hili sanduku ndilo hasa makala haya yamelenga kulizungumzia.

Sanduku la Agano la Bwana, LILIKUWA NDIO UWAKILISHO WA UWEPO WA MUNGU HASA HAPA DUNIANI, KATIKATI YA WANA WA ISRAELI.

Ni nini hasa kilitokea kwa Sanduku hili?

Lilienda wapi hadi leo dunia haijui lilikopotelea?

Fanya hivi:

Usiache kujipatia vitabu vyetu viwili ambavyo vimekusanya zile habari za kusisimua ambazo biblia haikupata fursa ya kuziandika, ingawa ni nzuri na zina mafunzo mema yasiyopingana na biblia. wote tunajua kwamba biblia isingeweza kuandika kila kitu hata kama ni kizuri.

Katika vitabu hivyo:

Utapata kuijua stori ya kweli ambayo wengi hawajawahi kukutana nayo ya Simoni, yule mchawi anayetajwa kwenye Biblia Matendo 8. Huyu twaweza kusema ndiye mchawi mtenda miujiza wa kutisha zaidi kuwahi kutokea na kuutikisa Ukristo kwa matendo yake!

Mtume Petro na Paulo walivyomshughulikia mbele ya umati wote wa jiji la Roma wakati akiwa anapaa, ni tukio tukufu la kupaswa kuhadithia vizazi vyetu, ingawa anguko lake lilisababisha visasi vibaya ikiwemo kuuawa kwa Mtume Petro na Paulo, na tumekueleza kwa kina jinsi walivyouawa na miujiza iliyotokea siku hiyo walipouawa.

Katika vitabu hivyo utapata pia zile nyaraka za mambo ya kale yaliyogundulika hivi karibuni nchini Uturuki, Israeli pamoja na Italia, kuhusiana na habari za Yesu zilizokuwa zimefichwa na wale waliomchukia. Moja ya nyaraka muhimu iliyopatikana ni pamoja na hii yenye mahojiano waliyowahi kufanyiwa enzi hizo Mariamu mama yake Yesu, Josefu baba yake, Martha na Maria dada zake Lazaro, na mtu aitwaye Masaliani.

Utamfahamu Yesu kiundani tangu utoto wake, maisha yake ya kawaida na tabia zake akiwa nyumbani, na alichokuwa akifanya nyumbani hasa kukitokea ugomvi. Pia utafahamu kuhusu tabia ya ajabu aliyokuwa nayo kwenye kula kwake na kuvaa kwake.

Utamwona Mariamu alivyokuwa akiudhika kwa vile Yesu alivyokuwa hahangaiki kutafuta utajiri, mke, umaarufu, wala kujijenga kisiasa, akiamini Yesu angekuwa mfalme wa siasa za kidunia.

Utamwona pia Martha dada yake Lazaro alivyokiri kutamani kuwa mke wa Yesu, lakini soma uone jinsi Yesu alivyokuwa akiishi dhidi ya wadada, hadi watoto wadogo wa kike.

Pia, utayajua maisha ya Yohana Mbatizaji ambayo Biblia haikuandika. Biblia imetuacha na maswali kadhaa kumhusu Yohana Mbatizaji: Mfano, Yohana aliweza vipi kuishi ndani ya jangwa lile hatari la Yudea, tena tangu akiwa mtoto mdogo? Alifikishwaje katikati ya milima hatari ya jangwa lile? Soma utapata majibu na pia utaona jinsi malaika walivyomlea Yohana tangu akiwa mtoto mdogo hadi alipokuwa mtu mzima na kuanza huduma rasmi.

Hatukuacha kukupa vile visa vya kusisimua vya jinsi Pontio Pilato pamoja na Kuhani Mkuu Kayafa walivyokuja kuupojea Ukristo baada ya kushiriki kumtoa Yesu asulibiwe.

Kama unasumbuliwa na yale mawazo kwamba una matatizo magumu sana kiasi kwamba Mungu hawezi kukutoa hapo, tafadhali hakikisha kwa nguvu zako zote unasoma ushuhuda wa maisha ya Bernard kwenye kitabu hiki. Mwone Bernard kutoka Ghana, mtoto wa kahaba aliyekulia majalalani, akaugua ya kufa, akamjua Mungu, hadi kualikwa White House na Rais wa Marekani, leo akiwa ni mtu aliyefanikiwa sana duniani.

Stori ya wale majitu wanefili waliotajwa kwenye Mwanzo sita hatukuiacha, utawajua kwa undani na visa vyao vya kutisha vilivyomfanya Mungu afute dunia kwa mafuriko ya enzi za Nuhu na kuanza upya uumbaji.

Mwisho, tumekupa hii stori yote kuhusu lile sanduku la Agano, tangu kutengenezwa kwake, miujiza yake, na mambo ya ajabu yaliyotokea siku ile lilipopotea hadi leo.

Kitabu kimoja kina kurasa 92, kingine kina kurasa 104.

Vyote vinapatikana kwa shilingi 20,000 pekee.

Kama unataka hard copy utafikishiwa ulipo. Kama unataka soft copy utazipata kupitia whatsapp.

Wasiliana nasi kwa namba 0762731869.

Hiyo ni namba ya whatsapp na kupiga pia.
 
Haha! ya kwamba ukatoka mkono mbinguni ukaja kuchukua funguo...🤣🤣
Hii yamoto sana!
Ni ngano kama ngano zingine mkuu-japo jamaa anazipa hoja za kusema uhakika.
 
Acha uongo
Biblia inasema tokea kuharibiwa kwa hekalu ambalo tokea siku hiyo sanduku la agano halikuonekana tena wakati wa mfalme sedekia wa Yuda mpaka Yesu anazaliwa ni miaka 1400 (ni miaka 1000 mpaka wakati wa malaki na malaki mpaka yesu ni miaka 400)
 
Haha! ya kwamba ukatoka mkono mbinguni ukaja kuchukua funguo...🤣🤣
Hii yamoto sana!
😆😅😀 Yani we mwamba unanifanya nicheke kabla sijasoma hata uzi wenyewe...!!
 
Sanduku alipewa menelik mtoto wa suleiman aliyezaa na malkia Sheba
 
Back
Top Bottom