Hii Hofu ya Historia ya TANU na Uhuru Inaletwa na Nini?

Hii Hofu ya Historia ya TANU na Uhuru Inaletwa na Nini?

Historia ya kupigania uhuru ilianza na Mwl Nyerere na ilimalizika na Mwl Nyerere.

Mikutano ya TANU ilifanyika katika michezo hasa Dar Young Africa na kumbi za starehe full stop.
 
Screenshot_20241019-195155.png
 
Historia ya vuguvugu la siasa lilianza mbali sana.

Ukipenda unaweza kuanza 1924 Dr. Kwegyir Aggrey kutoka Achimota College, Ghana alipomshauri Kleist Sykes kuunda African Association.

View: https://youtu.be/7xhv_ZEn51M?si=PgoVhCUbGsDGhTC8

Sikuhitaji hayo maelezo lakini kile kipengele Cha matamasha ya taarabu kutumika kama sehemu ya mikutano kama alivosema kijana wa baba wa taifa mbona wewe mwenyewe uliwahi kukiandika?
 
Sikuhitaji hayo maelezo lakini kile kipengele Cha matamasha ya taarabu kutumika kama sehemu ya mikutano kama alivosema kijana wa baba wa taifa mbona wewe mwenyewe uliwahi kukiandika?
Mpaji...
Hakuna mkutano wowote wa siri au wa dhahiri uliofanyika katika taarab ukitoa taarab moja tawi la TANU Mtaa wa Mvita.

Taarab hii iliitishwa makhsusi mwaka wa 1957 Nyerere alipozuiwa kuhutubia mikutano ya hadhara.

Si kuwa taarab ikipigwa ili kuwepo na mkutano.

Wala hapakuwa na mkutano wowote wa TANU Club ya Yanga Mtaa wa Mafia na Sukuma.

Hakuna kiongozi yeyote wa TANU aliyepata kuhudhuria mkutano hapo Mafia na Sukuma.

Viongozi wa yanga 1940s hadi uhuru unapatikana Mohamed "Mabosti" Sultan, Kondo Kipwata hadi Mangara Tabu hakuna hata mmoja aliyejishughulisha kwa ndani katika harakati na mipango ya kudai uhuru.

Wote hao walikuwa wanachama na wapenzi wa TANU wa kawaida.

Harakati zote za TANU na mikutano ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu na mikutano mingine nyumbani kwa Bi. Mwamtoro bint Chuma Mtaa wa New Street na Kariakoo.

Uliza uelezwe.
Ulikuwa hujui utajua.
 
Sikuhitaji hayo maelezo lakini kile kipengele Cha matamasha ya taarabu kutumika kama sehemu ya mikutano kama alivosema kijana wa baba wa taifa mbona wewe mwenyewe uliwahi kukiandika?
Hili hawezi kukujibu.
 
Back
Top Bottom