Hii ikoje kwa Premio (F) 1490?

MUBIKU

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2014
Posts
283
Reaction score
384
Wakuu ninatumia Premio f , cc ndogo 1490, kwa sifa nilizowahi kusikia kuhusu gari hii upande wa matumizi ya mafuta ni mdogo kama vile ist, ila kinachonishangaza nimeweke lita 10 ( mafuta ya elf 30,000) ile Taa nyekundu kwenye Dash board inawaka muda wote, mpaka gari ikanizimikia na nimetumia mafuta hayo kwa kutembea takriban KM 20 Tu.

Shida nini hapo haswa mbona sion ile sifa ya kuwa na low fuel consuption. Nawasilisha naiman ya kupata majibu mazuri kwenu.
 
Na nyie wa premio mnalalamika mafuta tena?
 

Kama gari ni Nzima umeibiwa!
Umewekewa mafuta ya shs 3,000 badala ya mafuta ya 30,000
Kwa hiyo gari yako, huo umbali ni mafuta ya shs 3000 tena kama injini iko vizuri haingekausha

Tafuta tena shs 30,000 nenda kituo cha mafuta, na angalia pale kabla ya kuweka ionekane 00.00 na aweke mafuta hadi iandika 30,000 utuletee mrejesho
 
Umepigwa hukohuko sheli
 
Napinga mkuu,

Ila unaweza kujaribu kuwa unazima gari kabla ya kuweka mafuta
 
Muwe makini mnapoenda kujaza mafuta kwenye kituo chochote. Tatizo wengine mkishatoa maelekezo ndio mnatoa smart phone zenu nakuwa busy na "nini kinaendelea huku mitandaoni". Mjanja kwanini asikupige hapo kama hufuatilii?
 
Muwe makini mnapoenda kujaza mafuta kwenye kituo chochote. Tatizo wengine mkishatoa maelekezo ndio mnatoa smart phone zenu nakuwa busy na "nini kinaendelea huku mitandaoni". Mjanja kwanini asikupige hapo kama hufuatilii?

Nawapenda wa Bajaji wanashuka kabisa kuangalia

Wenye magari wanapandisha vioo wasipaliwe na harufu ya Diesel na petrol
 
Hii ishawahi kunikuta , umakini inahitajika kweli
Hata mimi ilishanitokea, now nikienda kituo cha kujaza mafuta macho yangu yote kwenye kusoma amount bar na kiasi cha mafuta kilichoingia kwenye tank. Pia ilishwahi kutokea tena hivi karibuni tu, nimemwambia "Elfu saba" ye akaweka 17k, nampa elf 10 ananiambia ongeza hela kaka. Nikamwambia nimekwambia weka ya elf 7 kama unaweza yatoe hayo yaliozidi mimi sina hela ya ziada, tena hiyo chenji ni yakula. Dereva wa gari ya nyuma akawa anasumbua kwakupiga honi ili nimpishe, mi nikaamua kuondoka bila chenji na sijampelekea hiyo hela mpaka leo
 
Umepigwa jombaa. Siku ingine kuwa makini na wadada wa sheli😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…