KERO Hii ikufikie Rais Samia, kama ulipanga kutoa zawadi basi toa ila hili la Muleba unadhalikika

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
221
Reaction score
542
Kuna haja gani ya kuchangisha watumishi pesa ili mitungi ya gesi inunuliwe kwa pesa za watumishi kwa lengo la kutengeneza taswira kuwa mama katoa zawadi ya mitungi ya gesi kwa wananchi.

Kama mpango wa mwaka huu katika siku ya wanawake ilikuwa ni kutoa mitungi ya gesi kwanini hiyo budget isiandaliwe chini ya budget ya Ikulu ili lengo litimie?

Muda wa ku fake maisha umeisha, kama ni kweli siyo wewe Rais ulowatuma hawa viongozi wa Muleba kunyanyasa watumishi kwajili ya wewe kutimiza lengo lako, please toa tamko kabla ya tarehe 8 kuhusu jambo Ili, tuma TAKUKURU wachunguze jambo Ili isijekuta kuna baadhi ya watu wanataka kupiga pesa kwa kigezo cha maagizo ya Rais kuchangiwa mitungi Ili aje kufanya show off kwenye siku ya wanawake duniani.

 
MMECHEMKA MAMA HADHALKILIKI KWA UONGO KAMA HUO HAKUNA KITU KAMA HICHO HEBU UKILAZIMISHWA KATAA WATU WANATAKA KUPIGA HELA KWAKUTUMIA JINA LA MAMA MSIKUBALI
 
Yaani mtu unamkataza kutumia Kuni (which is free)...

Unatumia Kodi zake ili gharama ya Mitungi iwe ndogo.., Unampa mtungi ambao kujaza ni gharama kuliko mbadala (UMEME) ambao upo na unatoka nchini...

Unatumia hizo fedha kuagiza Gesi kutoka nje ya nchi (WAKATI NDANI UNA MBADALA) na wakati wote huu unafanya kampeni kutumia pesa zake (KODI / RUZUKU) ili kufanyia kampeni biashara za watu binafsi (GESI)...



 
.
WEKENI na mawasiliano ya huyo MKUU wa WILAYA IKIWEZEKANA na picha yake tumtambulishe kwa UMMA kuwa
 
Nachukia sana zile vitenge vya ccm, kofia na skafu....na sasa Gesi.

Watanzania wenzangu njaa zetu ndizo zinazofanya tuweke nchi rehani...
 
Iiih, mama wanamzuguka !
 
Kwanza gesi yenyewe bado ipo juu
Mitungi inatakiwa kwa watani at least elfu 5 na kujaza gesi shillingi elfu 5 at least kwa gharama iyo kila mtanzania atakimbilia gesi bila hata kuhamasishwa. Customers always look for cheaper options.
 
Asante.
Unafikiri Mazezeta yatakuelewa?....
Chawa watakuja mbio kukuvamia....kama mazombi...
Huu ni msumali wa moto kwa vilaza
 
Mitungi inatakiwa kwa watani at least elfu 5 na kujaza gesi shillingi elfu 5 at least kwa gharama iyo kila mtanzania atakimbilia gesi bila hata kuhamasishwa. Customers always look for cheaper options.
Unajua hio mpaka wewe ununue elfu tano sio kwamba muuzaji au kule nje tunapoagiza wanachukua elfu tano..., Ni kwamba pesa yako unayokatwa kwenye TOZO badala ya kufanya maendeleo mengine ndio inawalipa hawa wenye biashara zao (Hence ni kwamba umenunua kwa njia nyingine, Kodi na Direct)

Sasa kwanini tufanye hivyo wakati kuna mbadala kwa huyo mwanakijiji ambao ni wa gharama nafuu na tunazalisha nchini ?

 
πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ”¨
 
Hayo mavyuma yanasambazwa kweli.
Binafsi ninayo ya kg 15 sijui ni mwaka wa ngapi familia yangu haijayatumia baada ya gas kupanda bei.
Gawa gas watu waghalimie mitungi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…