tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Hii ilikuwa ni 30.09.2020 Tundu A.M Lissu akiwa mgombea Urais wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa 2020 akiingia Moshi Mjini. Watu walimsubiri uwanjani hadi usiku wa saa mbili kasoro hivi.
Hawakutaka kuondoka, wakaamua kuruka majoka uwanjani wakimsubiri kumpokea Tundu A.M Lissu. Kumbuka, hapa mgombea wa CCM alikuwa John Pombe Magufuli, akiwa Rais.
Kuchelewa kwake kulitokana na wananchi wengi kumsonga na kuziba njia asipite bila kuwasalimia. TAL alisimamishwa Marangu, Jimbo la Vunjo na nyomi kubwa haijawahi tokea Marangu
Baadae msafara wa Tundu A.M Lissu ulifanikiwa kufika Moshi Mjini usiku. TAL alikuta maelfu ya watu waliokuwa wakimsubiri bila kukata tamaa na walionesha kuwa na hamu nae kubwa
Tundu A.M Lissu alishindwa kuzungumza kwa jinsi wananchi walivyokuwa wakiimba na kupiga kelele za kuonesha mahaba mazito kwake wakisema “RAIS! RAIS! LISSU! LISSU!’
Kuwatuliza ikashindikana. Mwisho ikabidi, awatangazie wananchi atarejea tena kufanya mkutano, alishangiliwa na vifijo vya faraja kuu. Akaondoka na akarejea Moshi Mjini 19.10.2020
Nimeona picha za mbogamboga jana wakiwa katika viwanja vya uchochoroni wanasema wa wamevunja rekodi – ukitazama uwanja ule wamejazwa watoto wadogo wa shule hadi noma..
Shule zimepewa maelekezo kuwataka wanafunzi na walimu kuruhusiwa kuhudhuria shughuli hiyo ya mkutano wa hadhara. Halafu wanasema wamevunja rekodi zote. Rekodi?
Mkutano wa Tundu A.M Lissu ni ‘organic crowd’. Mikutano ya hadhara ya mbogamboga ni ‘rent-a-crowd’. Ndiyo maana unaona waliohudhuria wote wamevalishwa sare za mbogamboga
Kwa kugundua hilo, mbogamboga sasa wametengeneza upinzani wa kughushi. Wamechonga vikaragosi vyao wenyewe na wanashindana navyo. Hawawezi kushindana na CHADEMA
Mbogamboga wanaelewa, upinzani pekee ambao ungeweza kuwapelekea pumzi ya moto ni CHADEMA pekee tu. Hivyo, wamewazuia kufanya shughuli za kisiasa, hata vikao tu
Mbogamboga, mnasema mmevunja rekodi. Dhidi ya nani ambaye mnashindana naye? Mpango wenu wa kando, CHAUMMA? Kazi yenu maalum, ACT? Au vyama vya mfukoni kama AAFP?
Kila nikiwasikia wakirudia maneno ya “tupige kura tuwazibe midomo” nacheka sana. Huwezi kuwaziba mdomo watu hawa ambao wanaelewa nini msingi wa #NoReformsNoElection