Hii iliniuma sana; Minaki High School(2009)

Joined
Apr 7, 2012
Posts
21
Reaction score
4
Wanajf; Sitaki kuamini kama hii system ya kuweka wanafunzi barabarani ili msafara wa kiongozi flan apite.
Nakumbuka 2009,sikumbuki tarehe,nlikua form 6 pale Minaki chini ya Head master JJ Kaaya,tulitangaziwa sku moja kabla,kwamba kesho yake patakua na msafara wa makamu wa rais,Dkt Shein akielekea kisarawe,kwahiyo kuanzia saa moja asubuhi,kila mwanafunzi awepo barabarani na tawi lolote.
Sku ilipotimia watu tukaenda,tukaanza kuimbishwa nyimbo za CCM namba wani;time ilienda mpaka saa saba mchana,wachache wetu tukaamua kuondoka maeneo yale ya barabara.
Tarifa nlizo zipata ni kwamba mheshimiwa alipita saa tisa na nusu alasiri,baada ya hapo rollcall ikapita.
Kesho yake kwa wale ambao tuliondoka,tulipigwa adhabu kali,we spent almost two weeks tukiitumia. Kila nikikumbuka,nafadhaika sana;sjui kama hii sytem bdo ipo.
 
Hongera sana na uwashukuru waliokufanyia kitendo hiko kwani leo wamekupa ujasiri wa Kuichukia CCM na kama sio hilo tukio saa hizi ungekuwa mwana CCM.
 
Nashukuru mungu sijawahi kufanya upuuzi huo. Nilijitambua mapema na hakuna mwalimu aliweza kunipelekesha kihivyo. Offcourse nilichimba visiki na kuvhezea suspension kadhaa lakini mwisho wa siku walimu walinikubali kwa msimamo wangu. Thanks God
 
Kijana mimi 1992 baada ya magauzi kuanza nilikuwa sifanyi vitu kama hivyo hata aje nani. Nakumbuka nikiwa form 4 wakati huo nilikuwa nasumbuana sana na maticha kwenye kuchangia mafuta ya mwenge, mi nilkuwa sitoi. Maticha wanalazimisha tutoe. Tunapelekeshana hivyo hivyo.

Sasa wewe form 6 tena 2009 unakubali kukaa juani na matawi kumpungia mtu ambaye anapita kwenye gari full tinted kwa spidi ya 160, tena hata gari alilopanda hulijui!
 
minaki enzi za marehemu mjale (mwl.mkuu minaki) siku hiyo mngekula nyali na kesho yake uji mpaka wa paper two.
 
Acha ujinga bro, huu si muda wa porojo bali tunatakiwa tujadili kuhusu anguko la elimu. Ebooo
 
Nami nilishakaa pale barabarani chini ya kaaya. Kikwete alikuwa anapita anaelekea kisarawe. Vipindi vilivunjwa aiseee. Ilikuwa kati ya 2006 na 2008... Alikuja kupita kama masaa 6 baadae. Wakati tulikaa toka asu
 
hiyo system bado ipo... Na inakera kumtoa mwanafunzi darasani akaandame kisa sikukuu au shughuli za kiserikali au kichama... Hapa singida 2011 sikukuu ya wakulima ilidondokea weekday madogo walitembezwa umbali mrefu kwenda viwanja vya maonesho kimkoa...ILINITIA KICHEFUCHEFU SANA..watoto wanatembea kwa miguu,wengine viatu mkononi, hawana hela ya maji/nauli.. VERY DISGUSTING
 
Mimi nilisoma enzi za Mwalimu lakini hata hivyo marehemu baba yangu alinikataza kuuangalia MWENGE na mpaka hivi leo sijautia mwenge machoni mwangu!!
 
KIONGOZI INNO UPO? Aisee J J Kaaya alikuwa mtumwa sana kwa Serikali ya CCM! Hapakuwa na haja ya kukaa barabarani siku iyo coz hapakuwa na ratiba ya msafara kuzungumza na wanaminaki! Mbaya zaidi tulipoteza vipindi na msafara wao hukusima!
 
Tulipangwa na Teacher Papa Mukulu mwenyewe lakin msafara ulipita shwa! Kama hawatujui vile. I was form v at that time nilikuwa mtiifu.
 
Mkuu mwaka 2008 mwishoni kama sijakosea tulipangwa barabarani kisa JK alikua anamsafara kuelekea Kisarawe cha kushangaza J J kaaya nae hakujua ratiba ya rais kwani alikujakupita mida ya saa saba.

Kuna mwanafunzi wa f.six EGM alikuja kufukuzwa kwa mizengwe ya kuvaa suali ya jinsi wakati wa msafara wa rais, lakini hili lilitokea baada ya kumfikisha J J kaaya polisi kwa kumpiga bila kosa.
 

Huyu kaaya c ndo alikua tambaza? Dah alikua anapiga bakora sana, kuna siku alinionea sana, tulikua tunapanga viti kwa ajili ya necta sasa kuna kiti kilibaki nje jamaa kwa sababu nlikua karibu yake alinitandika bakora mbili mbele ya wanafunzi wote wa kidato cha sita, dah na kesho yake asubuh nlikua naanza pepa, alinichangaya sana, mpaka akasababisha nipate dv 2

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Habari hyo imenipa kichefuchefu,kama walimu wa minaki wanaendelea na hbr hzo nawaomba waache mara moja,hbr za kutafuta vipesa pesa vya msaada haiwasaidii coz wanahaibisha taalamu zao ,na wanaonesha kuwa na ufinyu wa demokrasia. Mimi nilitofautina na walimu kila siku kuhusu hbr hizo,nakumbuka kuna siku jamaa wa ccm ( makamba,msekwa,gachuma,lameck airo na zakaria) walileta mchele,ng'ombe na soda shuleni kwetu kwa makubaliano ya kuwapigia kura ccm. Mwl mkuu George opiyo akauliza wangapi hawatakula, tukanyoosha mikono! Akatuagiza tutoke mbele,tukafanya hvyo kama watu 15. Nakumbuka siku hiyo kulikuwa na mkutano wa cdm ulokuwa unaongozwa J.Mnyika,2kaenda pale kwa kuwa ilikuwa karibu na maeneo ya shule wanafunz wengi walijitokeza naomba kumunukuu JJ" mabadiliko yoyote,taifa lolote uletwa na kundi la wasomi,lakini wasomi wetu ndo hawa vijana wanaouza nchi na finyango ya nyama,sahani ya wali na soda. Yaani vijana wasomi wameamua kuuza haki ya baba,mama,shangazi,mjomba na watanzania wote kwa almost sh 2500!" kauli hiyo iliwabadili wengi kurudi chuo tukapata wafuasi wengi na mwisho wa siku headmaster alinitishia kunifukuza shule. Ajabu zaid cdm ilibadili upepo pale shule na kuzoa kura asilimia 98% ,so mambo ya Minaki yapo kila sehemu lkn niwajibu wa wale wenye uelewa kupinga ujima huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…