Hii imekaaje kudharau watumiaji wa simu za Tecno na Itel ilihali wote mnakuwa na access ya vitu vinavyofanana

Hii imekaaje kudharau watumiaji wa simu za Tecno na Itel ilihali wote mnakuwa na access ya vitu vinavyofanana

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Unakuna pale unapoweza.

Kumekuwapo na imani kuwa watumiaji wa simu wa makampuni ya Tecno na Itel ni watu washamba na wasio na uwezo kifedha. Kiukweli katika mtizamo wa kutokuwa na uwezo kifedha naweza kuunga mkono lakini katika kuwa washamba ni jambo lisilo na ukweli.

Hivi inakuwaje mtu una akili zako timamu kabisa unaanza kumdiss mtu anayetumia Tecno au Itel wakati wote.

1. Mna access ya internet
2. Mnaweza pata kile mtakacho kama apps, muziki, videos na movies
3. Mna Ram na storage zinazofanana.
4. Camera yenye quality
5. Tunapost, tunacomment, tunashare na kulike.

Yawezekana utofauti upo kati ya makampuni aya na mengine lakini sio utofauti ule wa kuanza kukejeli na kudharau hizi simu.

Na kama ushamba ni yule anayemiliki simu ya gharama kubwa wakati angeweza kuwa na simu ya gharama nafuu lakini yenye performance kubwa.

Je simu ya gharama kubwa inayotumika kusikiliza muziki na kufuatilia maisha ya wasanii inaweza kulingana na simu ya gharama ndogo inayotumika kujisomea na kwenye biashara?

From northern part of Tanzania.
 
Unauliza maswali ya kijinga.

Utofauti ni class/hadhi na ubora.

Ndio maana kuna basi la Shabiby na La Al hushum, yote yanafika Dar ila hadhi na ubora yanatofautiana.
Kivipi unafananisha basi na simu? Na kama class ndo inakufanya utumie simu fulani bila kuangalia specifications ni wazi unahitaji ukombozi wa kifikra.
 
Mkuu jifunze kwa wazungu..
Wale jamaa awapendi vitu under quality
Simu tajwa hapo juu zina vingi vya kujifunza kutoka kwa Simu za mzungu..
Na kwa kuanzia tu hizo simu tajwa hazitumiki huko zinakotengezwa.

Just imagine mtu anapika vitumbua af yeye mwenyew hatak watoto wake wale ila anawauzia wengine..
 
Acha kukariri mkuu, kaangalie top ten ya smartphone hizo za mzungu zipo ngapi
 
Mkuu jifunze kwa wazungu..
Wale jamaa awapendi vitu under quality
Simu tajwa hapo juu zina vingi vya kujifunza kutoka kwa Simu za mzungu..
Na kwa kuanzia tu hizo simu tajwa hazitumiki huko zinakotengezwa.

Just imagine mtu anapika vitumbua af yeye mwenyew hatak watoto wake wale ila anawauzia wengine..
Hizi simu ni under quality kwa tafiti za nani? Na nani alikwambia hazitumiki zinapotoka? Narudia tena mnao diss hizi simu hamna hoja za msingi zaidi ya kashfa na dharau.
 
Unakuna pale unapoweza.

Kumekuwapo na imani kuwa watumiaji wa simu wa makampuni ya Tecno na Itel ni watu washamba na wasio na uwezo kifedha. Kiukweli katika mtizamo wa kutokuwa na uwezo kifedha naweza kuunga mkono lakini katika kuwa washamba ni jambo lisilo na ukweli.

Hivi inakuwaje mtu una akili zako timamu kabisa unaanza kumdiss mtu anayetumia Tecno au Itel wakati wote.

Passo vs bmw utakuwa umeshaelewa maana ya matumizi
 
Back
Top Bottom