Hii imekaaje, lugha ya Kiswahili kutambulika kama lugha ya Kenya katika apps?

Hii imekaaje, lugha ya Kiswahili kutambulika kama lugha ya Kenya katika apps?

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Moja kwa moja..

Leo katika kuperuzi katika nikakuta adds ya app ya kujifunza kuongea kimalkia nikaamua kuipakua .

Nimestaajabu kikivyokuja kipengele cha kuchagua lugha yako unayoitumia Kiswahili kukuta imewekewa bendera ya Kenya wakati Tanzania ndiyo wazungumzaji wa Kiswahili kwa asilimia kubwa.

Hiyo siyo mara kwanza kuna sehemu nyingine niliwahi kukuta Kiswahili imewekewa bendera ya Kenya .

Hii kitaalamu imekaaje kwa nini Tanzania isitambulike?

Kapicha cha kusindikizia uzi hako

IMG_20220314_150751.jpg
 
^Watanzania wanapaswa kufanya mabadiliko muhimu & ya lazima; vinginevyo, kila kitu wao watakuwa wakishangaa na kusema, Ala! Wachina hawa!^ ~ JKN
 
Moja kwa moja..

Leo katika kuperuzi katika nikakuta adds ya app ya kujifunza kuongea kimalkia nikaamua kuipakua .Nimestaajabu kikivyokuja kipengele cha kuchagua lugha yako unayoitumia Kiswahili kukuta imewekewa bendera ya Kenya wakati Tanzania ndiyo wazungumzaji wa Kiswahili kwa asilimia kubwa

Hiyo siyo mara kwanza kuna sehemu nyingine niliwahi kukuta Kiswahili imewekewa bendera ya Kenya .Hii kitaalamu imekaaje kwa nini Tanzania isitambulike ?

Kapicha cha kusindikizia uzi hakoView attachment 2150133
Kenya ndio inatambulika kwa kiswahili. Hata inapotokea ukapata kazi ya localization ambapo hawajaspecify kisw cha nchi gani wana expect localization itatumia kisw cha kenya.

Google wana localize content zao via welocalize ambao wanashirikiana na DDD ambayo ni kampuni ya kenya, ila Google kwenye localization wanalocalize content kwa kisw cha kenya na tz, kwa tz DDD wamefungua ofs wakaajiri watz, ila bado ambaye anafanya final review ni mkenya kabla ya kutuma hizo content kwa Google.

Honor Os, whatsapp pia waliotengeneza gloassary ya key words kwaajili ya localization ni wakenya.
Sisi tumebaki tu na masifa tunajua kisw tunajua kisw
 
Kwani hujui hata mlima kilimanjaro upo kenya?
Inasikitisha sana kuna mpk muvi ya kizungu ya kilimanjaro niliiona nayo imeigiziwa Kenya humo kuna Wamasai mpk Kiswahili wanazungumza ila Tz hatujapaishwa wkt kilamanjaro ni yetu
In-the-Shadow-of-Kilimanjaro-large.jpg
 
Waache upuuzi tutawasukumia nondo marindani, wameanzaje kupora lugha za watu na kusema zao?
 
Waache upuuzi tutawasukumia nondo marindani, wameanzaje kupora lugha za watu na kusema zao?
Badala ya kukasirika na kulalamika tujiulize tumefail wapi? Kenya ni kati ya nchi 5 maarufu zaidi Afrika
 
Moja kwa moja..

Leo katika kuperuzi katika nikakuta adds ya app ya kujifunza kuongea kimalkia nikaamua kuipakua .

Nimestaajabu kikivyokuja kipengele cha kuchagua lugha yako unayoitumia Kiswahili kukuta imewekewa bendera ya Kenya wakati Tanzania ndiyo wazungumzaji wa Kiswahili kwa asilimia kubwa.

Hiyo siyo mara kwanza kuna sehemu nyingine niliwahi kukuta Kiswahili imewekewa bendera ya Kenya .

Hii kitaalamu imekaaje kwa nini Tanzania isitambulike?

Kapicha cha kusindikizia uzi hako

View attachment 2150133
Hapo hajamaanisha kwamba Lugha ya Kiswahili inatoka Kenya, amemaanisha App hiyo imeunganishwa na Kiswahili chenye ladha ya Kenya,

Kama vile ukiwa unachagua Lugha ya Kiingereza, Japo inafahamika Uingereza ndio muasisi wa Lugha hii lakini Kuna Kiingereza cha Marekani, Canada au Astralia na App nyingine zinakupa Option ya kuchagua unapendelea Kiingereza cha nchi Gani
 
Moja kwa moja..

Leo katika kuperuzi katika nikakuta adds ya app ya kujifunza kuongea kimalkia nikaamua kuipakua .

Nimestaajabu kikivyokuja kipengele cha kuchagua lugha yako unayoitumia Kiswahili kukuta imewekewa bendera ya Kenya wakati Tanzania ndiyo wazungumzaji wa Kiswahili kwa asilimia kubwa.

Hiyo siyo mara kwanza kuna sehemu nyingine niliwahi kukuta Kiswahili imewekewa bendera ya Kenya .

Hii kitaalamu imekaaje kwa nini Tanzania isitambulike?

Kapicha cha kusindikizia uzi hako

View attachment 2150133
Ni sawa tu, baadhi ya Apps Zina English American pekee, au English British pekee hata kiswahili Kuna Kenyan, Kiswahili Tanzania, Kiswahili Congo nk.

Nadhani wanakosea tu walipaswa kuweka jargons zote ili inulikane unataka kiswahili Cha wapi? Wenzetu wamezoea kuja hapa wakati mTZ atasema naomba uje.
 
Back
Top Bottom