Hii imekaaje mwanaume kunywa uji

Hii imekaaje mwanaume kunywa uji

We itakuwa umepitia yale malezi ya kikekike. Uji unanyweka sana na watu wanaofanya shughuli kama vile kilimo, ubebaji mizigo n.k
 
Tunatofautiana sana toka niko mdogo sana sipendi uji ila mpaka now huniambii kitu kwenye maziwa naweza kunywa hata dumu zima la 20ltr
Hadi mama hunitania kuniita kandamaa
 
Ila mimi mwanamke mwenyewe uji kunywa naona jau, [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] labda unibambe leba hivi hivi tu shenzi zake sinywi
 
Naupiga vibaya mno, Labda mngesema inakaaje mwanaume kula chips kaini ambazo hazijakauka ukisimamisha inainama na huwa na mafuta sana, huyu ni wakuhoji😄
 
Katika jitihada la kumiliki jina la uanaume , wanaume wengi tunakwenda kaburini mapema .

Ukiwa mwanaume unatakiwa usile sana , usilie , ujikaze hata kama unaumia ,ufanye kazi ngumu ngumu ect ,

Hii attitude ya kukumbatia uanaume ndo njia sahihi kabisa inayotupeleka kaburini mapema.
😇
 
Nimeenda kumtembelea lafiki yangu nimekuta ana kunywa uji hii imenishangaza sana najua uji ni kwa ajili ya wanawake na watoto wanaume ni chai na kahawa hii dunia ina enda kasi sana.

mimi mwenyewe hata leo hii nimekunywa uji. siku zile ambazo nimepiga sana kazi sijapata nafasi kula chakula mchana, nikirudi home lazima nianze na uji ndio vije vyakula vingine. pia, kuna mwaka nilikuwa ndio najenga nyumba yangu ya kwanza, nilijinyima sana kusevu pesa, na mkoa huo sikuhama na familia, nikawa kama bachela. basi, ikifika jioni naenda natwanga kikombe kikubwa cha uji sehemu moja mama ntilie alikuwa na machupa yake anauza everyday kuanzia saa moja, uji safi wa ulezi kachanganya na maziwa, karanga n.k, nikipiga uji siku hiyo naenda moja kwa moja kulala, ndo nikasevu pesa hadi kumaliza nyumba.
 
Katika jitihada la kumiliki jina la uanaume , wanaume wengi tunakwenda kaburini mapema .

Ukiwa mwanaume unatakiwa usile sana , usilie , ujikaze hata kama unaumia ,ufanye kazi ngumu ngumu ect ,

Hii attitude ya kukumbatia uanaume ndo njia sahihi kabisa inayotupeleka kaburini mapema.
uko sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom