Yaani hiyo ni mfano mbaya kwa jamii, maza house alipaswa kutoa onyo kali ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo na hao wahusika ili wasirudie tena huo ufenenge wao. Ucheka na nyani utavuna mabua. NDOA NA IHESHIMIWE
Hahahaaa imekaa vyema susy ukimkuta mwenye mali mwenye hasira anaondoka na sikio lako moja. Ni mchezo hatari sana huu
nilikuwa naziona sana pale mabibo hostel......!
jamaa anakaa na mwanamke semester moja,semester inayofuata the same woman anakuwa na rafiki wa jamaa....
halafu THEY LIVE HAPPILY THREE OF THEM!....
hasa hasa wale jamaa wa MUHIMBILI WALE.....
Hiyo red nimekusoma na ni ukweli kabisa eti wengine husema kwani tuliachana kwa ugomvi mara visingizio kibao ila lakini tukikutana kusalimiana ruksa eti DC au nayo noma??
Babu DC shikamoo nimekumiss sana babu yangu pamoja na busara zako. Naona leo umekua mkali sana kuhusu hili suala lakini ikumbukwe wanaume ndio mara nyingi hata kama mmeachana atakufuata fuata mpaka basi na sio mmoja yaani wengi wao sasa sijui unatusaidiaje sisi wajukuu zako kuhusu hii mitego ya wanaume tulioachana nao.
True, awe makini. Baba alimuagaje mama?????Duh, hii kali.. lakini imeonyesha uungwana kwa watu walioachana kistaarabu bila kutupiana mayai mabovu.. changamoto ni kwa huyo mke wake, awe serious ataibiwa!
huyo ni mwizi wa mapenzi kama wezi wengine tuliowazoea hakua la zaidi hapo anajipanga kufisadi ndoa ya mtu
Pia tukumbuke pamoja na kugombana kama wapenzi maisha bado yanaendelea, ipo siku mtakutana. Hakuna haja ya kuwekeana visasi mpaka mnavuana na c***i mlizopeana zawadi wakati mkiwa kwenye good terms
Kukuna ni jambo jingine kwani hiyo ni chance event (kama hakuna mawasiliano ya awali). Yaani ni probability kwamba mnaweza kukutana au la ambayo si kubwa sana. Ila kama mnakaa mnapanga kukutana na kufanyiana parties hayo ndiyo yanaleta mashaka.
Kusalimiana ni uungwana na hakuna dhambi hapo. Ila mkianza kutekenyana kwenye viganja ndipo tunawatilia mashaka kwama mnajizuga na kujidanganywa badala ya kuwadanya wenzi wenu na umma wote![/QUOTE]
Nimekusoma DC hiyo red umenichekesha kweli wewe
Maty wangu,
Upo wewe? Mwenzio nimelisusa hilo jina la babu...Sitaki mimi, nisijekuonekana na mimi ni mlozi kama huyo babu wa Loliondo.
:focus:
Maty, Maty.....Unataka niamini kwamba wanawake hawajui maana ya kuachana?
babu bora umetambua kwamba babu wa loliondo ni mlozi asee wewe unastahili sana, wanawake tunajua maana ya kuachana ila wababa wasumbufu sana tena sana unakuta hata alikuacha mwenyewe lakini baada ya muda eti................ ee mwenyezi mungu tujalie neema
Maty...Maty...Hebu basi acha kuniongezea huzuni mwenzio!
Kwa hiyo wakisumbua sana mnawakubali waendelee kuwachakachua? Hivi kwani hamjui kuwa wanaume wanapenda kuonja onja? Hamkuelezwa hivyo na bibi zenu?
Mwanamume wa kweli angefurahi kuwa na wake kama 5 hivi.. Mmoja anaishi kwenye wallet, mwingine anakwenda kumwona siku hiyo (date) na watatu wanakuwa kwenyereserve list huko home. Aki-miss date anaanza na yule wa kwenye wallet...Ikishindikana anaangalia reserve list.
Ningewambia shauri yenu..ila nawaonea huruma. Wengine ni wadogo zangu, wajukuu, shemeji, wanangu, mama ana shangazi zangu!