Hii Imepitiliza

Anfaal

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Posts
1,154
Reaction score
116
Picha hizi zinaonyesha ni kwa namna gani udhalilishaji ulivyokithiri. Huyu mama ni mama wa watu huko nyumbani na pia ni miongoni mwa raia ambaye anaamini kabisa haki zake zinapaswa kuheshimiwa. Lakini hili walilofanya mgambo kwa kuwa tu naibu waziri Nyalandu anakwenda kutembelea soko ni la kukemewa kwa nguvu. Kuna haja ya kuongeza sauti zetu, tupaze zaidi, tupinge hatua unyanyasi huu na ule unaoweza kuleta mauaji. Ni wakati sasa wa kusema hapana. Hawa watu wanaomfanyia hili huyu mama hawana moral authority wa kuendelea na kazi yao.
Picha hizo nimezitungua blog ya jiachie zikionyesha mgambo wakisafisha wamachinga kabla ya ziara ya naibu waziri.
 

Attachments

  • 163852_1759806724101_1507034707_31795657_3831575_n.jpg
    48 KB · Views: 453
  • 164851_1759807564122_1507034707_31795659_7604855_n.jpg
    45.3 KB · Views: 335
  • 162626_1759809324166_1507034707_31795661_2372790_n.jpg
    47.2 KB · Views: 841
Hadi mgambo siku hizi wana ruhusiwa kukamata raia?? sijui TZ inaeleke wapi. Soon kitanuka tu.
 
Naibu waziri, "mungu." Tanzania bwana!!
 
Yaani hii mambo bana, huku Lindi wazungu sometimes wanatuona sisi (Waafrika) uncivilized kwa namna tunavyofanyiana. Aibu aibu times 10 to the power of 10.
 



Mimi siwesi kucomment unless nijue tatizo lilikuwa nini!
 



Mimi siwesi kucomment unless nijue tatizo lilikuwa nini!
Well hao ni wale wanaoitwa wamachinga wanaofanya biashara katika maeneo yasiyotakiwa. Nami pia nimejaribu kufuatilia, inasemekana huyo mama walimwambia watamkamata na yeye akawatishia kuvua nguo zote.
 
Nimeumwa siku nzima kwa kweli nikajuta kwa nini niliiangalia,ukute ana watoto huyo na malengo yake ni wanae wasiwe kama yeye,jamaniii!!!
 
Huu ndo ujinga tunaofanyiwa na sisi tunashangilia. Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kumpiga mtu yeyote awe askari au nani. Lakini ni nini tunafanya kuonyesha kuwa hii siyo haki? Tunaandika tu na kuishia hapo. If we dont do something askari wateendelea kutunyanyasa na kutufanya punching bags.

If you keep doing what you always do, you will always be what you are. Period
 

Ukifungua mdomo wanakushoot, umesahau ya Arusha juzi? TZ sasa imekuwa kama German wakati wa Hitler,no democracy, bado kambi za mateso pengine nazo ziko mbioni kujengwa.
 
Mipango mibaya ya watawala ambao wapo bize kuuza nchi badala ya kuwasaidia the common wananchiz kama hawa ambao wanajitafutia rizki zao kwa njia halali. Huu ni ushenzi wa hali ya juu.
 
:A S-confused1: hawa mgambo nimesha wa mark sura zao, nitawafuatilia pale halmashauri, siwezi vumilia wakati uwezo ninao
 
:a s-confused1: Hawa mgambo nimesha wa mark sura zao, nitawafuatilia pale halmashauri, siwezi vumilia wakati uwezo ninao

wireless,utakuwa umesaidia sanaaaa,maana huwezi jua wamewanyia hivi wangapi au watawafanyia hivi wangapi. Mungu akuongoze ili tupunguze huu ukatili na uonevu.
 

kwa kweli inasikitisha sana, ila watz tujitahidi kufuata sheria, tusilete visingizio vya kutafuta riziki na kusomesha watoto kuhararisha kuvunja sheria. Huyo mama ni mama ntilie alikuwa anauza chakula mitaa ya kariakoo sokoni,
 
Jameni hii ni sirikali ya ccm kila mtu ana madaraka ni msemaji mtendaji. huu ndio shibe ya madaraka utawala usio na sheria
 
Sifa za kujiunga na jeshi letu ni nguvu nyingi akili kidogo
 
Mipango mibaya ya watawala ambao wapo bize kuuza nchi badala ya kuwasaidia the common wananchiz kama hawa ambao wanajitafutia rizki zao kwa njia halali. Huu ni ushenzi wa hali ya juu.

nakuunga mkono kuwa watawala wetu wa sasa wako bize kuuza nchi, naomba kutofautiana nawe kuwa wananchi hawa wanaosumbuliwa wanajitafutia riziki zao kwa njia halali. Kuuza chakula brbrn si njia halali hata kidogo, kupanga bidhaa brbrn si njia halali hata kidogo. Ni wazi sasa kwa sababu ya uzembe na uovu wa viongozi wetu tumezidisha chuki kwao hata pale wanapotekeleza majukumu yao ya kweli na kawaida.
 
hii nchi tunakoenda tutakuja uana wenywe kwa wenywe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…