Mkuu, Unadhani huyo aliyekuwa anaivaa alishindwa kuichoma?? Samahani nikupe kauzoefu kangu kidogo: Huko Denmark huruhusiwi kujiwashia moto hovyo eti unachoma takataka. Hiyo sio kazi yako - Wapo wenye kazi hiyo.
Taka aina tofauti-tofauti hutupwa kwenye mapipa zikiwemo pia na zile nguo-taka. Hizo nguo-taka huchambuliwa (sorted)na zile zinazoonekana zinaweza kutumika mahali pengine e.g. huko Tz, hutakaswa (sterilised) graded na kufungashwa marobota na kusafirishwa kama msaada au kuuzwa kama mitumba. i.e. nguo-taka zinakuwa Recycled. Hata chupi za mitumba ziliwahi kuwepo hapa Tz.
In short usichome wewe acha wanaolipwa kwa kazi hiyo waifanye. Zile ambazo ni "special case" choma au tumbukiza shimoni zijiozee zenyewe.