Hii inaonekana vipi katika hali ya kiroho?

kwa kweli sio kua nimeanza jana kuchoma no nishachoma sanaa sana na sjawah ona chochote kikitokea kwenye hii dunia ya macho ya nyama sjui huko kiroho
Mtu jamii fulani wanaweza tengeneza imani ya jambo fulani kwa mda mrefu, ikawa kama ndio reality yao,na kwenye jamii nyingine jambo hilo likawa ujinga tu na lisilo na maana yoyote.
 
Mtu jamii fulani wanaweza tengeneza imani ya jambo fulani kwa mda mrefu, ikawa kama ndio reality yao,na kwenye jamii nyingine jambo hilo likawa ujinga tu na lisilo na maana yoyote.
nimekupata vyema, kwamba nitakavyochukulia itakua hivohivo.
 
nii

fanyaje??
Utaratibu wa ku-dispose vitu chakavu ukoje? Sisi huku japo ni kijijini huwa tunatupa kwenye shimo la taka na baadaye watu wa usafi huvipeleka Dampo.? Kumbuka huko Dampo kuna baadhi ya watu huokota huko.
Nguo inayochomwa ni ile ambayo huitaki kabisa na haiwezi kutumika kwa vyovyote vile na mtu mwingine na haifai watu waione au iachwe kuzagaa hovyo e.g. pamba za usafi kwa Ke, Chupi za Me na Ke, bandeji zilizofungia vidonda, Pampas, n.k..
 
Mi nadhani ni Imani tu.
Nguo yenyewe utakuta ya mtumba waliotengeneza ni watu wa nje ya nchi na ilishavaliwa na mtu hata humjui.
Mkuu, Unadhani huyo aliyekuwa anaivaa alishindwa kuichoma?? Samahani nikupe kauzoefu kangu kidogo: Huko Denmark huruhusiwi kujiwashia moto hovyo eti unachoma takataka. Hiyo sio kazi yako - Wapo wenye kazi hiyo.
Taka aina tofauti-tofauti hutupwa kwenye mapipa zikiwemo pia na zile nguo-taka. Hizo nguo-taka huchambuliwa (sorted)na zile zinazoonekana zinaweza kutumika mahali pengine e.g. huko Tz, hutakaswa (sterilised) graded na kufungashwa marobota na kusafirishwa kama msaada au kuuzwa kama mitumba. i.e. nguo-taka zinakuwa Recycled. Hata chupi za mitumba ziliwahi kuwepo hapa Tz.
In short usichome wewe acha wanaolipwa kwa kazi hiyo waifanye. Zile ambazo ni "special case" choma au tumbukiza shimoni zijiozee zenyewe.
 
Hujaelewa mada soma vizuri mada then uje utoe tena maoni.
 
Hujaelewa mada soma vizuri mada then uje utoe tena maoni.
Inawezekana sijaelewa mada lakini mbona mtoa mada amesema 'Naomba kuuliza hii imekaaje kwa wale wanaojua mambo ya spiritual, kuhusu kuchoma nguo ambayo unaona imeisha na huwezi kuigawa solution ni kuchoma, je unaichoma tu moto au kuna manuizi fulani unanuia ........
Mimi nimesema:
In short usichome wewe acha wanaolipwa kwa kazi hiyo waifanye. Zile ambazo ni "special case" choma au tumbukiza shimoni zijiozee zenyewe.

Sasa mkuu; ni wapi nimechemka? Kama ni kuhusu Habari ya manuizi; hiyo haina mashiko kwa sababu huendi kuichoma wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…