Hii inaweza kuwa Picha Halisi au Picha Inayokaribiana kabisa na Mwonekano wa Yesu Kristo

Hii inaweza kuwa Picha Halisi au Picha Inayokaribiana kabisa na Mwonekano wa Yesu Kristo

1. si tamaduni za Wayahudi mwanaume kuwa na nywele ndefu
2. sanda za Wayahudi si kitambaa kimoja. Maiti hufungwa vitambaa vingi mfano wa Bendeji kuviringisha mwili wote (Rejea Injili zote zilivyoelezea maziko ya Yesu, ufufuko wake na vitambaa vilivyokutwa kaburini)
 
Tumsifu Yesu Kristo....
Bwana Yesu Afisiwe....

Tukiwa katika kipindi hiki cha kuelekea Pasaka, tuchukue muda kutafakari Mwanakondoo huyu, Sadaka na Kafara wa ulimwengu kwa ajili yetu, kwa namna alivyoamua kujitoa mwenyewe kutukomboa kupitia kifo chake.

Mada ya Shroud of Turin imeshapostiwa mara kadhaa hapa huku kukiwa na mitazamo tofauti kutoka kwa wana JF juu ya uhalisia wa sanda ya Yesu Kristo (nitaita tu Shroud au kitambaa) iliyohifadhiwa huko Turin, Itali. Picha hii ni ya mwanaume aliyelala huku akiwa amenyoosha mikono huku viganja vyake vikiwa vimefunika maeneo ya privates, huku kitambaa chenyewekikiwa na damu all over. Na Upande wa nyuma anaonekana mwili mzima (mkunjo wa nusu ya pili ya wa kitambaa kwa marefu). Ni picha ya mwanaume kijana anayekadiriwa kuwa na urefu wa kama futi 6 (yaani mrefu kabisa) na "well built muscles" yaani mwenye misuli inayoonesha alikuwa mtu wa kazi za mikono, na " a well groomed hair." Anakadiriwa kuwa na uzito kama 80kg hivi.

Picha hii inaonekana vizuri ikiangaliwa kama negative. Inaelezwa kuwa, mpiga picha wa kwanza hakuelewa vizuri alipokuwa anachukua picha hicho kitambaa lakini alipoangalia negative alipatwa na mshituko mkubwa sana kwa namna inavyoonekana kwa uhalisia.

Sasa kama tunavyojua faida za AI ikitumiwa vizuri, wataalam wamejaribu kuzipa uhai zaidi zile picha kutoka kwenye kile kitambaa ambacho kutokana kuungua, kukunjwa kwa muda mrefu na ajali ya moto ambayo kitambaa hiki kilipitia, kumekuwa na reflection kubwa kwenye kamera na kuathiri kwa kiasi fulani picha zake.
Ni picha nzuri sana ambayo huenda inatupatia fursa ya kumuona Mungu wetu Emmanuel yaani akiwa katika umbo la kibinadamu akizunguka Israeli yote miaka 2000 iliyopita.

Kwa nyongeza, mambo kadhaa ambayo labda huyajui kuhusu kitambaa hiki ni kama ifuatavyo.
  1. Damu kila Sehemu!: Shroud ina alama za damu zilizotapakaa kitambaa kizima na zinazolingana precisely na maelezo kwenye biblia. Tafiti za kimaabara zimethibitisha serum, na damu yenye kiwango kikubwa cha bilirubin. Bilirubin huzalishwa pale mtu anapopitia hali ya acute physical, emotional na hata psychological stress kiasi kwamba, seli nyekundu za damu huvunjika na kuvuja kwenye jasho. Hali hii hutokea nadra sana kwa binadamu na kisayansi inaitwa hematidrosis. Yesu alipitia hali hii angalau usiku ule kabla hajakamatwa Luka 22:44, Marko 14:32-36. Na aliendelea kupata majeraha na kuvuja damu hadi katika hali ya umauti wake. Kutokana na kiwango kikubwa cha pigment ya bilirubin, damu hii imebaki kuwa nyekundu hadi sasa, ( kwa kawaida damu hubadilika na kuwa nyeusi baada ya muda inapokuwa exposed to elements. Funny fact, damu zote za miujiza ya ekaristia nazo zimebaki katika hali hii hii duniani kote na zote ni type AB blood group common kwa watu wa Middle East hasa Waisraeli, to be precise). Hata jeraha la mkuki upande wake wa kulia limethibitishwa kutokana na uwingi wa damu iliyovujia kwenye kitambaa tofauti na upande wa kushoto ambako hakuchomwa.
  2. Ushahidi wa Pollen: Utafiti umebaini pollen zilizopatikana kwenye kitambaa hiki zinatokana na mimea inayopatikana katika maeneo la Yerusalemu au eneo ambalo kwa sasa ni huko Israeli na maeneo yanayozunguka tu eneo hili, na ni mimea ambayo hutoa maua nyakati za baada tu ya majira ya baridi (around March na Aprili)
  3. Picha ya 3D: Picha ya mwanaume anayeonekana kwenye kitambaa hiki iko katika ubora wa hali ya juu sana ya 3D, teknolojia ambayo ni mpya kabisa. Ni kitu cha ajabu kuwa, iwapo picha hii ni forgery, teknolojia ya 3D haikuwepo duniani hata ukisema ni kazi ya sanaa ya medieval era yote, bado hawakuwa na uwezo wa kutokeza picha kama hiyo. Sambamba na hilo, kuna uwiano sahihi mno baina ya viungo vya mwili (precisely proportional) isiyoweza kufanikisha kupitia kazi ya sanaa ya mikono, mfano uchoraji nk.
  4. Picha Yenyewe Ilivyotokeza: Picha hii haijatokeza kwa kuchorwa (hakuna rangi iliyotumika) , na haijajitokeza kwa kukwanguliwa. Kwa maelezo rahisi, picha hii ilipochunguzwa imeonekana imetokezwa kwa mionzi (UV rays), na mtaalam aliyechunguza picha hii anasema hadi sasa, hakuna teknolojia inayoweza kutokeza picha hiyo. Wataalam wa mionzi wamejaribu wameshindwa, au wakifanikiwa taswira ya object hupotea ndani ya muda mfupi tu au kila kitu kinaungua. Imeelezwa kuwa, ili picha hiyo itokee, inahitaji mwanga mkali sana upitishwe kwenye material kwa muda mfupi sana (milliseconds under very strong UV from a single source). Picha yenyewe iko juu sana ya kitambaa (very superficial) , kwamba ukichukua, mfano wembe ukwangue, picha hiyo itaondoka kabisa na kubaki kutambaa chenye damu tu. Yaani picha imetokeza kwenye sehemu ya nyuzinyuzi za juu kabisa za kitambaa wakati damu imetokeza hadi upande wa pili wa kitambaa. Hali hii inafanya kitambaa hiki kiwe displayed kwa nadra mno na inadhaniwa itachukua muda mrefu sana kukitoa tena hadharani kutokana na kuwa na public interest kubwa sana kwa sasa. Kwa sasa kimetunzwa kanisani huko Turin ndani ya bullet prove glass. NB: Kuna wakati miaka ya nyuma moto ulizuka hapo kanisani ambako kitambaa kimehifadhiwa, mtu mmoja alikimbia kuokoa boksi lililohifadhi kitamba hicho na alifanikiwa kutoa nje, moto ulipodhibitiwa, watu walishangaa mtu huyo aliwezaje kubeba hilo boksi peke yake, kwakuwa kulirejesha ndani ilihitaji msaada wa watu kadhaa.
  5. Mkanganyiko wa Carbon Dating: Hii ilikuwa moja ya point kuu kwa walioamini kuwa hiki kitambaa na contents zake zilikuwa fake. Tafiti za C14 za mwaka 1988 zilisummarize kuwa kitambaa hiki ni cha enzi za medieval yaani karne ya 5 hadi ya 15. Kwa lugha nyingine ni miaka kama 600 hadi zaidi ya miaka 1600 tangu Yesu kuondoka duniani. Ikumbukwe kuwa, kulitokea mvutani mkubwa sana wakati majibu haya yalipotolewa, maana haya ni majibu pekee yaliyoleta confusion. Watu waliomba raw data ziwe released, vyuo vilivyofanya tafiti hii vilikataa kutoa. Ilichukua zaidi ya miaka 20 na kwa amri ya mahakama hatimaye wakaachia data hizo, na ilionesha kuwa analysis za umri wa kitambaa zili-range kuanzia enzi za Kristo hadi nyakati za medieval. Kutokana na data hizo, ikaonekana vyuo vilifanya average ya hayo majibu ili kuja na huo umri wa kitambaa na hawakudisclose hilo kwenye report yao ( labda ni sababu kubwa iliyofanya wagome kwa muda mrefu kuachia raw data). Yaani walijumlisha na kugawanya wastani wa umri wa kila sample waliyochunguza kupata umri wa kitambaa. Sasa, kama nilivyoandika hapo juu, kitambaa hiki kilishaungua na kufanyiwa repair (masista kufuma kwa ustadi sehemu zilizokuwa zimeungua kukipa muonekano mzuri miaka kadhaa kabla ya huo utafiti). Kama haitoshi, sample ya vipimo vya utafiti huu wa awali zilikatwa sehemu moja tu pembeni, badala ya kuchukua sehemu tofauti tofauti za kutambaa hali iliyoleta majibu yenye biased na uwezekana kuwa, sehemu kubwa ya kitambaa iliyokatwa ni ile iliyofanyiwa repair. Utafiti uliofanywa mwaka jana (2024) umethibitisha kutambaa original kina umri wa zama za Kristo.
  6. Rekodi ya Kihistoria ya Shroud: Kuna uthibitisho wa matumizi ya picha ya muonekano wa Shroud of Turin ya muda mrefu kabla kitambaa hiki hakijawekwa public. Ikumbukwe kuwa kitambaa hiki kilikuwa owned privately kwa karne nyingi kwa usiri kwenye familia fulani bora na za kifalme na kurithishwa toka familia moja hadi nyingine. Michoro iliyogunduliwa huko Uturuki na hadi huko Ulaya Mashariki inaashiri watu walijua uwepo wa kitambaa hiki miaka mingi kabla. Hata DNA zimechunguzwa na kuwa watu toka mataifa mbalimbali walikigusa kitambaa hiki licha ya kwamba umaarufu wa kitambaa hiki umekuja baadaye sana hasa baada ya utafiti wa mwaka 1988. Swali ni je, watu walijuaje hadi watengeneza details za michoro na sanamu za Yesu zenye muonekano wa picha ya kitambaa hiki kama hawakujua uwepo wake? Wengi wanakubaliana kuwa, kutokana na ukweli kuwa, kuna nyakati fulani ilikuwa ni marufuku kuzungumzia habari za Yesu na watu waliokamatwa wakieneza injili walihukumiwa na kuuwawa na Watawala kwa muda mrefu, usiri wa hali ya juu sana ulihitajika ikiwa ni pamoja na mahali kilipokuwa kinahifadhiwa kitambaa hiki, lakini watu kwa siri walijua na walikiona kitambaa hiki kwa muda mrefu tu. Na hata katika Yohana 20:6-8, watu wanaamini kuwa, ni katika hali ya nguo ( damu na sura iliyobaki kwenye sanda zilivyokutwa kaburini) ziliwafanya wanafunzi wa Yesu waamini mara moja kuwa Yesu alifufuka. Ila kutokana na marufuku ya dini ya Kiyahudi katika kuhusianisha dini na picha na michoro, haikuwa sawa kuandika waliona sura ya Yesu kwenye sanda. Sambamba na hilo, Biblia haijasema zile nguo zilienda wapi, ikiashiria huenda usiri wa kutunza nguo zile ulianzia siku ile. Kwa kuwa kaburi lilikuwa liko wazi na halina mtu, ni dhahiri liliachwa hivyo kwa ajili ya kuzikia mwili mwingine kwa wenye kaburi lao kama ilivyokuwa desturi ya wakati ule (kumbuka makaburi hayakuchimbwa chini bali yalichimbwa kama kichumba kwenye mwamba na kufunikwa kwa jiwe lilichongwa kama tairi, ndiyo maana waliingia as wanaingia ndani ya nyumba wanainama tu kidogo, video za makaburi ya kale ya Wayahudi zipo all over YouTube)
  7. Uthibitisho wa Kisayansi wa Majeraha kwenye Kitambaa: Picha kwenye Shroud inalingana moja kwa moja na maelezo ya biblia kuhusu majeraha ambayo Yesu alipata. Kazi hii ilifanywa na timu ya forensic experts ( wale wataalam wanaongalia mwili au picha ya marehemu na kukuambia alikufaje?, aliuwawa?, na kama aliuwawa, aliuliwaje?). Waligundua mengi, mfano kupitia picha ya kwenye Shroud wamethibitisha uwepo wa vidonda vilivyotoboa viungio vya vidole vya mikono na sehemu ya nyayo za miguuni, jeraha kubwa kwenye mbavu, na damu nyingi kuvuja kichwani kunakoashiria taji la miiba kama inavyoelezewa, na katika hilo, inaonesha siyo tu taji liliwekwa juu ya kichwa, kwa kifupi taji lilishindiliwa kabisa kichwani na kutoboa vibaya kichwani na paji la uso na damu nyingi zilivuja uso mzima hadi maeneo ya karibu na macho na masikioni. Kama haitoshi, inakadiriwa alipigwa mijeredi zaidi ya 270 mwili mzima (zaidi kabisa ya ile ya wastani wa mijeredi 39-40 aliyopigwa mfungwa chini ya Utawala wa Kirumi kama historia inavyoonesha). Kuna ushahidi pia kuwa majeraha yalichimba kabisa ngozi, adhabu inayoendana na tamaduni zilizotumiwa na askari wa Kirumi kuwaadhibu wafungwa, ambapo walifunga vitu vyenye ncha kali for maximum pain. Kwa kifupi the punishment was severe and personal, aliteseka siyo kitoto ndiyo maana alikufa mapema kuliko wale wafungwa wengine (Yohana 19:31-34). It was even worse than what the Bible narrates but very consistent. Ndiyo maana akiwa katika mwili wa nyama, Yesu alifadhaika sana juu ya adhabu ile iliyokuwa inamjia given that alibeba uzito wa dhambi za ulimwengu wote!.
  8. Hakuna Mfupa ukiovunjika. Hakika picha hii inaonesha vizuri mifupa yake toka kichwani hadi vidole vya miguuni. Sayansi imethibitisha picha ya Shroud inaonesha hakuna mfupa uliovunjwa. Hii inaendana sawasawa na Biblia mfano katika Yohana 19:33-36. Iweje huyu mwanaume alichakazwe hivyo, bado hakuwa na kuvunjika hata mfupa wake mmoja.
  9. Sanda ya Kitajiri: Uchunguzi wa wanahistoria umethibitisha kuwa kitambaa hiki ni teknolojia ya ufumaji wa wataalamu wa enzi ya Kristo, lakini ilikuwa common tu kwa wenye hali nzuri kiuchumi, siyo watu masikini kama Yesu. Sasa utajiuliza kama Yesu aliishi maisha ya ufukara, iweje nguo ya bei mbaya itumike kumzikia? Well, kumbuka habari ya Yusufu wa Arimatheo ambaye Biblia inasema alikuwa mtu wa haki na tajiri, ( mfano Mathayo 27:57-60.) Huyu alitoa nguo ya thamani na kaburi jipya kabisa kwa ajili ya kumzika Yesu siku ile kuiwahi Sabato.

Wataalam wengi waliofanya study mbalimbali ya kitambaa hiki wala siyo waamini wa dini ya kikristo. Kanisa Katoliki liliruhusu wataalam wafanye tafiti kwa namna wanavyojua wao bila kuingilia kazi yao, yaani, waliruhusu sayansi iseme yenyewe, na experts duniani kote wametumika, ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu mbalimbali vikubwa duniani. Kitambaa hiki ni artifact, au kitu cha zamani lilochofanyiwa tafiti nyingi zaidi duniani . Wataalamu wengi wameweka wazi kuwa walienda wakiamini wanaenda kuprove kitambaa hiki kilikuwa fake. Matokeo yao, waliishia kusema ingawa hawajui picha ilitokeaje, lakini siyo forgery. Wengine wakawa Wakristo, kuna mwingine alifanya dedication katika maisha yake kufanya publication ya findings kwa kutengeneza website watu wajisomee na waamue wenyewe.

Licha ya wataalam wengine wa forensics kusema ni picha inayoonesha waziwazi mtu akiwa kwenye rigor mortis, yaani hali ya mwili kukakamaa muda fulani baada ya kufa, wengine wanasema picha hii huenda ilijitokeza katika ile moment ya kufufuka, likely kulikuwa na devine power kubwa ilivyoacha alama hiyo kwenye nguo baada ya kuyashinda mauti (kwamba ni picha ya mtu akiwa kwenye moment ya kuinuka).

Why kitambaa kina damu nyingi hivyo, je hakuoshwa kabla ya kuzikwa? Wachambuzi wa historia wanasema huenda hakuoshwa kutokana na sheria chini ya Utawala wa Kirumi kuzuia wafungwa kuoshwa, au muda haukutosha Sabato ilikaribia ilibidi waharakishe kuzika, au huwenda walimfuta kwa kitambaa na maji ila kwavile mwili ulikuwa "haujapoa vizuri" bado aliendelea kuvuja damu hadi anaingizwa kaburini.

Biblia inasema heri yao wale ambao hawakuona lakini waliamini. Huenda ni muhimu sasa na Mungu ametunza kumbukumbu hii kwa ajili ya wale ambao wataamini kwa kuona kama akina Tomaso. Whatever it is, it is indeed, very fascinating artifact!!!

Pic 1 and 3: AI modified image (zipo nyingi Google lakini zote zinaleta look inayoendana na hizo)
Pic 2: picha za awali za Shroud bila AI modification

Source ya information na picha ni Google searches, documentaries na online seminars za wachambuzi na wahubiri mbalimbali duniani.

Asanteni sana.
imani ni kuwa na uhakika na mambo yatarajiwayo na ni bayana ya MAMBO YASIYOONEKANA ..............................................................ww unataka picha??
 
1. si tamaduni za Wayahudi mwanaume kuwa na nywele ndefu
2. sanda za Wayahudi si kitambaa kimoja. Maiti hufungwa vitambaa vingi mfano wa Bendeji kuviringisha mwili wote (Rejea Injili zote zilivyoelezea maziko ya Yesu, ufufuko wake na vitambaa vilivyokutwa kaburini)
Sijaelewa essence yako ndugu. Ulitarajia vitambaa vyote vipatikane takribani miaka 2000 baadaye? Kitambaa cha usoni kipo Spain na kinafanana kabisa na majeraha yaliyoko kwenye Shroud. Ila hakina picha kwakuwa huwekwa juu ya kitambaa kikubwa.
 
Back
Top Bottom