Hii interview imenishangaza

Hii interview imenishangaza

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,275
Reaction score
3,316
Wakuu,


Sijui mimi ndiye mshamba wa haya mambo ya interview au vipi!

Kuna kampuni walinipigia niende kwenye interview, siku hiyo nimefika receptionist akanipokea vizuri then akanipeleka boardroom, nikajua kule ntakutana na panelists, cha ajabu nikakuta tu screen kubwa mezani. Then yule panelists akasema kwa kunitaja jina kuwa Joseph is here for interview.

Then nikaona watu wako kwenye screen wananikaribisha kwenye interview, wakajitambulisha kuwa mmoja alikua mmama wa makamo hivi akasema ni HR Manager wa hiyo kampuni na kwa muda huo alikua headquarters ya hiyo kampuni kwa ukanda wa Africa zilizopo Nairobi Kenya, na mwingine alikua ni mkaka mzungu,akajitambulisha kuwa ni General manager wa hiyo kampuni kwa tawi la Africa ila kwa wakati huo alikua anaongea kutoka London zilipo ofisi zao kuu kwa duniani.

Kilichonishangaza ni aina ya hiyo interview how comes interview ifanyike kwa njia ya zoom wakati pale ofisini kwao kuna watu wangeweza kutufanyia interview?

Changamoto niliyoipata ni kwamba maswali yao nilikua siyasikii vizuri sababu spika zilikua haziko poa hivyo kunilazimu kuwa kila muda naomba muuliza swali aulize swali upya ili nipate idea ya anachokiuliza.

Pia interview yao kwa kukadiria imeenda dakika nyingi almost 15-20 minutes kitu ambacho kwa mimi niliyezoea interview za utumishi zinazolast 5-7 minutes nimeona ni mashikolo mageni.pia wanauliza maswali mengi sana, waliniuliza karibu maswali 15 hivi kwa kukadiria.

So naomba tuelimishane, interview hizi za njia ya zoom ziko sahihi kweli au ni kuchoshana tu?
 
Duh wewe kweli mshamba sikuhizi interview hufanyika via Microsoft team popote pale hasa ka office Iko sehemu tofauti tofauti ni kawaida, sasa wewe kutaka waliobaki wakufanyie intrview hata vigezo hawana ni kichekesho.
 
Duh wewe kweli mshamba sikuhizi interview hufanyika via Microsoft team popote pale hasa ka office Iko sehemu tofauti tofauti ni kawaida, sasa wewe kutaka waliobaki wakufanyie intrview hata vigezo hawana ni kichekesho.
kilaza huyu na hapo ana degree gpa 4.5, yaani vyuo vyetu haviwapi kabisa hawa vijana exposure
 
Mkuu, inawezekana hujazoea interviews za Organizations ambazo zina international presence duniani, huo ni utaratibu wa kawaida kabisa wa interviews kwa mashirika ambayo international.

Na ni lazima kwa sababu key decision makers unakuta wako nje ya nchi kama hivyo London, Nairobi, Kwa hiyo ni lazima interview iwe virtually kama hizo zoom na zinazofanana na hizo. So, wengine wanakwepo nchini, ila ambao wako nje basi wana-join virtually. Inaonekana bado ni mgeni sana kwenye issues za interviews.

Huo muda wa interview pia ni kawaida kabisa, kwanza mbona ni mchache, usilinganishe na interviews za utumishi za dakika 5. Mimi nilishagonga interview lisaa limoja na nusu.

Kwa hiyo kaa kwa kutulia, endelea kumuomba Mungu uwe umepita upate hiyo kazi... Uzuri wa interview za hivyo hazina figisu, ni kwa merit tuu, kwa hiyo hata ukikosa huwezi ukasema kuwa ulipigwa fitna.

All the best.
 
Mkuu kutokana na changamoto ya covid muingiliano wa watu haushauriwi hivyo kampuni ambazo zinajali afya za watu wanafanya hata vikao vya ndani tu kwa zoom conference. Hivyo ni hali ya kawaida.

Kuhusu changamoto za kutokusikia maswali vizuri ni sahihi ulivyoomba mhusika arudie na pia ingewezekana ungeomba kibadilishiwa vifaa ili usikie vizuri.

Kuhusu muda wa interview kuwa dakika 15 hadi 20 hapo mkuu naona kama unatania asee. Yani hizo ni nyingi? Watu tulishawahi kupiga interview ukitumia saa moja zima wewe ndio umewahi kutoka kuliko wengine.
 
Duh wewe kweli mshamba sikuhizi interview hufanyika via Microsoft team popote pale hasa ka office Iko sehemu tofauti tofauti ni kawaida, sasa wewe kutaka waliobaki wakufanyie intrview hata vigezo hawana ni kichekesho.
Usiniite mshamba.kwani wewe unajua kila kitu hapa duniani?
 
Back
Top Bottom