Hii jeuri Mkurugenzi wa Kilimo Uyole anaipata wapi?

Hii jeuri Mkurugenzi wa Kilimo Uyole anaipata wapi?

kimpe

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
911
Reaction score
862
Jana niliona kwenye mitandao ya kijamii wananchi wakilalamika kuchukuliwa eneo lao na Taasisi ya Kilimo Uyole. nilipofuatilia hili suala ni kwamba lilishafanyiwa maamuzi miaka mitatu iliyopita na waziri wa Ardhi wa kipindi hicho Mh Lukuvi kwa kuwarudishia wananchi hekari zao 67 ambazo kilimo walizihitaji lakini wakashindwa kuzilipia fidia kwa miaka takribani ishirini.

Mbele ya Mbunge wa Mbeya ambaye ni spika wa Bunge ambaye aliwaombea wananchi hao na mgogoro huo ukatatuliwa lakini siku tatu zilizopita Mkurugenzi wa Kilimo kawapa tenda Suma JKT Uyole wajenge ukuta ndani ya makazi ya watu ambao wameshahamia kwa nia ya kutaka kulitwaa upya

Taharuki hii anaypianzisha mkurugenzi haijulikani ni nani yupo nyuma yake lakini kwa anayoyafanya ndo yale Miaka ya unanijua mimi nani wapeni haki zao wananchi kuwafidia hamuwezi
 
Wana eneo kubwa sana lakini bado wanataka maeneo ya wananchi, nashauri hii taasisi ipo katikati ya mji ihamishwe ilo eneo wauziwe wananchi ili wajenge
 
Wana eneo kubwa sana lakini bado wanataka maeneo ya wananchi, nashauri hii taasisi ipo katikati ya mji ihamishwe ilo eneo wauziwe wananchi ili wajenge
Ni kweli kabisa katikati ya jiji Alizeti zinafanya nini unganisha Uyole na Sae kwa majumba makali waende Inyala huko mapori kibao
 
Hapo kuna mkono wa wakubwa mkurugenzi kuna mtu anampa kiburi
 
Nchi Imejaa Muhari Sana, Anabatilisha Maamuzi
Nchi hii kila mwenye kacheo ni kambale nae ana sharubu, anaweza kukufokea muda wowote ule hata kama hakujuwi wwe ni nani! Basi unabaki kumwangalia na kumuomba msamahaa fake huku unatabasamu kama Mkwelee vile!![emoji3][emoji3]

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom