Hii jezi ni yenyewe au nimepigwa?

danhoport

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2020
Posts
1,984
Reaction score
4,502
Habari wana jamiiforum, mimi ni shabiki wa Simba na juzi hapa nilienda Sunderland Kariakoo kununua jezi mpya ya timu yangu ila kilichonishtua ni baada ya kuiscan ile QR code imetokea jezi tofauti na ile niliyoinunua japo iliyotokea ni ya Simba lakini mdhamini akiwa ni Sportpesa, mdhamini wa sasa ni Mbet,swali langu je hii jezi ni original au fake?
 
Sunderland ni wakala wa kuaminika wa hizi simba na yanga. Kwa sakata hili, shida ipo kwa simba. Msimu ulopita ukiscan ile barcode inakwambia jezi ni ya GSM, nadhani sote tunakumbuka hili. Jezi ni original, ondoa mashaka boss.

Sent from my SM-G930F using JamiiForums mobile app
 
Afadhali..
 
Simba si ilichachukua hela yake? Imebaki kwa Vunjabei na mashabiki, asiyetaka jezi anunue soksi
 
Hujapigwa kwasababu kama code ingekuwa fake isingeleta results zozote.

Inawezekana website admin haja-update picha mpya zinazopaswa kutokea ukiweka code. Hiyo code ipo kwenye database ndiyo maana imeleta results.
 
Simba anahusika nini?
Vunja bei hakuwa amejipanga kufanya production ya maana ktk hizi jezi, kwahiyo akaona bora atafute mtu mwenye uzoefu na mwenye pesa ya kuweza kumsaidia kupata hizo jez.

Akaenda kwa GSM, Barcode na QR code zote ukiscan ilikuwa inakuletea nguo zinazomilikuwa na GSM, yamkini GSM alifanya hivi ili Vunjabei huko mbeleni asije akamgeuka ndo maana akatumia barcode zake.

Tafuta nyuzi za mwaka jana tulizungumzia kwa mapana hili sakata. Labda nikuongezee kitu kimoja cha kutafakari, unafikiri ni kwanini Jezi za Simba zimekata mapema sana? Hakukuwa na Marketin Research kujua demand?

Ishu ilikuwa ni mtaji wa kutosha, mwaka jana vunjabei alishirikiana na GSM kufanya production ya uhakika na sote kwa sehemu tuliona hakukuwa na changamoto kubwa kama ya msimu huu.

Huu ni ndio uhalisia, nimeweka pembeni uSimba na uYanga, kama hutanielewa hapa, basi wengine wataendelea pale nilipoishie kukuelewesha zaidi.

Sent from my SM-G930F using JamiiForums mobile app
 
Yote uliyoyaongea hapo hayajibu swali langu....
Simba anahusika nini hiyo Error....
Maana ni nje ya circle yake.
 
Siko kwa ajili ya kuwaharibia watu biashara ila kuna wakati nilikwenda hapo nilitaka niwanunulie ndugu jezi za Simba na za Yanga, zile jezi za Yanga hazikiwa na ubora nikashangaa wanayanga wakijitapa kwamba jezi zao zina ubora mzuri, nikaacha kununua hizo jezi.

Nikatembelea duka la GSM yaani jezi nilizozikuta zina ubora nikawaambia mbona hizi jezi mlizonazo hapa zina ubora tofauti na nilizozikuta Sunderland, hawakunipa jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…