Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Jumikita kwa wale msiyojua kirefu chake ni Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii, wanawakilisha wanahabari wote wa mtandaoni nchini. Rais Samia anawasifia na kuwaambia mwende mkachuje yanayosemwa mtandaoni watu waseime wanayoyataka na nyie mnakenua na kuinama kuonesha mnashukuru na kupokea maagizo!
Mnajielewa kweli nyie? Yaani watu wanapigania uhuru wa vyombo vya habari halafu nyie mnakuwa sehemu ya kukwamisha juhudi hizi kwa kuungana na Raisi!
Eti chujeni wasiende kusema wanayotaka! Kutwa kuchwa ni uozo kila sehemu, serikali inanuka wizi na ubadhirifu, halafu unataka watu wote wawe kama hao nyuki wako akina Lucas Mwashambwa kusifia ovyo kama vile hawana vichwa!
Jumikita hamsathili kuwepo, nyinyi ndio mtakuwa wa kwanza kukandia wenzenu wanaotoa taarifa kwa maslahi ya umma. Ni kweli sasa hivi mazingira yamebadilika, kidogo ukatili umepungua, lakini uminywaji wa haki uko pale pale.
Rais Samia ungekuwa na mshauri mzuri hata mmoja leo ilikuwa ni nafasi nzuri ya kumaliza utata kuhusu suala la X na kuonesha kweli unaunga mkono suala la uhuru wa vyombo vya habari.
Akaitaja JF na Tanzania Leaks ili tu afikishe maagizo yake vizuri ya vyombo vya mtandaoni kufanyiwa censorship!
Hapa mama (kama anavyokuita Lucas Mwashambwa) unazidi kuchemka, unazidi kuharibu, mama ametukwamisha!
"Kwanza nawashukuru (JUMIKITA) kwa kazi nzuri mnayoifanya lakini mnawajibu wa kujichuja huko kuhakikisha.... Uhuru wa mawazo upo, mtu anaongea anayotaka lakini nyinyi mliofanya jumuiya kuangalia mawasilianano huko (chini) muweze kuchuja sasa na kuwaelewesha wale wengine wanaoandika wanavyotaka. Tutumie vyombo vyetu
"Kujenga nchi yetu na si kuboa. Watu wakisoma nje tunajibomoa wenyewe na sifa yetu Tanazania wanayoijua hawatuelewi. Unajua mimi nikienda nje na kufika kwenye mkutano na kukutana na wenzangu unasingia “Hongera sana Samia..” unajiuliza mh hongera za nini? Mngekuja huku kwetu mkasikia wanayosema? Lakini kumbe nje wanayaona na wanayapongeza sana, lakini njoo Tanzania!
"Kwahiyo JUMIKITA wanangu mkafanye kazi nzuri. Nawashukuru sana kwamba Makongamano haya yanawapa fursa ya kujitathmini je tunafanya vyema? Tumefika wapi? Tunakwendaje? Kwahiyo na katika vikundi vyenu vidogo vidogo hivyo hebu kakaeni kwenyewe na mjifanyie tathmini na kuona je kazi yetu inaleta matokeo Chanya au hasi. Hasi hayaachi kuwepi lakini yanaathiri kiasi gani katika nchi yetu? Nendeni mkafanye hiyo kazi lakini nawashukuru kwa kazi mnayoifanya ya kusambaza habari." - Rais Samia