Hii kasi ya Marekani kujisogeza kwetu baada ya kifo cha Rais Magufuli inatia shaka

Hii kasi ya Marekani kujisogeza kwetu baada ya kifo cha Rais Magufuli inatia shaka

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Kama nimekosea nisahihisheni. Serikali ya Marekani haijatoa rambirambi rasmi kwetu kufuatia kifo Cha Rais Magufuli.

Lakini Marekani inajisogeza Sana kwa mama wakidai kutaka kutupa 'misaada' ya kupambanana korona. Tusiwaonee aibu! Tuwaambie hatuhitaji msaada wa kupambana na korona! Kama Wana Nia ya kutupa msaada watupe pesa zitusaidie kumalizia SGR na mradi wa Stigler's George.

Wakapambane na korona huko kwao maana wao tatizo Ni kubwa kuliko kwetu! Hawa mabeberu hawana aibu.
 
Kuna ubaya gani kuwa marafiki na Marekani? Ni vizuri sana tupate misaada ya kuinua hali ya maisha ya watu wetu. Umeshasafiri sehemu za Tanzania ambako hadi sasa watu wanahangaika maji ya kunywa? Ni nyingi.

Asante Marekani kwa misaada yenu. Zingatieni maji, elimu, afya na barabara tafadhali.
 
Ujinga wetu na kuaminishwa na baadhi kwamba kuna mabeberu na tunatakiwa tuwe wana ‘Umajumuhi wa Kiafrika’ bila kuangalia hali halisi ya dunia ya kisasa ni shida

Huyo Mwendazake alitumia mbinu za zamani na kutengeneza maadui wa kufikirika tu ( Mabeberu) ili apate umaarufu wa kisiasa na yake mengine yaende kwa mkono wa chuma

Dunia yetu toka zama ni ya ushindani na ukiwa weak utapelekwa tu kuanzia ngazi ya mtu mmoja mpaka Taifa na kama tunataka tuwaepuke hawa so called mabeberu ni mkakati wa muda mrefu sana na labda hata uwe wa siri ( mpaka tuwe imara kusimamia kuanzia mifumo yetu ya siasa, uchumi, tamaduni nk )

Unamchukia beberu hata kusoma mikataba haujui, na bado unaona ufahari kula pesa za umma kwenye miradi na huduma za jamii kama madawa,madawati , mradi wa maji, umeme , bila kusahau unapanda vipandio vyao, unatumia simu zao na unajinasibisha hata kutumia lugha yao achia mbali ujinga wetu wa kujaza watu wa kabila, ndugu na dini tunazotoka eti ndo tunaweza pambana na Beberu na tunataka mpaka tumpangie nini cha kutupa kama msaada

Tuamke wa Afrika tunatakiwa mikakati imara na tuache ubinafsi ndo tunaweza pambana na hawa sijui mabeberu (USA na nchi za magharibi) sio ‘one man show’ ili kupata umaarufu wa kisiasa na kuendeleza ukandamizaji wa raia na kuwa na uhakika wa kula mali zao (wananchi)

Sorry nimejikita zaidi kwenye term ‘Beberu’ kama ulivyo ainisha hayo ya misaada ya korona na sijui SGR wataona wao inavyofaa
 
Kuna nchi zina vita na zenye majanga mbalimbali watu wanakufa kwa njaa ila Marekani katuona sisi ndio wahitaji zaidi wa msaada wake ni mahaba kiasi gani kutoka kwa wapendwa wetu Wamarekani.
Marekani akikusaidia sio lazima awe amekuona masikini kuliko wengine. Anatoa msaada sana kwa Israel, Kenya, Misri n.k. ambako hali sio mbaya. Kimsingi husaidia wale wanaoendana na mtazamo wao duniani. Mtazamo wao hauna ubaya kwetu.

Watu mnalia mitaani hakuna fedha. Mnadhani zitakujaje huko bila FDI na misaada kama hii ya WB, IMF na Marekani? Kwani wametupa CONDITIONS mbaya ili tupate hiyo misaada?

Msaada wowote wa fedha ambao conditions zake zinakubalika kwetu ni vizuri sana kuupokea.
 
Kama nimekosea nisahihisheni. Serikali ya Marekani haijatoa rambirambi rasmi kwetu kufuatia kifo Cha Rais Magufuli. Lakini Marekani inajisogeza Sana kwa mama wakidai kutaka kutupa 'misaada' ya kupambanana korona. Tusiwaonee aibu! Tuwaambie hatuhitaji msaada wa kupambana na korona! Kama Wana Nia ya kutupa msaada watupe pesa zitusaidie kumalizia SGR na mradi wa Stigler's George.
Wakapambane na korona huko kwao maana wao tatizo Ni kubwa kuliko kwetu! Hawa mabeberu hawana aibu!
Inatia dhaka?

Anyway, Marekani walitoa rambirambi na ushahidi huo hapo chini. Penda kujisumbua kupata taarifa sahihi kabla ya kuandika. Mengine sitachangia.

Screenshot_20210421-031238_Twitter.jpg

Screenshot_20210421-031252_Twitter.jpg
 
Ninakubaliana na wewe kuhusu wao ndio kuwa wachaguzi wa wapi panapohitaji msaada.

Haya makosa yamefanyika miaka mingi ya hawa watu kuleta vimisaada vyao visivyolenga kutatua matatizo yetu, bali kuwanufaisha wao zaidi.
 
Marekani akikusaidia sio lazima awe amekuona masikini kuliko wengine. Anatoa msaada sana kwa Israel, Kenya, Misri n.k. ambako hali sio mbaya. Kimsingi husaidia wale wanaoendana na mtazamo wao duniani. Mtazamo wao hauna ubaya kwetu.
Huko kote anayo maslahi makubwa zaidi. Hatoi tu msaada kumfurahisha mtu au kumfaidisha mpokeaji bila yeye kufaidika zaidi.
 
Kuna ubaya gani kuwa marafiki na Marekani? Ni vizuri sana tupate misaada ya kuinua hali ya maisha ya watu wetu. Umeshasafiri sehemu za Tanzania ambako hadi sasa watu wanahangaika maji ya kunywa? Ni nyingi.

Asante Marekani kwa misaada yenu. Zingatieni maji, elimu, afya na barabara tafadhali.
Huko Moshi hakuna Maji? Hakuna shule? KCMC imefungwa lini? Barabara za lami toka mjini hadi kilema zimehama?
 
Kama nimekosea nisahihisheni. Serikali ya Marekani haijatoa rambirambi rasmi kwetu kufuatia kifo Cha Rais Magufuli.

Lakini Marekani inajisogeza Sana kwa mama wakidai kutaka kutupa 'misaada' ya kupambanana korona. Tusiwaonee aibu! Tuwaambie hatuhitaji msaada wa kupambana na korona! Kama Wana Nia ya kutupa msaada watupe pesa zitusaidie kumalizia SGR na mradi wa Stigler's George.

Wakapambane na korona huko kwao maana wao tatizo Ni kubwa kuliko kwetu! Hawa mabeberu hawana aibu!
Nadhani unaishi kwenye wakati usio wako. Ulistahili kuishi miaka ya 1800.
 
Back
Top Bottom