Ujinga wetu na kuaminiswa na baadhi kwamba kuna kuna mabeberu na tunatakiwa tuwe wana ‘Umajumuhi wa Kiafrika’ bila kuangalia hali halisi ya dunia ya kisasa ni shida
Huyo Mwendazake alitumia mbinu za zamani na kutengeneza maadui wa kufikirika tu ( Mabeberu) ili apate umaarufu wa kisiasa na yake mengine yaende kwa mkono wa chuma
Dunia yetu toka zama ni ya ushindani na ukiwa weak utapelekwa tu kuanzia ngazi ya mtu mmoja mpaka Taifa na kama tunataka tuwaepuke hawa so called mabeberu ni mkakati wa muda mrefu sana na labda hata uwe wa siri ( mpaka tuwe imara kusimamia kuanzia mifumo yetu ya siasa, uchumi, tamaduni nk )
Unamchukia beberu hata kusoma mikataba haujui, na bado unaona ufahari kula pesa za umma kama madawa,madawati , mradi wa maji, umeme , bila kusahau unapanda vipandio vyao, unatumia simu zao na unajinasibisha hata kutumia lugha yao achia mbali ujinga wetu wa kujaza watu wa kabila, ndugu na dini tunazotoka eti ndo tunaweza pambana na Beberu na tunataka mpaka tumpangie nini cha kutupa kama msaada
Tuamke wa Afrika tunatakiwa mikakati imara na tuache ubinafsi ndo tunaweza pambana na hawa sijui mabeberu (USA na nchi za magharibi) sio ‘one man show’ ili kupata umaarufu wa kisiasa na kuendeleza ukandamizaji wa raia na kuwa na uhakika wa kula mali zao (wananchi)
Sorry nimejikita zaidi kwenye term ‘Beberu’ kama ulivyo ainisha hayo ya misaada ya korona na sijui SGR wataona wao inavyofaa