Hii kauli ya kocha wa Red Arrows ina maana gani?

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Baada ya mechi kwisha alihojiwa akasema.

"Hali ya hewa haikuwa nzuri Ila maamuzi ya refa yalitugharimu kwakuwa alitoka ukanda huu,tutarudiana na pia refa atatoka ukanda wetu"

NB: Simba waanze mkakati wa kujipanga magoli yasirudi , benchi la ufundi ijipange mapema kuhusu hiyo kauli maana inaonyesha tutafanyiwa ngojera.
 
Naomba kueleweshwa kidogo kuhusiana na hili, hivi ikitokea tumepigwa goli 3 bila kule, si ndo tunaenda kwa faida ya goli la ugenini au inakuaje?
 
Si ni kama Ile ya jwaneng Galaxy, mzani ulisoma 3-3 wao wakaenda ..
Ile ilikuwa tofauti... Wao walitufunga nyingi kwetu, kama tungeshinda 2-0 kwetu kisha kwao wakashinda 3-1 hapo aggregate ni 3-3, simba angeenda kwa faida ya goli la ugenini..

Ila hii ya juzi, kwao tulifunga na kwetu wakafunga, hivyo hakuna wa kuhesabiwa goli la ugenini, ila wanaangalia nani kafungwa mengi kwake.
 
Jana tulikosa umakini tu ila hakukua na element ya dharau kabisa. Wachezaji walipambana sana.

Red Arrows washaelekea kibla tayari wale
Tuombe dua wasipindue meza kibabe.
 
Kwa Simba hii, mishare myekundu lazima wakae.
 
Simba wamshitaki CAF kwani ni kiashiria cha kupanga matokeo na pia ni tuhuma kwa CAF wanaopanga hao waamuzi.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo refa alikuwa akichukua mipira na kuiingiza golini kwao halafu anasema ni goli!
 
Naomba kueleweshwa kidogo kuhusiana na hili, hivi ikitokea tumepigwa goli 3 bila kule, si ndo tunaenda kwa faida ya goli la ugenini au inakuaje ??
Tukipata goli la ugenini kule watapata wakati mgumu ,ila 3-0 tunaenda extra ,2-0 tunapita . Ni kufanya juu chini Simba wapate draw yoyote
 
Ukubwa hauzungumzwi unaonekana kwa macho.huwezi kusikia Al ahl wakisema sisi ni timu kubwa utajionea Mwenyewe..
Jamaa hata kwenye page yao ukiangalia wengi wanacoment hawashangazwi na matokeo Simba ni timu kubwa kwao
 
Baada ya mechi kwisha alihojiwa akasema.

"Hali ya hewa haikuwa nzuri Ila maamuzi ya refa yalitugharimu kwakuwa alitoka ukanda huu,tutarudiana na pia refa atatoka ukanda wetu"..
Hii habari umeifupisha sana, kasema hata kabla ya mechi walifanya kautafiti kadogo kupitia zao walio Uganda na wakaambiwa kile kile kilichotokea uwanjani (matokeo ya mchongo).

Sasa kasema mechi ya marudiano refa anatoka ukanda wao na wanaweza kufanya kinacholalamikiwa na zaidi. Pia kasema angalau wengefungwa na timu nzuri asingelalamika, ila amefungwa na timu yenye mchezaji mmoja (Morrison ) huku refa akiwa man of the match.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…