Hii kauli ya "Mwenye nacho huongezewa" naona kama ina ukweli

Hii kauli ya "Mwenye nacho huongezewa" naona kama ina ukweli

bafetimbi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2018
Posts
1,085
Reaction score
1,741
Habari wazee,

Nimechunguza kwa muda mrefu sana nikagundua kwamba hii kauli au msemo unaukweli kwa asilimia kubwa sana. Na sijajua ni kwanini hii kauli inatimia kwa urahisi sana kwa wenye nacho, wasionacho hupata kwa taabu sana na hata wakipata hakidumu na wanarudi tena kwenye msoto.

Angalia hata kwenye kubeti unatafuta Odds mbili ambazo unaamini ni za uhakika unaweka jero yako upate buku kisha utafute zingine mbili uweke buku ije buku mbili lakini cha ajabu unaliwa hata kile kidogo ulichonacho. Anatokea mtu huko anaweka laki tano kwa Odds mbili anapiga milioni, anatafuta tena Odds mbili anaweka ile milioni anapiga milioni mbili yaani kiurahisi tu, lakini wewe na vijero vyako kwa Odds hizo hizo mbili upate buku unapukutishwa ghafla bin Vuu....... Huu mfano nilioutoa kuhusu betting nina ushahidi nao kabisaa. Naomba kwa wale wenye ufahamu wa mambo tofauti tofauti

mnisaidie kuyafahamu mambo haya matatu:

NI KWA NINI?

Ukiwa na pesa ni rahisi sana kupata zingine.

Ukifahamiana sana na watu neo ulipo, hata ukienda ugenini watu watakua wanajilengesha kwako kiurahisi tu ili mfahamiane.

Ukiwa na mpenzi mmoja ni rahisi sana kumpata mwingine na mwingine tena.

Kitaalam ni kipi kinatokea ambapo hivyo vitu vitatu hupatikana kwa urahisi ukiwa tayari unavyo?

Karibuni.
 
hapo kwenye betting ukiona mtu kaweka jero ujue kaweka team kuanzia kumi na kuendelea alaf ajabu yake anakosa team mbili au moja, unaliwa kila siku
 
Back
Top Bottom