Hii kesi hii sijui kama anaweza chomoka!?


Kimsingi, Jamhuri haiwezi kumfanya mtu awajibike moja kwa moja kwa kitendo kilichotokea Oktoba 2025 kwa sababu tu alisema Aprili 2025 kwamba kitafanyika, bila kuthibitisha uhusiano wa kisheria unaohitajika kati yake na tukio hilo.

Wanapaswa kuonyesha ushahidi unaounganisha mtuhumiwa na kitendo hicho, kwa mfano mawasiliano, maagizo, mipango, watu aliowatuma, fedha, au ushahidi mwingine unaoonyesha kwamba hata akiwa mahabusu alikuwa bado anaendesha au kushiriki mpango huo.
 

Usaliti?
Usaliti kwenye kitu gani?
Raia wa kawaida haweziitwa msaliti.
Usaliti unahusu makubaliano. Sio nje ya hapo. Dudukwe au wewe huna uwezo wa kuisaliti nchi yako kama ni raia wa kawaida.
Labda kama mlifanya makubaliano fulani.
Ndio maana kuna Viapo.
Au labda wewe tangu umezaliwa kuna sehemu uliapishwa na kukubaliana kuhusu nchi yako. Ndio unaweza kuwa msaliti.

Iko hivi, hii Dunia mambo ya nchi, utaifa yapo kisiasa, nje ya hapo hapana mipaka, ndio maana leo hii nchi inaweza kuwa Tanganyika kesho ikawa Na jina jingine kabisa na mipaka mingine kabisa.
Wanaosaliti nchi ni waliokula viapo.

Kingine kuna tofauti kubwa kati ya Usaliti na uhaini.
Mhaini ni mtu yeyote anayetaka, mwenye nia, au anayetaka kupindua serikali iliyopo madarakani. Huyo ni mhaini.
Msaliti ni mtu aliyegeuka, aliyeasi makubaliano. Huyo ni msaliti.

Tukirudi kwenye mjadala.
Suala la Niffer lilikuwa kisiasa.
Wewe kusema utagawa barakoa kwa watakao Andamana sio kosa. Ukizingatia maandamano yapo kisheria na yapo kikatiba.

Watu kufanya vurugu siku ya maandamano haihusiani na Niffer kugawa barakoa au kusema atagawa barakoa. Hakuna uhusiano..

Kwenye maandamano kunakuwaga na mabomu ya machozi ni kweli kwa sababu kunatokea vurugu. Kwa sababu sio watu wote wanaweza kuandamana bila vurugu. Hivyo kuwaambia watu waende na maji na barakoa sio kosa kisheria.

Mtu anaweza kubeba barakoa kwa sababu ya vumbi kutokana na Umati, afya kutokana Umati kuwa mkubwa na watu wanaafya tofauti, na kubeba maji kwa sababu ya kunywa.

Hivyo kisheria huwezi mkuta na hatia mtu aliyesema mbebe maji na barakoa kwenye maandamano au nitawapa maji na barakoa.
Labda uamue kumuonea tuu lakini sio kosa.

Kwenye maandamano hata halali uhalifu unaweza kutokea ndio maana polisi wanakuwepo.

Kwenye mechi tu za Simba na yanga uhalifu unatokeaga, watu wanaharibu uwanja wanang'oa viti n.k.
 
Lissu aliweka pingamizi on number of issues, ikiwemo kwenye admissibility ya flash kwa hoja kwamba shahidi aliyetaka kutoa flash ile kama kielelezo wasnt competent to do so.
 

Kuna mawili hapa naomba uyafahamu.
1. Kifungu cha 129 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 kinakataza matumizi ya nguvu, vitisho, utekaji, au hila yoyote kumshawishi au kumzuia mpiga kura kushiriki au kutoshiriki katika uchaguzi. Kitendo hiki kinatafsiriwa kisheria kuwa ni kosa la ushawishi mbaya (undue influence).

2. Kuchoma mali Yoyote ya Serikali, Ya Umma ni kosa la Kigaidi.
Hii ni sheria ya TZ.

Kwahiyo kama Umehamasisha watu na kweli wakafanya fujo kujaribu kuzuia uchaguzi una kosa namba 1 hapo juu. Na kama fujo ikawafanya wakachoma mali. Unakuwa na kosa namba 2. Na unapewa mashtaka yote mawili.
La kwanza lina dhamana ila la Pili halina.

na Kuhusu Uhaini.
Uhaini limetokana na neno la kiarabu "khiyana", yaani Usaliti.
Na sio lazima mpaka uwe na mkabata alaf ukienda kinyume ndio uitwe usaliti.
 
Lissu ameshinda kesi kwa mstari wako wa kwanza....

Maana kuchoma ofisi za Serikali..labda kama Tarehe 29 October walimuachia akaja mtaani akachoma moto ofisi na kurudi Ukonga
 
Lissu ameshinda kesi kwa mstari wako wa kwanza....

Maana kuchoma ofisi za Serikali..labda kama Tarehe 29 October walimuachia akaja mtaani akachoma moto ofisi na kurudi Ukonga
Sahihi Lissu anashinda.

Ila turudi kwenye mantiki ambayo mawakili wa serikali wanapambana kuiweka.
Wao wanataka kuonyesha kuwa yale maneno ndio yalisababisha watu kuchoma majengo ya serikali.

Je hapa umenipata?.
 
Hata akihukumiwa atakuwa kahukumiwa na mashetani zaidi yake bora hata huyo abaki wale wanaomshitaki wanyongwe kwa ubaya wao waliofanya siku nyingi. Viva viva TAL
 
Vurugu zile wapo JKT ambao walipewa ahadi ya ajira na Jiwe wa Chato baada ya kufyatua maelfu ya tofani kushiriki ujenzi wa Chamwino...wakaachwa mtaani...

Wapo JWTZ...

Wapo CCM...Tena wengi sana... Wengine waliachwa au kukatwa na mavikao yao huko Lumumba

Wapo CHADEMA ...Hawa wameumizwa vibaya sana...unaenda Mahakamani kuhudhuria kesi ya Lissu...Polisi wanaachia mbwa watu wanang'atwa..
Polisi walichukua wafuasi zaidi ya 100 wakatupwa porini, wakachapwa mijeledi mgongoni na wengine kuvunjwa miguu

Yapo baadhi ya Makanisa...yalifungiwa...
Hao walipiga show ya kibabe sana..

Serikali ilisababisha No reforms No Election baada ya madudu yaliyopitiliza Uchaguzi wa Serikali ya mitaa mwaka 2024..

Sasa sijui kama wataamua kubadilika ili chaguzi ziwe na maana...huko mbeleni sijui....sijui
 
Sanduku la Pandora likifunguka si ndo safi sasa serikali ipate aibu vizuri? Yaani nyumbu hamjiulizi inakuwaje lissu aihurumie serikali eti ushahidi huu mnaotoa utawaleteeni aibu hii na hii ohh sijui italazimika samia naye aje atoe ushahidi!! Sasa adui yako anataka kujichanganya wewe unamsahihisha si umwache ayakoroge ili umunyweshe vizuri?
Mie nawaambieni leo lissu anakalangwa mpaka mtapoteana nyie nyumbu!!
 

Lisu hajazuia wapiga kura wasipige kura.
Hajawahi kuwashawishi wapiga kura wasipige kura.
Yeye alikuwa anawaambia watu ambao watu hao walikuwepo watoto, wakubwa, wanaume, wanawake.
Hakuwa anahutubia wapiga kura.

Wewe utajuaje huyu ni mpiga kura au sio mpiga kura kwa kumuangalia?

Wapiga kura wanapatikana siku ya uchaguzi tena kwenye vituo vya kura huko. Je Lisu au kuna mtu alienda kuwashawishi wasipige kura au wafanye vurugu?

Kisheria ili mtu awe mpiga kura anatakiwa aweje? Chukulia hana kitambulisho kabisa

Ndio maana kwenye mikutano ya siasa wakati wakampeni wanaoenda kusikiliza ni watu sio wapiga kura.

Tukirudi kwenye uhaini Vs Usaliti.
uhaini unaweza kuhusisha mambo kama:
Kujaribu kuipindua Serikali kwa nguvu au kwa njia haramu.
Kuanzisha au kusaidia uasi wa kutumia nguvu dhidi ya Serikali.
Kushirikiana na adui wa nchi kwa namna inayohatarisha usalama wa taifa.
Kufanya vitendo vingine ambavyo sheria ya nchi imevitaja mahsusi kuwa uhaini
 
😂😂😂 wamechelewa sana mkuu
Soma hati ya mashitaka hayo hayapo kabisa ni habari ya ndoto za mchana hivyo hayo usemayo hayapo mbele ya mahakama kuu kilichopo ni kile kilicho andikwa kwenye hati ya mashitaka.
 
Nyie ndio mnamdanganya Samia kuwa Lissu ana kesi ya kujibu kwa sababu ya maelezo yaliyoandikwa “chini ya usimamizi” ? Madogo wote walilazimishwa kukiri kama bait ya kuachiliwa huru.

Sidhani kama kuna mjinga asiyefahamu sifa za ushahidi.


Next time muwe mnafikiria vizuri mkiwa mnaandaa mashtaka. Hii tabia ya kuwasilikiza polisi na tisi form fo felia, incompetents ndio inayowafanya sasa mnaona aibu kwenda mbele na kurudi nyuma juu ya hii kesi.
 
Huwa una kaujinga kakomavu kwenye DNA yako.Hata tukijidai tunakuwahi,hakuna tutakachofanya kukuokoa.
 
KWA ROHO SAFI TENA NYEUPE NAIOMBA MAHAKAMA NA DPP WAONE HILI NA KWA HEKIMA APEWE ONYO JUU YA KAULI ZAKE NA AWE HURU,LAKINI SI HURU KABISA HAPANA CHINI YA UANGALIZI MAALUM KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO!
#IKAWE HIVYO AMEN.
Hatutaki huruma, kesi ifutwe au iendelee…..
 
Hiyo ni mifano ya kufikirika tu. Kisheria kuna kitu kinaitwa circumstantial evidence , na mara nyingi unakuwaga dhaifu sana ukikutana na mawakili makini. Usijidanganye kabisa kwamba hapo kuna kesi ya maana.
Upuuzi wa CCM tu..huwezi kusababishia maumivu ya kichwa Majaji ..wajenge picha ya vitu vichwani mwao.visivyokuwepo kwa kuviona!!!
Utetezi umejaa maneno ya Video na Flash ..ambazo Majaji hata hawana na hakuna namna ya kuvipata!!!
 
Hujui unaloongea ww, mashitaka yaliyoko hapo ni mengine, kinachofanyika ni kukubali amewashinda na kumuachia, kisha kumfungulia mashitaka mengine ya hicho mnachodhani mtamuweza. Mbona ni rahisi tu, siku hizi kila mara mnashindwa, na kufungua mashitaka mengine, na sio kukoroga nje ya utaratibu. Kama mmelewa madaraka hadi hamfuati utaratibu, basi mnafundishwa kufuata utaratibu. Umeelewa au nikupe dozi nyingine?
 
Ukahidi haulipi?,nitishie utanikata mapanga,niripoti tishio, halafu miezi mitano mbele nikatwe kweli mapanga uone kesi itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…