Hii kitu haikubaliki, hii nchi udini umeota mizizi sasa

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
SAKATA LA KUPOTEA RAJAB OMARI MTANA KIJIJI CHA LULAGO HANDENI 2013 NA HUKUMU YA KUNYONGWA MASHEIKH 10 TANGA 2013

Waislam 10 wamehukumiwa kunyongwa kwa tuhuma za kuua mlinzi mmoja.

Kufikia hukumu hii kuna mengi na chanzo chake kilianzia katika biashara ya hiliki na malipo ya ushuru kijijini Lulago.

Ninaanza leo kueleza kisa hiki kama nilivyotafiti na kuweka kumbukumbu miaka 10 iliyopita.

Rajab Omar Mtana alikuwa mwanakijiji wa kawaida tu akiishi kijijini Lulago, Handeni kama wanavijiji wengine wanavyoishi na alikuwa na biashara yake ya kuuza hiliki kama mkulima wa zao hilo.

Siku moja akaja mnunuzi mfanyabiashara wa hiliki nyumbani kwake kununua hiliki na akamuuzia.

Yule mfanyabiashara alipokuwa anatoka na gari yake akasimama kwenye kizuizi cha kulipia ushuru.

Alipotakiwa kulipa ushuru akasema kuwa si hiliki yote amenunua katika kijiji hicho kwa hiyo hawezi kulipa ushuru wa hiliki yote.

Hapo palitokea ubishi na mfanyabiashara yule akagonga lile geti na akaondoka.

Hii ikapelekea kwa wakusanya ushuru wa hapo kijijini kwenda nyumbani kwa Rajab Omar Mtana kumkamata na kumweka chini ya ulinzi katika ofisi ya serikali ya kijiji hadi hapo atakapolipa ushuru ambao yule mfanyabiashara alitakiwa alipe.

Ndugu zake Rajab Omar Mtana wakaenda pale ofisini kwa nia ya kumtoa ndugu yao na hapo pakatokea vurugu na mapigano.

Katika mapigano hayo, mgambo ambae ndiye aliyekuwa akishughulika na kudai ushuru akauawa.

Kisa hiki cha ushuru wa hiliki ndicho kilichozua balaa kubwa la mauaji na uchomwaji moto nyumba za Waislam wa kijiji cha jirani cha Madina na kuvunjwa kwa misikiti katika vijiji ambavyo vilikuwa na idadi kubwa ya wakazi wake Waislam.

Baada ya haya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akatoa amri kuwa hapana ruhusa tena ya sehemu hizo kuwa makazi kwa kuwa hizo ni kambi za ugaidi.

Mkuu wa Mkoa alisema mengi ambayo takriban yote yamedhihirika baadae kuwa hayakuwa na ukweli.

Mkuu wa Mkoa alisema kuwa wapo Al Shabab vijijini, kumechimbwa mahandaki ya vita katika vijiji na kuna silaha za kutungulia ndege nk. nk.

Mkuu wa Mkoa alizungumza na Radio Nuur, Tanga inayomilokiwa na Msikiti wa Ibadh.
Nilifunga safari hadi Radio Nuur Tanga kwa nia ya kupata taarifa kamili yalivyorushwa.

Radio Nuur waliogopa kunipa juu wala kuniruhusu kusikiliza kipindi hicho cha Mkuu wa Mkoa ingawa kabla sijahama Tanga nilikuwa mmoja wa Wakurugenzu wa radio hiyo.

Lakini niliwahoji watu waliosikia kipindi hicho.

Katika Waislam waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani Handeni ni huyu kijana Rajab Omari Mtana.

Baada ya kukaa rumande alipata dhamana yeye pamoja na wenzake na akawa nje.
Rajab Omar Mtana alirejea kijijini kwake.

Wakati anakaribia kuingia kijijini alisimamishwa na askari wa kijiji akapekuliwa na akanyang'anywa simu yake na fedha taslimu.

Baada ya mkasa huu walimwachia na yeye akaendelea na safari yake.

Lakini wakati akiwa rumande nyumba yake ilikuwa imevurugwa haifai kuishi mtu kwa hiyo alifikia kwa dada yake.

Akiwa nyumbani kwa dada yake alifatwa na watu wa serikali ya kijiji usiku akatolewa ndani na kuanza kupigwa kwa bakora na kisha kwa mapanga.

Kujitetea kijana huyu alikimbia huku akikimbizwa.
Asubuhi kulipokucha palionekana damu nyingi sana.

Taarifa ilitolewa polisi lakini hakuna kilichofanyika.
Polisi walitoa taarifa (SON/RB346/2014).

Dada yake na mumewe walikamatwa na kushitakiwa katika mahakama ya hapo kijijini na wakapigwa faini ya kila mtu shs. 20.000.

Kosa lao ni kumleta kijiji Rajab Omari Mtana mtu asiyetakiwa.

Miaka 10 imetimia Rajab Omar Mtana hajulikani alipo na inasadikiwa ameuawa na wale waliokuja kumtoa nyumbani kwa dada yake.

Rajab Omar Mtana ametafutwa kote hajapatikana na waliompiga na kumjeruhi wako huru nje hawajaguswa wala kuhojiwa na polisi.

Lakini wale waliotumiwa kwa mauaji ya mlinzi wa kijiji wamehukumiwa kifo.

Hapa kuna mengi sana ya kufikirisha mbali ya yale kuwa kulikuwapo na silaha za kutungua ndege katika vijiji hivi vya Waislam wa Handeni vilivyokuwa na nyumba za nyasi na udongo.

# mods acheni huu uzi na nyie acheni udini wenu#
 
Attachments

  • FB_IMG_1687703290421.jpg
    FB_IMG_1687703290421.jpg
    58.3 KB · Views: 3
Mkuu wewe ndiye unaeleta huo udini. Hao unaosema walikanatwa, wakadhtakiwa na hatimaye kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa hawakukamatwa Kwa misingi ya kidini bali walikamatwa Kwa misingi ya uhalifu.

Au Kuna wasio waislamu ambayo walifanya uhalifu huo lakini hawakushtakiwa Kwa sababu tu siyo waislamu?
 
Huyo mkuu wa mkoa dhehebu gani mkuu?
 
Wewe ndo unaleta udini, halafu hoja yako haina mashiko kwa sababu ni ya upande mmoja
 
Mshtakiwa wa kesi ya mauaji haonekani, afu mnailaumu serikali, Mbona iko wazi, kakimbia hukumu.
Pamoja na kuandika story ya upande mmoja lakini iko wazi hukumu ni halali kwani waliua, na huyo kijana kakimbia.
Nyie wenzetu kutwa kulialia mnataka nini? Tuondoke tuwaachie hii nchi au?
 
Siku hizi Huwa polisi hawataki tabu wanakupa tu kesi ya ugaidi ili wakuue

Alafu polisi wakishastaafu wanajifanya wanajifanya wazee wakanisa au wanaswali swafu sa mbele misikitini

Huyo galawa sijui yupo wapi kwa sasa
 
Sasa udini uko wapi hapo! Mimi naona tu kulikuwa na makosa ya mauaji kwa mgambo, na watuhumiwa kuhukumiwa kifo na mahakama. Na kama upande wa washtakiwa kama haujaridhika na hiyo hukumu, bado wana nafasi ya kukata rufaa.

By the way, huyo Mkuu wa Mkoa wa wakati Chiku Galawa angekuwa ni mtu wq imani nyingine, ungepata kisingizio. Ila kwa bahati mbaya nakumbuka ni mwenzenu huyo! Na muda wote nilimuona akivaa kiremba kichwani. Una maoni gani juu ya hili?
 
Back
Top Bottom