Hii kitu siku siyo ya kuisahau kabisaaa..........

basha unguja

Member
Joined
Sep 28, 2016
Posts
83
Reaction score
77
Wanajamvi kwanza wasaaalam!

Napenda kushare nanyi hii siku ambayo ilikuwa kizungu mkuti lakini yote ikiwa ni utoto plus utundu.

Tukiwa na tabia ya kudandia magari mimi na wenzangu siku moja ilipita gari aina ya TATA kubwa ambalo limefunikwa kwa maturubai kwa nyuma na sehemu ya mlango wa nyuma ikina wazi...Tulipoliona gari linakuja mimi na wenzangu wapatao watatu na mimi nikiwa manne tukalisubiri lipunguze mwendo kwa kuwa barabara haikuwa nzuri sana.

Kweli gari ilipunguza mwendo , kama makomandoo tukadandia kwa ustadi mkubwa, wote wanne tukawa ndani ya gari ..Baada ya hapo tukaridhika kuwa tumefanikiwa sasa issue ikawa kushuka daaaah! dereva ndiyo kwaaaaanza anakanyaga wese....Sasa kwa hofu tuliyonayo tukasema tujifiche mulemule ndani bila kujua gari inaenda wapi...

Baada ya mwendo mrefu gari ikasimama.. tukajaribu kuchungulia nje tukiwa mule ndani kumbe bwana tumeingia kambi ye JESHI daaah! Nakumbuka nilipowaambia wenzangu kuwa tupo ke kambi ya jeshi mmoja kwa upoleee akajisemea tu TOBAAAAA ..

Busara tuliyoitumia ni kushuka wenyewe na kujisalimisha kwa kuoonyesha mikono juu....Wale wanajeshi waliokuwa pale walishangaa huku wengine wakicheka wakiwa hawaelewi kinachoendelea, Dereva naye akashikwa na butwaa...

Tukawa wawazi pale kuwa ndiyo kamchezo ketu ila siku hiyo ilikuwa arobaini yetu ....wakatusamehe wakati wa kurudi tulirudishwa hadi tulipodandia na kuonywa tusifanye tena aseeeee......

ETI BAADA YA KUACHWA PALE MIGUU NDIYO IKAISHA NGUVU KWA UOGA HAHAHHAHAHA!!!
 
Mi nakumbuka tulikua watoto wanne katika wote mkubwa alikua la tano sisi wengine tupo la kwanza na la pili, tulikodi baiskeli tukaingia nazo Lugalo sasa kuna kibao kimeandikwa hakuna njia ila yule mkubwa wetu kusoma hajui kwahiyo tukaingia tu bila kujua.
Mbele tukakamatwa tukarudishwa hadi kwenye bango na tuliposhindwa kulisoma tukazidi kuwakera, wakaona kumbe hawa ni machokoraa.
Ikafuata adhabu sisi wa la kwanza na la pili maumbo yetu madogo tukapiga pushap kumi, yule mkubwa akaambiwa aibebe baiskeli mgongoni huku anaruka kichura chura, sasa hivi tukikutana tunamtania sana jamaa kua badala ya baiskeli kumbeba yeye, yeye ndiye akaibeba baiskeli.
 
Kama nawaona sura zenu mlivyoshuka wote wanne mikono juu [emoji23][emoji23][emoji23]
Yaaani tulikuwa tunatia huruma ebu fikiria wajeda wakuache hivi hivi weeee......yaani hali ilikuwa mbaya maleria si maleria , homa si homa acha kabisa ila walicheka sana kuona ile style ya kuonyesha mikono juu ka mateka hahahaa aseeπŸ™‚πŸ™‚πŸ˜€
 
Ndo maana mliachwa mlikuwa watoto.
Movie za the hard way et ee?
tena yule nigger ndiyo alikuwa anatutua kiburi kweli tulikuwa tunaona kumbe hata sisi weusi tunaweza kuwa makomandoo sem akaliwa na mamba pale mtoni kaka ke sinema nilikuwa vzr alafu ungekuwa unatuona tunavyochezea kifo kwa kudandia magari mmhh! kwa upande mwingine ungeweza kutupa hata zawadi manake over makomandoo faster like fast furiousπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…