basha unguja
Member
- Sep 28, 2016
- 83
- 77
Wanajamvi kwanza wasaaalam!
Napenda kushare nanyi hii siku ambayo ilikuwa kizungu mkuti lakini yote ikiwa ni utoto plus utundu.
Tukiwa na tabia ya kudandia magari mimi na wenzangu siku moja ilipita gari aina ya TATA kubwa ambalo limefunikwa kwa maturubai kwa nyuma na sehemu ya mlango wa nyuma ikina wazi...Tulipoliona gari linakuja mimi na wenzangu wapatao watatu na mimi nikiwa manne tukalisubiri lipunguze mwendo kwa kuwa barabara haikuwa nzuri sana.
Kweli gari ilipunguza mwendo , kama makomandoo tukadandia kwa ustadi mkubwa, wote wanne tukawa ndani ya gari ..Baada ya hapo tukaridhika kuwa tumefanikiwa sasa issue ikawa kushuka daaaah! dereva ndiyo kwaaaaanza anakanyaga wese....Sasa kwa hofu tuliyonayo tukasema tujifiche mulemule ndani bila kujua gari inaenda wapi...
Baada ya mwendo mrefu gari ikasimama.. tukajaribu kuchungulia nje tukiwa mule ndani kumbe bwana tumeingia kambi ye JESHI daaah! Nakumbuka nilipowaambia wenzangu kuwa tupo ke kambi ya jeshi mmoja kwa upoleee akajisemea tu TOBAAAAA ..
Busara tuliyoitumia ni kushuka wenyewe na kujisalimisha kwa kuoonyesha mikono juu....Wale wanajeshi waliokuwa pale walishangaa huku wengine wakicheka wakiwa hawaelewi kinachoendelea, Dereva naye akashikwa na butwaa...
Tukawa wawazi pale kuwa ndiyo kamchezo ketu ila siku hiyo ilikuwa arobaini yetu ....wakatusamehe wakati wa kurudi tulirudishwa hadi tulipodandia na kuonywa tusifanye tena aseeeee......
ETI BAADA YA KUACHWA PALE MIGUU NDIYO IKAISHA NGUVU KWA UOGA HAHAHHAHAHA!!!