t blj
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 7,035
- 16,705
VXR ni top model ya LC200 series. Unadhani ni sahihi kulinganisha na entry model ya GLS?
Kwenye Calculator ya TRA;
VXR wamewekea CIF ya $72,000 na GLS wameiwekea CIF ya $112,000.
Kodi ya VXR $47,000 na kodi ya GLS ni $73,000.
Kwa mujibu wa tovuti ya toyota.co.za wanaiuza VXR R1,606,600 sawa na $114,034.
Kwa mujibu wa mbusa.com wanauza;
GLS 450 = $77,000.
GLS 580 = $99,000.
GLS AMG 63 = $133,000.
GLS Maybach $160,000.
Na kusema Prado TX ni expensive kuliko GLS unapotosha pakubwa sana. Prado VX.L ambayo ni top model ya Prado Lineup inauzwa $119,000 sawa na Tsh. 279M tena hiyo ni pamoja na kodi.
Na kama unataka kulinganisha top model ya LC200 series na uhakikishe unalinganisha na top model ya GLS na sio uchukue VXR (top model) na GLS 450 (ambayo ni entry model). Sio sahihi.
Majadiliano mazuri ila naona tunatumia source zenye informations tofauti.
Kikokooo cha kodi cha Tra kimekuwa kikilalamikiwa kila mara kwamba hakipo fair kwa baadhi ya items, na mfano mzuri umeuoneshs hapa
Gls huko ulaya ikiwa imelipiwa kodi zote ina thamani ya 77000usd , ila kikokotoo chetu kina sema cif value tu ya Gls ni 112000 usd , hivi tukiendelea na majadiliano katika hali kama hii si tutakuwa tunapotosha watu? Na bahati mbaya kikokotoo chetu hakisemi ni model ipi ya gls , kama ulivyainisha hapo juu.