Hii lazima iwe Tanzania, ndiko huko watu huwa wabishi kiasi hiki

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kuna hii picha imezagaa kwenye mitandao ya Kikenya wengi wakihoji wapi Kenya ambapo kuna watu wabishi hata kwenye upumbavu unaoweza kuhatarisha maisha kiasi hiki.
Mimi nahisi hii picha iko Bongo, huko ndiko walivyo, wabishi hata wanapo ambiwa ukweli hawautaki, hususan hawa hukesha kwenye taarifa za Kenya humu JF.

Hata muundo wa nyumba, za aina hii huwa zipo Tanzania ikiwemo nguzo za umeme, zetu huwa round.
Kenya Power Responds to Viral Photo of Transformer Erected Through House

 










weee tanzania hatuna huo upuuzi


nikuulize mtoa mada umeshaenda kuokota msosi wa siku yaleo jalalani maana nasikia supermarkets zimewashinda mmehamia jalalani sikuhizi?
 
Kali sana. Kenya Power huwa hawatumii nguzo kama hizo, zao zote ni standard moja, za round. Hii lazima itakuwa ni huko huko kwa wajuaji. Jiweland. πŸ™‚

Wabishi sana wale.... Yaani hapo yeye keshajenga nyumba, humwambii kitu na haambiliki na hajaribiwi.
 
Hizo nguzo sio za umeme wa Tz. Zetu ni round wood.
 
sijawahi kuona nguzo ya square huku Tanzania.. Halafu hata iweje TANESCO hawawezi kuweka Transformer juu ya nyumba ya mtu.
 
Unatuonea tu arif. Tanzania hatuna nguzo za umeme za zege...

Jaribu kuotea nchi nyingine.
 
Wabishi sana wale.... Yaani hapo yeye keshajenga nyumba, humwambii kitu na haambiliki na hajaribiwi.
Ukute hapo ni Sumbawanga na mwenye nyumba kwenye garaji lake amepark bonge la uteo. [emoji38] Tanesco subutu!
 
Ha ha ha ha ha ha hakuna nguzo za hivyo huku tz
sisi tunatumia nguzo za miti then ziko round sio kama hizo za zege
hiyo still ni kenya maeneo ya.................
 
Kali sana. Kenya Power huwa hawatumii nguzo kama hizo, zao zote ni standard moja, za round. Hii lazima itakuwa ni huko huko kwa wajuaji. Jiweland. πŸ™‚
Pimbi Nywee, Tanzania hatuna nguzo za pembe 4, tunazo za round na tuna ardhi ya kutosha. Na sisi sio wabishi kwa maana hatuna damu ya kikikuyu.


June 2011



Dec 2014



Aug 2016



Jun 2017

Bado mwaka haujaisha. Huu sasa ndio ubishi wa Nairobi, wallah hilo banda la njiwa hapo likianguka litang'oa hizo nyaya za umeme.
 
Angalau hapo kama ni Nairobi(naona picha zenyewe sijui ni za Zanzibar) kuna uhakika kwamba hizo nyaya zina umeme maanake nyaya za umeme za tanesco huwa ni za kusapoti nguzo tu. .....na mahala pa njiwa kupumzikia. [emoji1]
 
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani leo jumanne Novemba 21, 2017 akiwa Mkoani Pwani katika Wilaya ya Bagamoyo ametembelea kiwanda cha kuzalisha nguzo za zege (Concrete poles) cha East Africa Infrustructure Engineering Ltd. eneo la kidomole, Bagamoyo.

Katika ziara yake Mhe. Waziri amesisitiza agizo lake alilolitoa la kuhakikisha kuwa nguzo zinazotumika zinazalishwa hapa Nchini.

" Nguzo tunazotumia sasa ni za miti ambazo zinaharibu mazingira lakini pia si imara kama nguzo za zege"

Alisisitiza Mhe. Waziri huku akiainisha kuwa nguzo za zege zina uwezo wa kudumu zaidi ya miaka 70.

Aidha, Dkt Kalemani alisema hivi sasa Umeme unaoingia katika gridi ya Taifa ni Megawati 1450 lakini ni nia ya serikali kuwa na Megawati 5000 kufikia 2020.

Alisifu juhudi za TANESCO za kuanzisha kampuni tanzu ya kuzalisha nguzo za zege ya Tanzania Concrete Poles Manufacturing Ltd

(TCPM).

Aliitaja miradi kama ya Stieglers Gorge( Megawati 2000) ambayo imekuja baada ya jitihada kubwa za serikali na kuiagiza TANESCO kuhakikisha kuwa nguzo za zege zinaanza kutumika kufikia mwezi Desemba mwaka huu.

"Kazi yangu ni kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika"

Alisema Dkt. Kalemani.

Katika ziara yake Mhe. Waziri aliambatana na Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Wataalamu wa TANESCO na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Alhaj Majid Mwanga na Mbunge wa Bagamoyo Mhe. Shukuru Kawambwa ambao walishukuru ujio wa Waziri kwani wametaja eneo la Bagamoyo kama eneo kubwa la viwanda ambalo litahitaji umeme wa uhakika.










2017 hiyo na hazijapitishwa kutumika na hazijakubaliwa na hazitatumika zitakuja kwenu ndio mnauziwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…