Hii lodge niliyofikia leo imenikumbusha mwaka 2015 nilipokuwa Arusha field kikazi

Hii lodge niliyofikia leo imenikumbusha mwaka 2015 nilipokuwa Arusha field kikazi

Ujana maji ya moto mimi huwa nalala hotel kubwa ambazo huwa wanawazibiti malaya hatoki hadi upigiwe simu chumbani kuwa unamluhusu huyu atoke hotel za kuanzia 40000 au elfu 50000 zina security unachukua malaya na unalala bila wasiwasi
Wewe ni Mwanaume?
 
Kilete hapa mkuu
Ni aibu tupu.
Niliwahi kuingia gesti moja hapo miaka ya 2009.
Sasa niko na jamaa yangu msukuma na demu wake wa huko Musoma bana.
Tukala vyombo vya kutosha, wakati tunapiga pombe hata nilikuwa sijui tunalala wapi Hapo demu wa mshikaji ndio mwenyeji wetu.

Kuangalia saa inaenda saa 6 usiku. Demu katupeleka lodge(gesti ya ajabu ajabu tu).
Nafasi ilikuwa imebaki ya chumba kimoja tu.
Wakati tunaenda kukiangalia mimi si nikajilaza kwenye kile kitanda mazima!!! Sikunyanyuka tena. Na akili haikusoma network yoyote.

Jamaa na demu wake wakaondoka kutafuta sehemu nyingine wakaniacha pale na mimi sikuwa na uenyeji wowote ule.
Nilishtuka mida ya saa tisa, nimekabwa na kiu isivyokawaida.

Sijui hata reception ni wapi...giza tororo! Nikawasha kisimu changu cha tochi (washukuriwe wachina).

Wenge linanicheza kama lote mwili unatetemeka balaa.
Nikakumbuka jamaa na demu wake. sikuhangaika kupiga simu nikijua ningewasababishia usumbufu.

Kwa shida nikafika reception, mdada anakoroma nikamshtua saa ngapi asipige yowe moja kali, akijua amevamiwa. Mlinzi akafika kulikuwa hakuna umeme. Na tochi yake, akajua ni mteja.

Mlinzi akaanza kunifokea mbaya mbovu, akijua nilikuwa nataka kum'baka yule dada wa mapokezi. Daah!! Nikamcool down na kumweleza kuwa nahitaji maji tu yakunywa.
Wakaniambia hakuna maji pale. Walishanidharau kuwa mimi ni mlevi tu.

Yule mlinzi alinisihi nilale tu hadi kukuche, nilijaribu kulazimisha kutoka kwenda kutafuta maji! Ikashindikana sasa wakati narudi room niliyokuwepo nikaona pipa kwenye kona moja. Mlinzi akawa ananifuata kwa nyuma, nilimtukana kidogo. Mzee lile pipa lilikuwa lina maji! Nikayapiga tena kwa kutumua kikopo kilichokuwepo humo humo.

Niliwasikia kwa mbali tu wakiambiana aisee huyu jamaa kanywa yale maji ya chooni. Sikujali nikaenda kuangusha zangu. Nilikuja kushtuliwa na jamaa yangu saa mbili asubuhi.

Si mchezo Musoma sitapasahau.
 
Like serious! Halafu ukute baada ya kumuabisha mdada wa watu uliendelea kumla 😭😭
 
Hii habari ya kunywa maji ya bafuni imewai kunikuta saizi nimekua mjanja nikiludi kulala chumbani nabeba na maji hasa castle lite zinaleta kiu sana usiku
Kipindi hiko nikinywa bia silewi kabisa!!!
 
Hii lodge nikiyofikia Leo imenikumbusha mwaka 2015 nilipokuwa Arusha field kikazi. Naandika huu Uzi nikiwa hapa Musoma (lodge kapuni), sasa hiki chumba kinafanana sana na kile Cha Arusha (Cha Arusha chumba sio mambo yenu yale wazeiya wa kupulizi)

Anyway ilikuwa hivi, enzi zile ujana mwingiii nimefika zangu Arusha nikatafuta pahala pa kujisitiri (namaanisha kulala sio kujisitiri unakowaza wewe bhana).

Mida mida nikatoka zangu kupata msosi wa usiku. Huku na huku nikajikuta nimetimba Shivaz. Enzi hizo inabamba, Malaya kama wote. Mipombe pombe nikaondoka mida mibovu Sana kumbonji.

Kisanga sasa, naamka asubuhi nakuta chumbani yupo demu (ofkoz ni malaya wa pale Shivaz. Khaa, kujikagua nakuta ndom mbili zimetumika. Cha kwanza nikashukuru alafu ndio nikaanza kujishangaa, yani nimechukua Malaya bila taarifa rasmi ya kushirikisha ubongo wangu. Kichwa cha chini cha kingethe thana.

Sasa yule demu alikuwa ameshaoga na kuvaa tayari kwa kuondoka. Unajua kwanini hakuondoka? Mzee nilijuongeza maana funguo nilificha ndani foronya ya mto niliolalia. Kwaio akawa hana jinsi ya kuchomoka. Mana nililala kizembe sana begi la laptop na waleti vipo tuu mezani. Yule manzi alikuwa anapiga ivo vitu kama sio kujiongeza.

Sasa hapo juu nimekwambia nilikuwa safari ya kikazi inabidi niende field vijijini huko. Kwahiyo pia nilikuwa na mzigo wa ofisi kwaajili ya kulipa watu posho zao na ukumbi si unajua Tena maswala ya masemina semina yalivyo. Nilikuwa kama na m7 hivi cash.

Akili yangu ikanituma ile pesa ipo kwenye begi. Kabla sijamsemesha chochote yule nikawahi kucheki kwanza mzigo upo? Kucheki hivi hola. Pesa haipo. Imeyeyuka. Dadeki. Hapa nikajua manzi keshanipiga. Nilipagawa. Fedha ya Ofisi halafu ndio field yangu ya kwanza pale Ofisini na ajira yenyewe ilikuwa mpya. Balaa.

Nikamwambia yule manzi mami ake leo umebugi. Yani umeingia cha kiume. Mzigo utarudisha. Nilomkomalia balaa halafu nishapagawa. Yule manzi aliapia miungu yote unayoijua hadi Budha lakini wapi. Nikamwambia wewe umewapigia simu wenzio mzigo umetolea dirisha. Anambia muulize mlinzi maana chumba changu dirisha lilikuwa linaangalia kwenye kibanda cha mlinzi. Nikamwambia nyie wote dili lenu moja.

Nikampigia simu dereva wa ofisi niliyesafiri nae akaja. Nayeye akapagawa. Mtiti ukawa ntiti. Demu analia mi namkaba shingo. Wahudumu wakaja, meneja akaitwa. Meneja akanijibu simple sana kwamba bro kuna bandiko kila chumba kama pesa au vitu vya thamani vikabidhi kaunta. Yaani muhudumu wa lodge umkabidhi 7m? Tena 2014? Aisee si amasepa na Kijiji? Nikajua huyu meneja nae dili lao moja nikamuunganisha na mlinzi aliyesema hajamuona mtu. Sasa mbona hela haipo? Nikàmbiwa bro labda utakuwa umehonga yote Mana watoto wa kimbulu waliojazana Arusha si mchezo.

Yule dereva niliyekuwa naye alikuwa na ndugu askari polisi pale Arusha. Akaitwa akaja na Difenda. Wakambeba yule dada na kwa kuwa alikuwa upande wetu akabebwa na meneja, muhudumu wa zamu na yule mlinzi, watu wababe sana ilikuwa ni uonevu kwa kweli. Yule polisi akaniuliza tu unauhakika ulikuwa na hela? Ndio. Ok Kama kweli wameiba watasema tu wacha tukawafinye kidogo.

Sasa bhana, wakati tunatoka nao kwenda kuwafinya kuna kitu kikaflash kwenye akili yangu. Nikamwambia wale polisi hold on. Nikatoka nduki kurudi room. Aisee nilipumua kwa nguvu sana, mzigo si nikauona.

Unajua ilikuwaje? Ni kwamba wakati natoka kwenda kula nilijiongeza. Ule mzigo niliuweka kwenye mfuko wa plastic ile mifuko laini halafu nikauficha ndani ya lile sink la maji ya kuflasihia toilet. Yale masink si huwa yanafunguka kwa kule juu. Basi ndio mzigo nikauhifadhi humo maana najijua nilikuwa nikishalewa naweza naweza beba malaya yoyote ambao ni wezi kama wemesomea. Kwahiyo nikaficha huko mzigo kwa usalama. Aisee Nina akili sana si, ndiyo? Yah, mimi sio fala.

Ikabidi nimuite yule bro polisi. Dah jamaa akacheka sana lakini pia alini-mind kimtindo. Ikabidi meneja wa lodge na yule kahaba waitwe room. Aisee yule manzi alinichapa kelbu moja matata sana. Unaijua kelb? Ni lile kofi la nyuma ya kiganja. Huwa linauma sana ukiotewa lakini ni dharau kubwa sana ukichapwa nalo. Ikabidi niwe mpole tu saa utafanyaje hata kama wewe?

Ustaarabu tunauweza waarabu, au sio? Ikabidi kwanza niwapoze. Yule demu nikamtia na 30, meneja nikamtia na 10, yule polisi nikamtia na 50 akawapoze na wenzake wawili alikuja nao. Halafu nikachukua namba ya yule manzi, usiniulize kwanini ila badae akaja kuwa mshikaji wangu sana. Si unajua mamanzi wa Chuga hawanaga kwere.

Baadaye Sasa nakuja kushtuka kumbe muda wote huwa naendesha mtiti niko na boxa tu. Yaani nazulula makoridoni nipo na boxa, khaa aibu sana!

Sasa nipo hapa Musoma muda huu nahofu yale ya Arusha yasije yakajirudia. I love you mai waifu.
Ha ha ha ha
 
Back
Top Bottom